Urembo Kwa wanawake na Nguvu Kwa wanaume

9mm

Senior Member
Aug 11, 2013
158
90
Habari za muda huu wana jamvi, poleni kwa majukumu na harakati za kila siku za ujenzi wa taifa na kuhakikisha mkono unakwenda kinywani. Bila kuchelewesha muda niende moja kwa moja kwenye mada. Uumbaji wa dunia na vilivyomo ni wenye kupendeza na kutukuka sana. Ila kwa bahati mbaya mwanaadamu hajaliona hilo na hapo ndipo kiumbe huyu msumbufu anapoanzisha balaa kubwa katika kuhakikisha anaboresha muonekano wake, kwa mwanamke ni kuutafuta urembo na mwanaume kuzitafuta nguvu.

Urembo kwa Mwanamke
Kuna usemi unasema “ukitaka kukmkamata mwanamke basi ujue urembo wake”. Yani fanya unachoweza kuongeza hicho kinacho mpendezesha.

Kitu mwanamke anataka ni kuonekana mrembo, binti, mwenye ngozi nzuri, nywele za kupendeza, umbile zuri, miguu, na kila kitu kinacho ugusa uzuri wake, hapo ndipo surgery inapoanza kujipatia umaarufu. Utasikia huyu kapunguza mbavu, mara yule kaongeza lips ili mradi uzuri wake uwe ni wenye kuonekana kwa wote watakao muona au kupita karibu yake.

Hili ni tatizo kwa maana katika mbio ndefu mara nyingi vitu haviendi vizuri au panaweza hitajika maboresho kwa hicho kilicho tengenezwa awali. Akina mama, shangazi mabibi na wasichana kuweni makini na mahitaji ya mioyo yenu.

Nguvu kwa Mwanaume
Katika vitu vyote alivyopewa adam, hakuna kitu ni mali kwake kama Nguvu . Hii ndio iyakayo mfanya aweze kufanya kila linalo mkabili mbele yake. Iwe kumpa huduma mama yeyoo, kutafuta mkate wa kila siku, kulea na hata kwa kuongoza vile anavyo vitawala.

Kila jambo litalo hitaji uwepo wa mwanaume basi nguvu lazima iwepo. Nguvu hii ni ya mwili akili na roho . Nitapenda kuangalia nguvu ya mwili na jinsi tunavyoitumia vibaya.

Wakati wanawake wakiwa na surgery na changamoto za urembo wao, huku kuna wa vumbi la kongo na steroids kwa maana vichochea misuli. Ndugu zangu hivi vitu havipo na tija katika mbio ndefu. Zingatia kula, fanya mazoezi na soma vitabu, hiyo nguvu unayoitafuta utaipata.

Mfano: Umejiandikasha gym halafu mvivu, unataka steroids zikusaidie. Nguvu kidogo matokeo makubwa, mafanikio utayapa kwa muda na pia itakukagharimu pesa bila kusahau hapo baadae athari za kimwili zitajitokeza. Sehemu peke ambapo nguvu inakaa ni penye pumzi, tafuta pumzi utaipata nguvu. Na pumzi inatafutwa kwa mazoezi na si kwengineko inaewa kuwa kwa kukimbia, kuogelea, kuruka kamba, push up na mazoezi mengine mengi yanayohusisha mwili katika mwendo.

Kuna usemi unasema “ukitaka kumkamata mwanaume, basi zingatia kula yake” kwa maana hapo ndipo nguvu inapo anzia sio mifuta kila siku kutiana magonjwa ya moyo na sukari.

Naomba kuwasilisha.

View attachment 2801768View attachment 2801769
 
Back
Top Bottom