Nimerudi mkuu na this time with a lot of research,tujadili:
QUOTE 1:
Genocide zinazokubalika bila kupingwa mfano ya wanazi vs wayahudi zilitokana na chuki tu (ukabila, dini n.k kama ulivyosema), hakukuwa na jeshi la wayahudi popote pale lililokuwa linashambulia serikali ya hitler kijeshi kwa miaka minne likiua raia wasio na hatia kama ilivyo Rwanda.
Sijakataa wahutu wachache kuua watutsi kwa sababu tu ni watutsi kama hao watoto wachanga lakini hiyo ilikuwa ni sehemu ndogo ya vita kubwa ya kikabila ambayo Kagame anataka kutusahaulisha na si a stand alone genocide. Bila vita hivi vikubwa mauaji haya madogo madogo yasingetokea. Kucategorise mauaji haya kuwa genocide ni sawa sawa na kudai vita vya walyanchali na walyanchoka kule Mara (sina uhakika na spelling) nayo ni genocide, mauaji ya wakulima na wafugaji morogoro nayo genocide simply tu kwa sababu ni kabila mbili zinapigana .....sijui Tanzania peke yake tungekuwa na mahakama za genocide ngapi. wachilia mbali mauaji ya chaguzi za kenya,mauaji ya sasa ya kikabila southern sudan etc. Kama ambavyo mifano hii haikidhi status ya genocide ndivyo hivyo hivyo mauaji ya Rwanda 94 hayakidhi kuitwa genocide. Lakini hata hivyo nakaribisha mjadala katika hili kwa sababu mpaka sasa hakuna makubaliano katika tafsiri ya genocide worldwide.
ARGUMENT 1:
Tukianza kwenye red ya kwanza hiyo ndio genocide yenyewe,rejea definition ya genocide niliyokupa na ulikubaliana nayo kwasababu kuna sehemu umeitumia kama ilivyo kujenga hoja zako.
Kwenye red ya pili,mauaji yaliyogusa kati ya watu laki 5 na milioni 1 unayaita madogomadogo?hayo makubwa yaliyofanywa na RPA yaligusa watu wangapi?
Kwenye bold,napata shaka sana na uelewa juu ya mambo haya,kufananisha mauaji haya na ya wakulima na wafugaji morogoro au walyanchali na walyanchoka au yeyote kati ya hayo ni upuuzi sana,situation ya rwanda ilikuwa tofauti sana,kulikuwa na makundi manne kama ifuatavyo:
Kundi la kwanza:
Jeshi la serikali likipambana na jeshi la waasi(kundi la pili) huku likiwa linatoa silaha na kuhusika kwa mafunzo kwa kundi la tatu(hutu extremists) na pia likihusika na mauaji ya kundi la nne.
Kundi la pili:
Jeshi la waasi likipata sapoti kutoka Uganda huku likipambana na kundi la kwanza na kundi la tatu.
Kundi la tatu:
Kundi la wahutu wenye msimamo mkali likipokea msaada wa silaha kutoka kundi la kwanza na lililenga kuua raia wote watutsi,wahutu na watwa walioshirikiana na watutsi(kundi la nne).
Kundi la nne:
Kundi la raia wasio na hatia wala silaha mikononi mwao,kundi hili lilikuwa linahangaika kujificha tu,halikuwa kwenye mapambano na kundi lolote kati ya hayo.Kundi hili liliwindwa na kundi la kwanza na kundi la tatu.Na tunapozungumzia genocide tunalilenga kundi hili tu na sio kundi lolote kati ya hayo mengine.
Sasa hayo mauaji unaweza yafananisha na ya wakulima na wafugaji wa moro?Na hata hivyo source zote za kuaminika na uchunguzi uliofanywa na UN baada ya mauaji umekiri kulikuwepo na genocide Rwanda 1994.
QUOTE 2:
sina ushabiki na kundi lolote. Msimamo wangu binafsi ni kuwa yoyote aliyehusika kufanya uhalifu wowote ule afikishwe mbele ya sheria. simple as that. Tatizo langu mimi ni case kama za FDLR ambao ni wanajeshi wa serikali halali ya Rwanda waliopinduliwa, hawa wanashitakiwa kwa lipi?kudefend nchi kwa mujibu wa katiba? What about Kagame na jeshi lake waliokuwa wanavamia Rwanda kwa miaka minne, mbona wao hawashtakiwi? je hawakuua watu (ambao 99% ni wahutu by the way)? Ndio maana wenye akili wote kama Kikwete tunaona njia sahihi ni mazungumzo. Watu wote washitakiwe kulingana na makosa yao.
ARGUMENT 2:
Hapo kwenye ushabiki sina shaka na hilo,mfano angalia unavyowasafisha FDLR hapo kwenye maelezo ya mbele,unajua kuwa 90% ya watu wa kundi hili hasa viongozi wanatajwa kuhusika na mauaji hayo?FDLR watashtakiwa kwa kuhusika kwao na mauaji hayo.
Unataka kusema walipokuwa wanaua wananchi wasio na hatia makanisani,mashuleni na barabarani kwa kuweka road blocks na kukagua ID au kuangalia kama wana-appear kwenye list ya wanaotakiwa kuuawa, ikiwemo vitoto vichanga walikuwa wanadefend nchi yao?Kipi kinakufanya uamini hawa walikuwa wanajeshi halali?Unafahamu kama na wenyewe waliingia madarakani kwa mtindo huohuo waliotolewa?Na kama ni halali kwanini walihusika na mauaji ya raia wasio na hatia badala ya kuwalinda.
Kagame na jeshi lake watashtakiwa kwa war crimes kama itabainika walifazifanya katika mchakato wao wa mapigano,Nikubaliane na wewe kuwa rwanda needs reconcillation lakini hiyo iendane na bold ya mwisho uliyoweka,kila mtu ashtakiwe kwa makosa aliyofanya.
Nakukumbusha tena tunapoongelea mauaji ya kimbari tunamaanisha kundi la nne,rejea ulitizame upya.
QUOTE 3:
kwa observation yako mwenyewe: paul rusesabagina ni mhutu lakini neutral kwa ukabila, kawasave watutsi (wajomba zake na wakwewe), lakini upande wa pilimtutsi pure Robert Kajuga kaongoza kundi la interahamwe kuchinja watutsi wenzie, hujiulizi how come? Maana kama mhutu anamlinda mtutsi, lakini mtutsi anaongoza wahutu kuua watutsi hapo hakuna genocide kuna conspiracy to frame the hutus. Hebu fikiria inavyosikitisha inawezekana baadhi ya watutsi waliolindwa na rusesabagina walikuwa wanakimbia kundi la interahamwe likiongozwa na mtutsi mwenzao aliyebeba ID ya kihutu!
ARGUMENT 3:
Kwenye bold zote ulilenga kutuaminisha kitu kimoja tu,kuwa watutsi waliuua watutsi wenzao kupitia interahamwe na wahutu waliokoa watutsi wasiuawe na watutsi wenzao baasiii,umetumia wahusika wawili tu kuthibisha hilo Rusesabagina na Kajuga.
Kwanza kabisa sio wahutu wote waliohusika na huu ushetani wa kuua raia wasio na hatia,si sahihi kabisa kuhukumu jamii nzima kwa kutumia kundi la watu,wahutu waliohusika sio aina ya rusesabagina ambao walikuwa na damu,uhusiano na mtizamo wa kawaida kwa watutsi,wahutu waliohusika ni wale extremists tu.
Tukirudi kwa
Kajuga huyu alikuwa rais wa interahamwe lakini sio muanzilishi wa kundi,duru huru zinamtaja
Theoneste Bagosora(hutu extremist aliyeplay part kubwa sana ya mauaji haya lkn nashangaa hujawahi muongelea)kama muanzilishi wa kundi hili na kama ni conspiracy basi ilianzia kwa mtu huyu, pia zinamtaja
Georges Rutaganda(makamu wa rais wa interahamwe)kama aliyehusika zaidi na mauaji ktk kundi hilo kuliko mtu yeyote,Prosecutor James Stewart alimzungumzia hivi, "
Without Georges Rutaganda, the Rwandan genocide would not have functioned the way it did."He was on radio RTLM in Kigali in 1994, encouraging Interahamwe Militia to exterminate all Tutsis.
Halafu natizama list yote ya interahamwe sioni mwingine aina ya
Kajuga,kama yupo unaweza leta jina lake hapa?Kama hayupo tambua kuwa si sahihi kuhukumu jamii nzima kupitia mtu moja tena mwenye utata rejea ktk historia yake,halafu nakuuliza swali kwanini alichukua ID ya wahutu wakati yeye ni mtutsi?
Kwenye red,mkuu unakumbuka uliwahi kusema interahamwe lilikuwa kundi la vijana la kisiasa na sio kundi la mauaji?Sasa umekubali kuwa lilikuwa linamalengo zaidi ya siasa?
QUOTE 4:
of course kitu kama interahamwe kilikuwa manipulated kupitia infiltration na mamluki, in such a way kwamba watendaji wanaoonekana walikuwa wahutu, hivyo ni vigumu kung'amua idadi ya watutsi humo , hata wewe mwenyewe si umeona kuwa RAIS wake alikuwa anaji-identify kama mhutu?
Pili, kagame anatumia wenzake kama condom, hivyo kufungwa kwa kajuga kusikufanye kudhani kuwa kagame yuko fair! he does not need him any more ni kama vile alivyowatumia kina Bosco ntaganda, Laurent Nkunda, m23 etc. wakishamaliza uthamani wao basi tena.
ARGUMENT 4:
Kwenye blue nilikuuliza swali rahisi tu,majina ya watutsi waliohukumiwa au wanaotafutwa na ICTR tofauti na
Kajuga kwa kuzingatia maelezo yako kuwa wenyewe ndio waliuwa watu kupitia interahamwe na wahutu walihusika kuokoa watutsi wasiuawe na watutsi wenzao(rejea jinsi ulivyowazungumzia Kajuga na Rusesabagina),kama unayo yawasilishe walau hata machache tu,kama huna basi tuendelee kuamini kuwa awapo wengine na ukumbuke kuwa ni karibu miaka 20 sasa tangu mauaji yatokee na kama Kajuga aliweza kujulikana maana yake hata wengine wangejulikana.Au tuamini kuwa yeye pekee ndio alihusika na mauaji ya watu wote? Pia,tusiruhusu sana kutawaliwa na hisia hasa ktk jambo kama hili liliogusa maisha ya watu takribani milioni 1.
Kwenye bold, nakukumbusha tusitawaliwe sana na hisia katika suala hili,come with evidence(kama zipo),kutoka vyanzo huru.
QUOTE 5:
Nchi iliingia kwenye machafuko baada ya ndege ya rais habyarimana kutunguliwa na majeshi ya waasi wa RPA wakiongozwa na kagame. Jeshi lilikuwa bize kupigana na Majeshi ya kagame yakisaidiwa na majeshi ya Uganda. Hawakuweza kuzuia hisia za raia wahutu wachache (baadhi yao wakiwa ndani ya majeshi yenyewe) kulipiza kisasi kwa watutsi at the same time. Narudia tena wachache kumbuka takwimu watutsi walikuwa less than 15%, hivyo hata wakiuawa 2 lazima wataonekana ni wengi tu, katika nchi ambayo zaidi ya 80% ni wahutu.
nani alizuia yasiendelee? well, yaliisha kwa sababu VITA viliisha kagame akiwa mshindi (sadly), hayakuisha kwa sababu kagame aliyazuia. Kagame was fighting Rwanda since 1990, hivyo obviously sababu ya yeye kupindua Rwanda haina uhusiano wowote na kuzuia 'genocide'.
ARGUMENT 5:
Tuanze kwenye green hapo,source zote huru nilizotembelea zinasema hakuna upande uliothibitika kuhusika na mlipuko wa ndege hiyo,kila upande unalaumu upande wa pili,je kwa kusema ndege hiyo ililipuliwa na RPA haikufanyi wewe kuwa wa upande pinzani wa RPA?Lakini ktk utetezi wako moja humu,ulisema RPA walihusika na mauaji yote ya mto kagera kwasababu wao ndio walikuwa wanacontroll eneo lote hilo(bahati mbaya sijaona kitu kana hicho wakati natafuta kwenye mitandao,nategemea utanisaidia kwa hili kwa kunipa source huru na za kuaminika),
sasa if it was about who was where,je ufikiri kuwa unawa-clear RPF kwenye hili?Kwasababu ndege ililipuliwa Kigali tena karibu na uwanja wa ndege,na ukumbuke Kigali was under the gvt forces kwa wakati huo.
Kwenye blue wewe ni muongo,unataka kutuaminisha kuwa mlipuko huo uliendana na RPF kuvamia eneo lote la nchi,kitu ambacho uchunguzi wangu umebaini ni tofauti,wacha nikupe mfano moja kwa kutumia eneo la Kigali,ndege ililipuliwa tar 6 April na mauaji yakaanza usiku huohuo tena ktk taarifa ya UN inasema mauaji yalianza ktk muda usiofika nusu saa toka ndege ilipolipuliwa na watu wa kwanza kutajwa kuhusika na mauaji haya ni members of presidential guards, karibu kabisa na mlipuko ulipotokea,hapa ukumbuke kuwa RPA walishaweka silaha chini kupisha mazungumzo ya Arusha na walikuwa sehemu za mipakani na Uganda na kama ni mapigano na serikali basi walikuwa wanapigania huko na sio kigali,na kwa uchunguzi wangu RPA waliingia Kigali mwezi July,hapa ni miezi 3 baada ya mauaji kuanza,sasa serikali Kigali ilifanya nini kuzuia mauaji haya?Na hata hivyo mahakama ilimpata na hatia waziri mkuu wa nchi hiyo wakati wa mauaji
Jean Kambanda kwa kuhusika na mauaji hayo na kuhukumiwa kifungo cha maisha.
Na kwenye blue ya pili,sio kweli kuwa ni sehemu ndogo tu ya jeshi ilihusika na mauaji hayo,uchunguzi wangu umebaini ni jeshi zima la rwanda likiongozwa na
Theoneste Bagosora lilihusika sio tu kuua,bali kupanga mauaji hayo siku nyingi kabla ikiwemo kuanda list ya watu wote wanaopaswa kuuawa.Kuna ushahidi juu ya hilo,bado naukusanya lakini hata uliopo unatosha kabisa kuwatia hatiani,kama unahuitaji ntauweka hapa.
Fatilia link hii ktk website ya UN utaona baadhi ya hayo niliyoandika :
Rwanda: A Brief History of the Country - Outreach Programme on the Rwanda Genocide and the United Nations
Tukihamia kwenye red ya kwanza,hapo umenisikitisha sana,
Do you think the value of life of human being is determined by numbers?hao wachache waliouliwa unaweza kuwarudishia uhai wao?Na hata hao wengi,wala uonyeshi kujali uhai wao uliopotea,mfano hakuna sehemu yoyote unayotoa suggestion ni namna gani mauaji haya yasitokee,wewe unachosisitiza humu ni habari ya wengi na wachache,
ni dhahiri kuwa unataka ufahari au huruma ya kufiwa na wengi na sio vinginevyo.Na kama wao walikuwa wachache sana kiasi wakifiwa wawili inaonekana ni wengi sana mbona waliwaenyesha namna hiyo tena kwa miaka 4 na mwisho wakawa washindi?
Lakini wacha tutumie takwimu ulizotoa na ambazo mimi nimezipata sehemu nyingine(huru),hadi kufikia mwaka 1993 Rwanda ilikuwa na watu wanaokadiriwa kufika 8 milioni,ukifanya hesabu hapo kwa 14% unapata watutsi wanaofikia 1,120,000 hivi,na kwa kadirio la mauaji ya watu laki 5 mpaka milioni ni kitu kinachowezekana kabisa,ukuzingatia mauaji haya yalihusisha pia wahutu na watwa walioshirikiana na watutsi kwa mambo ya kijamii kama kuoana.
Kwenye vita kuisha,vp kama ingekuwa vice versa hali ingekuwaje?yaani namaanisha majeshi ya serikali yangeshinda,na tafadhali usifananishe mauaji haya na 1959,ukumbuke kuwa 1959 hakukuwa na list ya watu wanaotakiwa kuchinjwa na hakukuwa na interahamwe na mpasuko miongoni mwa jamii haukuwa kubwa kama 1959.
Na hapo nilipopigia mstari,so umekubali kuwa kulikuwa na genocide?
QUOTE 6:
- Baadhi ya raia wa kawaida ambao ni wahutu, wenye hasira kali kulenga watutsi wote bila kujali, kulipiza kisasi cha kutunguliwa ndege ya Rais (mhutu) na kuvamiwa nchi na jeshi la kitutsi la kagame.
- Jeshi la RPA likiongozwa na Kagame kulenga wanyarwanda wote lengo likiwa kupindua nchi na kuchukua madaraka ikiwa ni muendelezo wa mashambulizi yao toka mwaka 1990.
- Jeshi la nchi ya Rwanda wakati huo (ambao leo hii linaunda sehemu kubwa ya FDLR): kuua askari wa RPA katika mapambano halali ya kulinda nchi ya Rwanda kama wajibu wao kwa mujibu wa katiba. Askari wa Kagame wa RPA ni watutsi, wakati jeshi la nchi liliundwa na majority wahutu.
- Kiasi kidogo cha askari wa jeshi la Rwanda ambao wali-commit war crimes against tutsi, idadi yao kubwa ilikuwa inapambana na RPA.
swala la mafuvu milioni moja kama ni watutsi au wahutu lilishawahi kufanyiwa utafiti na takwimu zilipotolewa serikali ya kagame ikazikataa. yenyewe ilidai kuwa wahutu ambao ni missing ndio waliocommit mauaji wakakimbia, lakini watutsi ambao ni missing ndio wameuawa! Matokeo yake there are more hutu missing kutokana na genocide kuliko watutsi, lakini somehow maiti zooooote officially ni za watutsi, sasa uliza walijuaje utaishia kama ingabire!
ARGUMENT 6:
Kwenye blue nakukumbusha tena dunia inapoongelea na kukumbuka genocide tunamaanisha lile kundi la nne la raia wasio na hatia tu na si vinginevyo.
Kwenye green;where did you find this?nategemea utanipa source huru isiyo na maslahi na upande wowote.
HITIMISHO LANGU:
Kwakweli napata uvivu kuchangia sana post ya namna hii ukizingatia mingi ya michango yetu haitoi suggestion ya nini kifanyike kuzuia mambo haya zaidi ni kama tunabeza waliouawa,mfano mtu anapo-denie kuwa hii haikuwa genocide.
Na wengi wawachangiaji wanapoonekana kuwa na chuki baina yao makundi mfano kama mada yenyewe ilivyoanza "Uraia wa watutsi",ukijiuliza hata kwa akili za kawaida unaweza kupata sababu ya kusambaa kwao,halafu muanzisha mada mwenyewe anapowafananisha watutsi na
masultani au
wakoloni(invaders) na sio
waafrika wanyarwanda,allegation kama hii nimekutana nayo katika upekuzi wangu,kwenye kitu kilichokuwa maarufu sana miongoni mwa jamii za wanyarwanda hasa
hutu extremists kilichoandaliwa na
Hassan Ngeze 1990 kilichojulikana kama
"Ten Hutu Commandments" ambacho baadae kilikuja kuwa basis ya kutengeneza
"Hutu Power Ideology" sasa nakuwa nashaka sana na mtu ninayejadiliana nae,halafu ktk akili za kawaida,Tanzania tukiona mtu anashepu ya kitutsi ndio tunawaita wanyarwanda regardless wawe wametokea rwanda or not,lkn mtanzania mwingine anasema ni invaders,how comes?
Hata hivyo haimaanishi nimekuvua Utanzania wako,usinielewe vibaya mkuu,sitaki kukuhukumu kwa vitu nisivyo na uhakika navyo,tujadili taratibu.