Gazeti gani limetoa hiyo habari Meku? Kuwa muwazi kidogo
Sasa huyo SIOI awapo Tanzania anakuwa na muhuri wa Tanzania kwenye Passport yake ya Kenya?..............hii ni vita vya 2015 kwani naamini bila shaka huyo kijana ana PASS YA KUSAFIRIA ya Tanzania hivyo swala kwamba si raia ni kwa sababu tuu Mh. Lowassa yuko nyuma yake
hakuna swala la raia wa nchi mbili au tatu sheria zipo wazi, ukizaliwa nje ya Tanzania na wazazi wa Tanzania initially unakuwa na urai wa nchi mbili ulikozaliwa na Tanzania ukifikisha miaka 18 unatakiwa ukane uraia mmoja na kubaki na mmoja usipofanya hivo automatically unapoteza uraia wa Tanzania hivo huyu mheshimiwa kama hakukana uraia wa Kenya alipotimiza miaka 18 basi kwa sasa ni raia halali wa kenya na anaishi hapa kinyume cha sheria hivo anatakiwa sio kunyimwa kugombea ubunge tu bali kufikishwa mahakamani kujibu shtaka la kuishi nchini kinyume cha sheria!!
Feedback, japo sina chama na Chadema naikubali sana tuu, ila kwenye uchaguzi wa Arumeru, nasimama na Sioi na machalii wote wa AR wako nyuma yake!. Asipopitishwa na CC leo, ile kambi yote ya Sioi, watashiriki kampeni za CCM, ila kura Chadema!. Kiuhakika bila Sioi, CCM itaangukia pua!.
Igunga RA ni muoga kama kunguru siku za mwisho alijitokeza kuokoa jahazi, Sioi asipopitishwa Mmeru No. 1 hatatia mguu Arumeru!, CCM ni kifo cha mende straight away!.
Igunduliwe na nani EMT hawa hawa CCM?, tatizo hapa si uraia wa Sioi ila wameona hauziki hapa zinazitafutwa sababu tu za kumridhisha yeye na wafuasi wake kuhusu kuenguliwa, kwa vile CCM wana uwezo kabisa wa kusema juzi aliukana uraia wa Kenya and no one can question.
Hakuna kesi ya uraia hapa labda kwa kujifurahisha tu.
Huyo kijana amezaliwa baada ya Uhuru wa Tanganyika na baba yake wakati anamzaa alikuwa ni raia wa Tanzania. Huyu ni mtanzania piga ua labda tu awe amechukua uraia wa nchi nyingine alipokuwa mdogo.
Kuzaliwa nje ya Tanzania na mzazi mmoja Mtanzania hakukuondolei wewe Utanzania wako.
hao wanaoleta tetesi hata hawajui sheria za uraia za Tanzania zinasema nini.
Hii sheria ya uraia inatamka wazi juu ya hili.
Every person born outside the United Republic on or after Union
Day shall, with effect from the date of his birth, be deemed to have
become and to have continued to be, and with affect from the commencement of
this Act shall become and continue to be, a citizen of the United
Republic if at the date of his birth his father or mother is or was a citizen
Republic on or after Union of the United Republic otherwise than by descent, subject to the provi
sions of section 30.
Mkuu unataka kutuambia baada ya wiki moja kampeni kuanza kama ukiona upepo haufai utambadilisha?, kina cha maji hakipimwi ukiwa ndani ya maji huu ndio wakati mwafaka wa kupima mgombea yupi anafaa kama wanavyofanya sasa CCM.Analysis yako imeshindwa kunitoa tongotongo.Imejaa ushabiki,tusubiri vyama vyote vikamilishe kutoa wagombea,tupime upepo wa kampeni walau wiki ya kwanza
Possibly.Au wanamfanyizia Lowassa kiana?
Asante Mkulima kwa kutuletea kifungu hiki, watu wanafikiri uraia wa Sioi una utata, tatizo lilopo huko CC and always has been ni maslahi ya pande zinazovutana.Hakuna kesi ya uraia hapa labda kwa kujifurahisha tu.
Huyo kijana amezaliwa baada ya Uhuru wa Tanganyika na baba yake wakati anamzaa alikuwa ni raia wa Tanzania. Huyu ni mtanzania piga ua labda tu awe amechukua uraia wa nchi nyingine alipokuwa mdogo.
Kuzaliwa nje ya Tanzania na mzazi mmoja Mtanzania hakukuondolei wewe Utanzania wako.
hao wanaoleta tetesi hata hawajui sheria za uraia za Tanzania zinasema nini.
Hii sheria ya uraia inatamka wazi juu ya hili.
Every person born outside the United Republic on or after Union
Day shall, with effect from the date of his birth, be deemed to have
become and to have continued to be, and with affect from the commencement of
this Act shall become and continue to be, a citizen of the United
Republic if at the date of his birth his father or mother is or was a citizen
Republic on or after Union of the United Republic otherwise than by descent, subject to the provi
sions of section 30.
mimi ni chadema, kwa uraia wa sioi sina tatizo mana huyu bwana kazaliwa ubalozini kenya,baba yake alikuwa afsa kule,sheria za kimataifa zinatambua ofisi let say ya ubalozi wa tanzania huko zambia ni si ardhi ya zambia.kwa mfano pale ofisi ya Us pale msasani peninsula ni ardhi ya marekani.leteni hoja
Nimemfahamu marehemu Jerry Solomon Sumari kwa muda, sikumbuki kama aliwahi kufanya kazi kwenye ubalozi wetu huko Kenya!! Swali ni kwanini SIOI mwenyewe hakujaza sehemu ya uraia wake kwenye form yake?