Uraia wa Sioi utata mtupu,CCM kutangaza mgombea mpya ARUMERU leo!!

jamani mimi nimezaliwa namanga ni raia wa wapi? upande wa tanzania hakuna matibabu mazuri ikabidi mama yangu avuke aende upande wa kenya kwenye matibabu afadhali. sasa ninataka kugombea udiwani lakini sina uhakika na chama changu cha magugumaji wataniacha kweli?
Teh teh teh teh teh!mkuu wewe ni mkenya,
Ila bado hujachelewa,kama vp nenda pale uamiaji Arusha kaukane ukenya wako kabisa.
 
Naona wanaendelea kumfuata fuata Lowasa na kuna wadau walisema uyo kijana kaoa kwa EL!
Yetu macho!
 
Ngoma inogile,wakimpitisha yeyote chadema tulivyojipanga haitasaidia.wote sagamba sio sioi ama sarakikya ar da same
 
Una maana raia wote wa kigeni wakamatwe au?
Huyu kesi yake ni special one sio ya kukamatwa, bali kufuata taratibu za uhamiaji ili kuubariki uraia wake, na hapa ndipo hoja ya kuwa na uraia wa nchi mbili inapozidi kupata nguvu, mkumbuke haya sio mambo ya kisiasa tu bali hata Kally Ongala, Maximo alisitisha kumtumia Taifa Stars kwa sababu anatumia British passport.
 
Feedback, japo sina chama na Chadema naikubali sana tuu, ila kwenye uchaguzi wa Arumeru, nasimama na Sioi na machalii wote wa AR wako nyuma yake!. Asipopitishwa na CC leo, ile kambi yote ya Sioi, watashiriki kampeni za CCM, ila kura Chadema!. Kiuhakika bila Sioi, CCM itaangukia pua!.

Igunga RA ni muoga kama kunguru siku za mwisho alijitokeza kuokoa jahazi, Sioi asipopitishwa Mmeru No. 1 hatatia mguu Arumeru!, CCM ni kifo cha mende straight away!.

Wamsimamishe hata kama ikigundulika sio raia wa Tanzania?
 
Sheria ni msumeno hivyo basi kama premji,bashe na wengineo walipita katika makali haya sioi naye lazima apite katika hili! Precedent factor! Sarakikya vs nasari arumeru mashariki. Funzo tunalolipata hapa tuache kukurupuka tufanye tathmini ya kina kabla ya kuliendea jambo fulani tena kwa papara1
 
Ha ha ha haaaa! Naona atakuwa raia wa India, si kazaliwa katika ardhi ya India?
At present all children born in the USA are automatically citizens of the United States. This applies even if one or both parents are not themselves US citizens – they could be illegal immigrants, tourists, students, or legal immigrants temporarily working in America. In many other countries birthright citizenship does not exist; babies born in countries such as the UK or Japan do not automatically become citizens as their status depends on the citizenship and immigration status of their parents.

 
Kama uchaguzi utakuwa huru na wa haki....tume ya uchaguzi kuto mbeba mgombea wa ccm:
CCM kushinda Arumeru ni sawa na Ngamia kupita kwenye tundu la sindano....Time will tell
 
Hakuna kesi ya uraia hapa labda kwa kujifurahisha tu.

Huyo kijana amezaliwa baada ya Uhuru wa Tanganyika na baba yake wakati anamzaa alikuwa ni raia wa Tanzania. Huyu ni mtanzania piga ua labda tu awe amechukua uraia wa nchi nyingine alipokuwa mdogo.

Kuzaliwa nje ya Tanzania na mzazi mmoja Mtanzania hakukuondolei wewe Utanzania wako.

hao wanaoleta tetesi hata hawajui sheria za uraia za Tanzania zinasema nini.

Hii sheria ya uraia inatamka wazi juu ya hili.

Every person born outside the United Republic on or after Union
Day shall, with effect from the date of his birth, be deemed to have
become and to have continued to be, and with affect from the commencement of
this Act shall become and continue to be, a citizen of the United
Republic if at the date of his birth his father or mother is or was a citizen
Republic on or after Union of the United Republic otherwise than by descent, subject to the provi
sions of section 30.
 
Wamsimamishe hata kama ikigundulika sio raia wa Tanzania?
Igunduliwe na nani EMT hawa hawa CCM?, tatizo hapa si uraia wa Sioi ila wameona hauziki hapa zinazitafutwa sababu tu za kumridhisha yeye na wafuasi wake kuhusu kuenguliwa, kwa vile CCM wana uwezo kabisa wa kusema juzi aliukana uraia wa Kenya and no one can question.
 
Huyu kesi yake ni special one sio ya kukamatwa, bali kufuata taratibu za uhamiaji ili kuubariki uraia wake, na hapa ndipo hoja ya kuwa na uraia wa nchi mbili inapozidi kupata nguvu, mkumbuke haya sio mambo ya kisiasa tu bali hata Kally Ongala, Maximo alisitisha kumtumia Taifa Stars kwa sababu anatumia British passport.

hakuna swala la raia wa nchi mbili au tatu sheria zipo wazi, ukizaliwa nje ya Tanzania na wazazi wa Tanzania initially unakuwa na urai wa nchi mbili ulikozaliwa na Tanzania ukifikisha miaka 18 unatakiwa ukane uraia mmoja na kubaki na mmoja usipofanya hivo automatically unapoteza uraia wa Tanzania hivo huyu mheshimiwa kama hakukana uraia wa Kenya alipotimiza miaka 18 basi kwa sasa ni raia halali wa kenya na anaishi hapa kinyume cha sheria hivo anatakiwa sio kunyimwa kugombea ubunge tu bali kufikishwa mahakamani kujibu shtaka la kuishi nchini kinyume cha sheria!!
 
Back
Top Bottom