Uraia wa Sioi utata mtupu,CCM kutangaza mgombea mpya ARUMERU leo!!

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,113
930
Uraia wa SIOI utata mtupu,CCM kutangaza mgombea mpya ARUMERU leo.
Chanzo:magazeti ya leo.

============

Updates:

Wakuu nimerudi na taarifa kamili sasa.
Taarifa kamili ni kwenye GAZETI LA MWANANCHI la leo uk4.

Tafuteni gazeti hili ili mpate taarifa kamili.
 
Akili zako sawa sawa kabisa na spika mwenyewe bi kiroboto. Sasa umeandika nini hapo? Sawa bwana. Naona umeweka chemsha bongo. Kazi kwetu wachangiaji. JF Tuwekeeni jukwaa la chemsha bongo.
Ngoja nifatilie hili gazeti then ntawajulisha mkalichukue.
 
ili mradi tu uwe wa kwanza kuweka habari humu...tunasubiri maelezo yako
 
Mkuu ngoja nikalicheki hili gazeti kisha ntakujulisha.

Wanajamvi! Mh. Spika kasema kweli kuwa magazeti ya leo ndo yameandika kuwa Sioi sio raia wa Bongo kwani alizaliwa Kenya! Kwa hilo sibishi ila naomba nami niulize swali! Je kama mama kaenda kutibiwa India (kama kawaida ya viongozi) kisha akajifungua mtoto huko huyo mtoto atakuwa raia wa India?! Wanajamvi nisaidieni!
 
Ha ha ha haaaa! Naona atakuwa raia wa India, si kazaliwa katika ardhi ya India?
 
Wakuu nimerudi na taarifa kamili sasa.
Taarifa kamili ni kwenye GAZETI LA MWANANCHI la leo uk4.
Tafuteni gazeti hili ili mpate taarifa kamili.
 
sarakikya ndo mgombea wa jimbo hilo.........kuna fitna imaeandaliwa
 
Wanajamvi! Mh. Spika kasema kweli kuwa magazeti ya leo ndo yameandika kuwa Sioi sio raia wa Bongo kwani alizaliwa Kenya! Kwa hilo sibishi ila naomba nami niulize swali! Je kama mama kaenda kutibiwa India (kama kawaida ya viongozi) kisha akajifungua mtoto huko huyo mtoto atakuwa raia wa India?! Wanajamvi nisaidieni!

Navyojua (Not 100% sure) mimi ni baadhi ya Nchi kama USA, wazazi wa kitanzania pindi ambapo watazaa mtoto wakiwa USA, Mtoto anakuwa raia wa US. Na kwakuwa kuwa Tanzania haina uraia wa nchi mbili hivyo hata akija TZ inabidi aukane uraia wa USA ndipo awe na sifa ya urai wa TZ.

Kwa swala la India nakumbuka aliyewahi kushinda ubunge katika uchaguzi mdogo Kigoma mmjini 1992 (Premji wa CCM) dhidi ya Dr Kabour wa CDM ...Ushindi wake ulifutwa na Mahakama baada ya kuwa wazazi wake walikuwa bado na sifa ya uraia wa India na mahakama ilisema Premji alitakiwa aukane uraia wa India pindi alipofika umri wa Miaka 18 (akufanya hivyo) hii ni kutokana na yeye Premi kuwa na sifa za uraia wa nchi mbili ambapo ni kinyume na Katiba ya Tanzania.

Angalizo: Elimu inatakiwa katika swala la Urai maana tunaweza kukosa viongozi wazuri kisa Urai na mara nyingine makosa sio yao bali wazazi.
 
Wanajamvi! Mh. Spika kasema kweli kuwa magazeti ya leo ndo yameandika kuwa Sioi sio raia wa Bongo kwani alizaliwa Kenya! Kwa hilo sibishi ila naomba nami niulize swali! Je kama mama kaenda kutibiwa India (kama kawaida ya viongozi) kisha akajifungua mtoto huko huyo mtoto atakuwa raia wa India?! Wanajamvi nisaidieni!
Sifa ya kwanza ya uraia wa binadamu yoyote ni pale alipozaliwa. Hii inaitwa "birth right". Hivyo mtoto anapozaliwa anakuwa na uraia wa alipozaliwa na uraia wa wazazi wake by proxy. Anapofika "majority age" kwa Tanzania ni miaka 18, anatakiwa kuukana ule uraia wake wa kuzaliwa na kuuchagua uraia wa wazazi wake, au aukane uraia wa wazazi wake na kuutumia uraia wa nchi alipozaliwa!.

Vivyo hivyo mtoto akizaliwa Tanzania na wazazi wake au mmoja wa wazazi wake sio raia by the time anazaliwa, anakuwa ni raia wa Tanzania by birth right na uraia wa wazazi by proxy. Akifika umri wa miaka 18, anatakiwa kuukana ule uraia wa wazazi wake ili abaki na Utanzania, hivi ndivyo walivyo mfanyia Bashe, Azim Premji, Balozi Bandora, Generali Ulimwengu etc.
 
Hii itasaidia kuokoa pesa zetu!! Mawaziri wajawazito hawataenda kutibiwa India.
 
sarakikya ndo mgombea wa jimbo hilo.........kuna fitna imaeandaliwa

Fitina ni kawaida ya CCM, Huyu yupo karibu na EL wakati huo huo kiukweli Lowassa hatakiwi na fungu fulani ndani ya CCM, kwa kifupi ngoma inayotaka kuchezwa hapa ni ile ile type ya Bashe-Nzega
 
Sasa huyo SIOI awapo Tanzania anakuwa na muhuri wa Tanzania kwenye Passport yake ya Kenya?..............hii ni vita vya 2015 kwani naamini bila shaka huyo kijana ana PASS YA KUSAFIRIA ya Tanzania hivyo swala kwamba si raia ni kwa sababu tuu Mh. Lowassa yuko nyuma yake
 
Back
Top Bottom