Uraia wa Sioi utata mtupu,CCM kutangaza mgombea mpya ARUMERU leo!!

Magazeti ya leo yameandika kuwa Sumari ana asili ya kenya so anatakiwa ajieleze.Kugombea kupitia CCM kuna hitaji moyo mgumu.
 
sasa hii ndo taarifa kamili? mtu unakua mvivu mpaka kuandika ulichosoma kwenye gazeti duuh wabongo bana.
 
Sio raia walimchaguaje wazee hawa kwa zengwe baadae utasikia asaidie kampeni, raia wa nje anaweza kusaidia kampeni upinzani?
 
Wanajamvi! Mh. Spika kasema kweli kuwa magazeti ya leo ndo yameandika kuwa Sioi sio raia wa Bongo kwani alizaliwa Kenya! Kwa hilo sibishi ila naomba nami niulize swali! Je kama mama kaenda kutibiwa India (kama kawaida ya viongozi) kisha akajifungua mtoto huko huyo mtoto atakuwa raia wa India?! Wanajamvi nisaidieni!

Atakuwa raia wa india mkuu, si ndo alikzaliwa. Na issue hii iliwatesa sana waingereza maana wanawake wengi wa kinaijeria walikuwa wakienda uk kila mimba zao zilipokuwa na miezi saba hadi nane ili wakizalia uk, watoto wanakuwa waingereza hadi hapo baadae watakapoamua kuukana huo uraia wa uk na kuchukua wa mama
 
Ktk uzi unaosema 'Sioi akataliwa arumeru' wa jana nimesema, km Hussen alibwagwa chn, then Sioi naye anatupwa nje! Ilikuwa rushwa, then uraia, hahahaha! ZIDUMU FIKRA ZA M/KITI WETU WA CCM, na NAPE OYEEE
 
CCM yataka kumtosa mtoto wa Sumari Arumeru.
MCHAKATO wa kumpata mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki umefikia katika wakati mgumu baada ya Sekretarieti ya chama hicho taifa kupendekeza mshindi wa kura za jimbo, Sioi Sumari atoswe kwa madai kwamba uraia wake una utata.

Sekretarieti ya CCM ilikutana Dar es Salaam jana na mapendekezo yake yamewasilishwa kwa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho inayoketi leo kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu nani atapewa jukumu la kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Aprili Mosi.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho cha sekretarieti, zilisema uamuzi huo ulikuwa na sababu kuu mbili, utata wa uraia wa Sioi na kutoungwa kwake mkono na wagombea wenzake aliowashinda katika kura za jimbo... "Wanasema kwamba, Sioi ana elimu nzuri lakini uraia wake una utata."

Mkutano Mkuu wa jimbo hilo uliofanyika Februari 20 ulimchagua Sioi, mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Jeremiah Sumari kwa kura 361, akifuatiwa na William Sarakikya aliyepata kura 259, Elishilia Kaaya (176), Elirehema Kaaya (205), Anthony Musari (22) na Moses Urio (11).
Ilidaiwa kwamba Sioi alizaliwa Kenya, hivyo kama akisimamishwa anaweza kukifanya chama kikawekewa pingamizi mbele ya safari.

"Kwa hiyo, hoja ni kwamba kama alizaliwa Kenya je, uraia wake ni wa kujiandikisha au kuzaliwa? Ndiyo maana, hata katika fomu ya uchaguzi ambayo ilikuwa na maswali mawili kama ni raia wa kuzaliwa au kujiandikisha, hakujaza hata moja," kilisema chanzo hicho.

Imedaiwa pia kwamba Sioi amekuwa mjanja kukataa kujaza vipengele hivyo viwili kwani labda kama kungekuwa na cha tatu ambacho ni uraia wa kurithi.

Kutokana na sababu hiyo na ile ya kutoungwa mkono na wagombea wenzake aliowabwaga, chanzo hicho kilisema Sekretarieti imempendekeza Sarakikya ambaye alikuwa mshindi wa pili apeperushe bendera ya chama katika uchaguzi huo kwani anaungwa mkono na wagombea wengine.
Imeelezwa kwamba Sioi ameitwa mbele ya CC leo ili kuwasilisha vielelezo vyake kuhusu uraia wake kabla ya kamati hiyo kufanya uamuzi.

Nape anena
Alipoulizwa juu ya taarifa hizo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema uamuzi wa mwisho kuhusu nani atagombea kwa tiketi ya chama hicho utatolewa leo na CC.
"Hata kama imetoa (Sekretarieti) mapendekezo kwa utendaji kazi wangu siwezi kulizungumzia. Kama nitazungumzia pendekezo maana yake nitakuwa nimezungumzia uamuzi. Mimi nazungumzia uamuzi wa chama ambao utatolewa na CC leo," alisema.

Alisema anajua kuwa wapo wanaoeneza taarifa hizo wakidhani kuwa wanaweza kukifanya chama kikaacha kufanya uamuzi wake.

"Kamati Kuu itakaa kesho (leo) hapa Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi, ndiyo itapitisha jina la mgombea wetu na kupanga mikakati mingine ya ushindi," alisema Nape.

Source:Gazeti la Mwananchi
 
Hata mimi nimeishtukia, hii ni habari njema kwani hivi ni vita vya panzi!. Kiukweli tukubali tukatae, angesimama Sioi, Chadema ingekuwa na kazi ya ziada!. Akipitishwa mwingine yoyote ni ushindi wa kiulani kama kumsukuma mlevi!.
Mkuu Pasco ni jana tu ulitudhihirishia kuwa Sioi atakuwa mgombea na atashinda inakuwaje tena, halafu ile plan A yetu ya washili itakuwaje au William naye ni mshili.

Nakukumbusha tu tamko la UVCCM-Arumeru kuwa kamati kuu isiporudisha jina la Sioi na wao watakuwa na mgombea wao.
 
Mkuu Pasco ni jana tu ulitudhihirishia kuwa Sioi atakuwa mgombea na atashinda inakuwaje tena, halafu ile plan A yetu ya washili itakuwaje au William naye ni mshili.

Nakukumbusha tu tamko la UVCCM-Arumeru kuwa kamati kuu isiporudisha jina la Sioi na wao watakuwa na mgombea wao.
Feedback, japo sina chama na Chadema naikubali sana tuu, ila kwenye uchaguzi wa Arumeru, nasimama na Sioi na machalii wote wa AR wako nyuma yake!. Asipopitishwa na CC leo, ile kambi yote ya Sioi, watashiriki kampeni za CCM, ila kura Chadema!. Kiuhakika bila Sioi, CCM itaangukia pua!.

Igunga RA ni muoga kama kunguru siku za mwisho alijitokeza kuokoa jahazi, Sioi asipopitishwa Mmeru No. 1 hatatia mguu Arumeru!, CCM ni kifo cha mende straight away!.
 
Inasemekana mchakato ni mkali ndani ya kikao kinachoendelea cha nec ya ccm na asilimia kubwa hawamtaki SIOI kwa kua ushindi wake wa uteuzi uligubikwa pia na rushwa,ngoja tuendelee kufatilia na yeyote atakaye pata taarifa aziweke hapa!!
 
Duh hii kali!!!!!!
Kwa hiyo wanajamvini mnamaanisha kua mtu ukitaka kujua kama wewe ni mtanzania halisi au lah....jaribu kuomba nafasi ya kuwania madaraka kupitia ccm???
Maana haya mambo ya fulani si raia au fulani ni mhamiaji yamekua yakijitokeza wakati wa chaguzi za ccm tu!!
 
Feedback, japo sina chama na Chadema naikubali sana tuu, ila kwenye uchaguzi wa Arumeru, nasimama na Sioi na machalii wote wa AR wako nyuma yake!. Asipopitishwa na CC leo, ile kambi yote ya Sioi, watashiriki kampeni za CCM, ila kura Chadema!. Kiuhakika bila Sioi, CCM itaangukia pua!.

Igunga RA ni muoga kama kunguru siku za mwisho alijitokeza kuokoa jahazi, Sioi asipopitishwa Mmeru No. 1 hatatia mguu Arumeru!, CCM ni kifo cha mende straight away!.
Sasa kama hatapitishwa kwa kigezo cha uraia watamwombaje raia wa kigeni (Kenya) awasaidie kampeni. Kuhusu ushindi wa Chadema hiyo haina mjadala nilishasema hata waunganishe majina Sioi na William waitwe Siwi CCM itashindwa tu, ngoja niseme msemo wa Nape kwa jimbo la Arumeru Mashariki CCM mnalo.
 
jamani mimi nimezaliwa namanga ni raia wa wapi? upande wa tanzania hakuna matibabu mazuri ikabidi mama yangu avuke aende upande wa kenya kwenye matibabu afadhali. sasa ninataka kugombea udiwani lakini sina uhakika na chama changu cha magugumaji wataniacha kweli?
 
Inasemekana mchakato ni mkali ndani ya kikao kinachoendelea cha nec ya ccm na asilimia kubwa hawamtaki SIOI kwa kua ushindi wake wa uteuzi uligubikwa pia na rushwa,ngoja tuendelee kufatilia na yeyote atakaye pata taarifa aziweke hapa!!
Kamati kuu ya CCM ndio inaitwa NEC!!?? na sio CC!!??
 
Back
Top Bottom