Uraia wa nchi mbili: Maendelo na Matokeo yake!

Uraia wa nchi mbili: Maendelo na Matokeo yake!

Mzee Mwanakijiji,msimuone nyerere kama ni mtu mwenye akili sana,kiasi kwamba mawazo yake yaendelee kuheshimiwa hata kama ni utmbo,........ mtibwa,lakini watu wa Moro hawauziwi sukari mpaka ije Dar,then ndio ipelekwe Moro.Kwa hiyo mawazo ya nyerere ama u-nyerererism umekwisha toka enzi ya uhai wake.Leo vyakula wananchi tunachagua madukani,mchele una unusa kama haunukii hununui.Mtoto unamtuma sukari,akija na sukari ya brown unamwambia rudisha nataka sukari nyeupe.

Marhabaa Mzee wa London,

Nimekuwa nasema kuwa JKN alikuwa kiongozi mzuri, ila hakuwa Mungu, ana mazuri na mabaya yake. Je leo tutupe televisheni zetu kisa ati mchonga aliziita anasa (ingawa yeye alikuwa nayo)?? Magari kwake yalikuwa anasa, Video player anasa, sjui hizi DVD au internet angeziitaje...(nadhani angeziita mashetani)
 
Mtukwao,

Kwenye uwekezaji, huwezi kujua mpaka uko involved kwenye hayo mambo.

Wewe unafikiri hao wageni hapo TZ kwanini wanang'ang'ania magamba ya TZ? Unafikiri wana mapenzi makubwa na Tanzania kuliko nchi wanazotoka? Hapana, jibu ni kwamba wanataka urahisi katika mambo wanayofanya. Ni rahisi kwa investor kufanya mambo yake mengi akiwa kama raia. Vibali mbalimbali hata bei zipo tofauti kati ya mgeni na mwenyeji. Mfano hiyo certificate ya TIC kupata kwa mwekezaji Mtanzania inatakiwa uwe na mradi wa dola laki moja wakati wageni ni dola laki mbili.

Kwa Watanzania wanaoishi nje, wakitaka kuja kuwekeza Tanzania kama wageni itakuwa ngumu sana kwa walio wengi, itatakiwa kushindana na hao wageni wenye mapesa, matokeo yake watashindwa na kuishia huko waliko miaka na miaka.

Soma mifano ya Ireland na hata Poland, jinsi raia wao waliokuwa USA walivyosaidi uchumi wa nchi hizo kwa kuanzisha biashara ndogo ndogo na pia baadhi ya watu kukubali kazi serikalini.
 
Jamani,
Ni kitu gani hadi leo hii kinafanya ni nchi chache tu dunuani hadi leo ndo zimekubali dualcitizenship? Maanake ingekuwa mali mbona kila nchi ingechangamkia mapema? Kwa nini hizi nchi zinasita? Lazima liko jambo? Siyo hivi2!
Haya mambo ya serikali to rush to do things 'kwa ajili ya presha' mimi naona sii sahihi! Kwa vile US na UK wamechangamkia nasi tuchangamkie?

Wazungu huwa hawachangamkii dili baya, ndo maana unaona nchi karibia zote zilizoendelea zinakubali, sisi akina yakhe tuna mnukuu JKN alivyosema miaka mia ngapi sijui iliyopita!

Binafsi nadhani watanzania tumeingizwa mjini na waTZ wenzetu ambao wala hawana uraia wa nchi mbili, ila tabia zao utadhani hawana utanzania kabisa. Viongozi wetu wanajifanya wanaipenda TZ hadi dili ya kuiibia TZ na waTZ wenzao ndio utajua wana utanzania kiasi gani.

Ninachosema ni kuwa uraia wa mtu si pasipoti ni matendo, na hilo tunatakiwa tulizingatie tunapojadili hili swala. Vigogo wetu hata macho hawapimiwi TZ wanaenda ulaya au india, je hawa ni waTZ wa kweli?, Tenda na dili nzuri za biashara wanawapa wakuja je uzalendo wao uko wapi?
 
Simu za mkononi?

Maana mwalimu alikuwa mgumu kinoma.Ni kweli amafanya kazi kubwa,kwa mafano ukabila alijitahidi sana tena sana.Mwalimu Rushwa alishindwa kupigana nayo,ndio maana alianzisha kikosi cha kuzuia rushwa 1973.Mwalimu ana mtani wake anaitwa "Sir" George Kahama,mpaka leo leo watu wanaamini kuwa kahama kweli ni Sir,lakini ukweli ni kuwa sio Sir,ila mwalimu alikuwa akimtania kahama kwa kumuita sir.Mwalimu aliwafukuza wahindi hapa,mwalimu akawapa wazawa nyumba za kisutu wazawa,mwalimu aliwapa madaraza marafiki zake amabo hawakusoma.

Nakumbuka Mzee Abeid Amani karume(former president of znz),alikuwa anapita mitaa amakuta rafiki yake anauza maziwa, akamchukua mpaka ikulu,akawambia kesho nenda kwa Goha ukashone suti tano kisha uje hapa, kesho alipofika akamwambia rafiki yangu nataka nikupe uwaziri unasemaje? Jamaa akasema sawa mzee, akampa uwaziri,akawa waziri anayeshughulikia kuweka hali za wananchi wote sawa, akaapishwa na kafanya hiyo kazi mpaka alipouawa karume, alikuwa ndio waziri wa kwanza wa wizara hiyi na mwisho, leo post hiyo ni department tu ktk wizara ya kazi znz.

Sasa leo hatuwezi kufanya mambo kama haya ya mzee Karume.
 
Ninachijua mimi,lengo la uraia wa nchi mbili,prioty itakuwa kwanza ni kwa watanzania ambao wanataka kunyakua uraia wa nchi nyingine,hao ndio watakao pewa kipaumbele,na sio raia wa nje wanaoutaka utanzania.Hivyo basi kama ni prioty itakuwa ni kwa watanzania kwanza basi hilo ni jambo zuri.
 
Marhabaa Mzee wa London,

Nimekuwa nasema kuwa JKN alikuwa kiongozi mzuri, ila hakuwa Mungu, ana mazuri na mabaya yake. Je leo tutupe televisheni zetu kisa ati mchonga aliziita anasa (ingawa yeye alikuwa nayo)?? Magari kwake yalikuwa anasa, Video player anasa, sjui hizi DVD au internet angeziitaje...(nadhani angeziita mashetani)

Sina la kusema na nimebaki kucheka tu....
 
Maana habari ni nzito,kiasi kwamba mwanangu Nyangi ngabu acheka.Lakini all in all hizo ndio khabari.
 
Tafadhali Shy unaweza kuiweka hii paper kwenye pdf,nataka kuipitia kwa umakini.Thanks in advance!!
 
Fears over dual citizenship no longer valid

2007-08-09 09:29:54
By Editor


The questions of dual citizenship in Tanzania has for the past fifteen years or so drawn up heated debates, some quite formal while still others have taken the grapevine course.

In the end of it all, two groups have emerged in the course of time, supporters and antagonists.

As we roll along, we have however discovered that time could be the best teacher. In the past, as we had strongly clinched on the socialist side of the Cold War, matters related to dual citizenship were seen as touching on sensitive national security issues.

Partly for similar reasons, a decision was taken to relocate the capital city from Dar es Salaam to Dodoma, lest sea-borne imperialistic stooges easily find some unknown field days and topple over the state.

Despite the billions spent to date to develop Dodoma as capital city, chances are still slim that it will ever become one. By good luck, the state is still safely seated in Dar es Salaam.

Of late however, an increasing number of countries are changing their citizenship laws from a single nationality stance to recognising dual citizenship.

The progress towards clinching dual citizenship has steadily been gaining thrust as nations become aware that their national security may not necessarily be jeopardised by mere application of dual citizenship under the present circumstances of intense globalisation and technological advancements which have melted territorial boundaries and surely merging the world into a global village.

The realities of the day forced the government to appoint a technical committee to seriously look into the possibility of introducing dual citizenship in Tanzania whose report is said to be ready and has been presented to the cabinet for scrutiny.

Insiders averred that Zanzibar, and by extension the Union factor, are holding back the fast-tracking of the issue to some final conclusions.
Members of Parliament have called for an immediate dual citizenship draft bill while the report is still under the cabinet`s microscope.

Indeed, lack of dual citizenship law in Tanzania can be shown to be an economic punishment of sorts. Groups of Tanzanians in Diaspora would very much wish to invest back home and boost the economy, certainly not as foreign investors but as nationals.

These groups, composed of Tanzanians who left the country in the early `70s and '80s are said to have amassed USD2.5 billion wealth and expertise and are ready to invest it at home, but the citizenship law is preventing that from happening.

While the citizenship law punishes the indigenous, the same is not for brethrens of Indian stock who enjoy trans-global lifestyle across two hemispheres, as they can conveniently claim dual lives in England, Canada, and the United States.

That would give them the leeway to run a mercantile store in Dar es Salaam with their nephews, and work to earn more money as labourers abroad while remitting back home more surpluses to recapitalize their businesses.

We should pick a leaf from India, a country that has developed a multi-billion dollar outsourcing industry partly because of the influence of dual citizenship.

Small businesses and entrepreneurs always benefit by outsourcing their services to professional service providers or freelancers as this saves them time and money.

The money saved due to outsourcing can be effectively and successfully utilized to focus more on strategic and core business functions.


SOURCE: Guardian
 
Mtukwao,

Kwenye uwekezaji, huwezi kujua mpaka uko involved kwenye hayo mambo.

Wewe unafikiri hao wageni hapo TZ kwanini wanang'ang'ania magamba ya TZ? Unafikiri wana mapenzi makubwa na Tanzania kuliko nchi wanazotoka? Hapana, jibu ni kwamba wanataka urahisi katika mambo wanayofanya. Ni rahisi kwa investor kufanya mambo yake mengi akiwa kama raia. Vibali mbalimbali hata bei zipo tofauti kati ya mgeni na mwenyeji. Mfano hiyo certificate ya TIC kupata kwa mwekezaji Mtanzania inatakiwa uwe na mradi wa dola laki moja wakati wageni ni dola laki mbili.

Kwa Watanzania wanaoishi nje, wakitaka kuja kuwekeza Tanzania kama wageni itakuwa ngumu sana kwa walio wengi, itatakiwa kushindana na hao wageni wenye mapesa, matokeo yake watashindwa na kuishia huko waliko miaka na miaka.

Soma mifano ya Ireland na hata Poland, jinsi raia wao waliokuwa USA walivyosaidi uchumi wa nchi hizo kwa kuanzisha biashara ndogo ndogo na pia baadhi ya watu kukubali kazi serikalini.

I contend .. "Dual Citizenship does not play any significant role in increased investments!"

Please prove me wrong!
 
Serikali yapania uraia wa nchi mbili

Na Mobhare Matinyi, New York

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, amesema serikali itahakikisha sheria ya uraia wa nchi mbili inapitishwa kwa manufaa ya Watanzania na taifa na si vinginevyo.

Akizungumza na baadhi ya Watanzania waliokutana naye mjini New York wiki iliyopita katika hoteli ya Grand Hyatt, Waziri Membe alisema lengo la serikali ni kuwasaidia Watanzania na si kugawa uraia wa Tanzania kwa wageni wenye uraia wa nchi zao.

Alisema haingii akilini ni kwa nini Mtanzania wa kuzaliwa anyang’anywe uraia wa Tanzania kwa kuwa amechukua uraia wa nchi nyingine kutafuta faida za kielimu, ajira au hata matibabu.

“Ni kwa nini tumuadhibu huyu Mtanzania wa kuzaliwa kwa kuwa tu amechukua uraia wa nchi nyingine ili apate elimu ama ajira na kusaidia ndugu zake waliobaki Tanzania?” alihoji Waziri Membe.

Waziri alisisitiza kuwa sheria hiyo itakapopitishwa haitatoa mwanya kwa kila mtu kuuvamia uraia wa Tanzania bali itawalinda Watanzania wanaotaka kuchukua uraia wa nchi za nje kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Akitoa mfano mmojawapo bila kutaja majina ya wahusika, Waziri Membe alisema anaifahamu familia moja ya Watanzania ambayo ililazimika kuchukua uraia wa Kanada kwa sababu za matibabu, na kwamba kuwanyang’anya uraia watu hawa ni kuwaadhibu bila kujali uhai wao.

Alieleza kuwa familia hiyo ina watoto wawili ambao matibabu yao hugharimu dola 2,000 kwa kila mmoja kwa mwezi, na kwamba kwa kuchukua uraia wa Kanada, matibabu hayo yanakuwa bure. Alihoji je, ni haki kuwanyang’anya uraia wao wa Tanzania?


Akitoa mfano wa manufaa yanayopatikana Ghana, Waziri Membe aliwaambia Watanzania hao kwamba ni muhimu kwa Tanzania kutumia raia wake walioko nje kwa manufaa ya taifa na siyo kuwabagua.

“Mwaka jana pekee wananchi wa Ghana walioko nje waliingiza dola bilioni 2.5 kwa njia mbalimbali halali,” na akaongeza: “Taifa dogo kama Komoro, mwaka jana lilipata dola milioni 89 kutoka kwa wananchi wake walioko Ufaransa pekee.

Akifafanua zaidi, Waziri Membe alisema wakati akiwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kipindi kisichofikia miaka miwili, Tanzania ilitoa uraia kwa wageni 101 na kushangaa ni kwa nini Watanzania wa kuzaliwa wapoteze uraia wao.

Waziri Membe aliwataka Watanzania kujenga umoja thabiti na kuwahakikishia kwamba serikali itakuwa pamoja nao ili kuleta maendeleo kwa taifa, na kwamba mawazo kuwa usalama wa taifa utakuwa hatarini si la jambo kuhofia iwapo sheria itatungwa vizuri.

Tanzania ina raia wake waliosambaa nchi mbalimbali duniani huku idadi kubwa ikiwa katika nchi za Kiarabu za Ghuba ambako wakati serikali ikiongeza ofisi moja ya Ubalozi nchini Oman miaka michache iliyopita ilikadiria kuwa kuna Watanzania laki tano.

Nchi nyingine ambazo Watanzania wanakadiriwa kuwa wengi ni za Marekani Kaskazini na Ulaya Magharibi ambako wako kwa maelfu, ambao wengi wao hukabiliwa pia na utata wa uraia wa watoto wao wanaozaliwa ugenini.

Mjadala wa suala la uraia wa nchi mbili umekuwa ukiendelea nchini katika siku za karibuni ambako kumeibuka kambi za wanaopinga kwa madai ya kulinda maslahi ya nchi na wanaounga mkono kwa madai hayo hayo ya kulinda maslahi ya nchi.
 
Katika Dunia hii Ya utandawazi tuwe makini...wakati afrika Bado Ina chechemea Mi nina fikiri Tanzania Iruhusu Uaraia wa nchi Mbili lakini iwe Ndani ya Africa..Kwanza..Unaweza ukawa Mtanzania laikini ukawa Raia wa Nchi nyingine Ya Africa!!...

Kama una akili Timamu utanielewa!! Kama Fala Itakuchukua muda sana...
 
Mheshimiwa Membe,

Naona argument yako ina nguvu mno. Tuelezeni lini hiyo sheria itapelekwa bungeni maana kila siku tunaambiwa itapelekwa lakini
hakuna ambaye anasema lini.
 
Haya Endelea Na Ufala wako!!...Mi naona Kama kichekesho!!Africa hata Vitabulisho vya Uraia Bado Havija Tangenezwa...Mimi Natumia cha kupigia Kura!!...aaah! nyie endeleeni na ubishi wenu...Kisa mawaziri wanataka Kua Wamarekani-wachina...We fikiria!!

Tamaa...Fala ni fala tu...
 
Kwa hiyo sheria hiyo ina faida kwa watu wa matawi ya juu pekee?
 
haya sisi tujivute tuu. wenzetu waganda wanaruhusu uraia wa nchi mbili hivyo mganda anaweza kuwa mganda na mtanzania. ndio maana m7 anataka uganda na kenya ziendelee na kuunda jumuia kwani tayari wananchi wake wanuwezo wa kuukwaa utz.

nadhani muda wa maneno umepita sana ni vyema serikali ikaanza hizo taratibu za kuruhusu uraia wa nchi mbili mapema kuliko juzi.

kwi, kwi, kwi, naona nami ni mmoja wa mafala nisiomwelewa mkuu hapo juu, kwi, kwi, kwi🙂
 
Naendelea sasa na nitaendelea tena kesho kuupinga Uraia wa Nchi mbili . Wazungu ndiyo model yetu ya maendeleo nadhani kila mara we must site them as an example hadi kufika hapo hawakuhitaji uraia wa Nchi 2. Wamefika hapo kwa kuuthamini uraia wao na kuachana na mawazo ya kifisadi na matendo ya kifisadi. Unaweza kupeleka pesa Tanzania hata sasa na watu wamekuwa wakipeleka pesa TZ kabla ya hata wazo la uraia wa Nchi 2.

Hapa Membe anaongeza speed mtaona sasa watakavyo kuja watoto wao kuchukua madaraka na kueneleza utawala waoa kwa manufaa yao . Uraia wa Nchi 2 hivi itakuwaje kwa ajira za polisi, usalama wa Taifa , jeshini nk ?Mnaongelea Waghana kupeleka pesa hizo kwao wakati hata sisi watanzania tunapeleka na baadaye wazungu wanapeleka mabilioni lakini bado tuko hata kadi za kupiga kura ughaibuni wala access ya kuchagua ukiwa ughaibuni haipo . We are not serious na dual is never an answer.
 
Haya Endelea Na Ufala wako!!...Mi naona Kama kichekesho!!Africa hata Vitabulisho vya Uraia Bado Havija Tangenezwa...Mimi Natumia cha kupigia Kura!!...aaah! nyie endeleeni na ubishi wenu...Kisa mawaziri wanataka Kua Wamarekani-wachina...We fikiria!!

Tamaa...Fala ni fala tu...

Gigo,

Kwa taarifa yako anayetaka kuwa waziri hawezi kutaka kuwa na magamba mawili. Kila mtu anajua yaliyompata Salim japo yeye ana gamba moja tu.

Kwa uzoefu wangu wa kukaa huku majuu, uraia wa nchi mbili unasaidia zaidi walalahoi kuliko wenye nafasi za juu.

Nimekutana na Watanzania ambao walikuwa wanasema hata iweje hawawezi kuchukua gamba lingine lakini through mihangaiko ya maisha na kunyanyaswa kwenye embassies mbalimbali wakaishia kugeuka na kuchukua.

Mtu mwenye kazi ya maana au pesa nzuri wala hahitaji hiyo dualcitizenship ili kuweza kunyosha maisha yake akiwa nje ya nchi. Kazi na pesa ni security tosha ya mambo yake kwenda sawa na kuweza kwenda popote bila matatizo.

Binafsi nilishasema sihitaji gamba la pili hata serikali ikiruhusu ila tu naelewa matatizo wanayopta baadhi ya Watanzania wenzangu huku nje na naamini kuruhusu uraia wa nchi mbili utawasaidia watu wengi hasa wale walalahoi kama mimi.

Ni rahisi sana kwa mtu aliyeko Tanzania kuona watu walioko nje wanaotaka gamba la pili ni watoto wa wakubwa. Hata mimi wakati nakuja Ulaya enzi hizo (miaka ya 90) nilikuwa najua Wakenya wanaokuja nje ni watoto wa vigogo. Nikaja kuta kuna watoto wa wakulima, waendesha matatu nk. Watanzania na sisi kwasasa tumefikia hapo, huku kuna kila aina ya watu, kwahiyo hili suala sio kwa faida ya wakubwa na badala yake watu wengi wakiwemo walalahoi wenzetu.
 
Back
Top Bottom