Upungufu wa Wahadhiri Vyuo vya Elimu ya Juu

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Taarifa kwamba taasisi za kitaaluma za elimu ya juu zinakabiliwa na upungufu wa Wahadhiri inastua sana na kuhitaji ufumbuzi kwa kasi ya mwendo wa mwanga. Binafsi nafikiri tatizo hili limesababishwa na uamuzi wa serikali ya awamu ya tano kutumia rasilimaliwatu hawa kwa kuwaondoa vyuoni na kuwaleta serikalini kwa idadi kubwa iliyovunja rekodi ya dunia bila kujuwa nafasi zao kule vyuoni zitajazwaje? Lini? Kwa utaratibu upi? Hii inaweza kufanya vyuo vyetu kushuka hadhi kimataifa na kukosa wanafunzi toka nje ya mipaka kwa vigezo hivyo kikiwemo kile cha kwamba vyuo vyetu vinahudumiwa na wahadhiri wapya wachache (waliohitimu karibuni) ambao kimsingi hawana uzoefu kama wa wale watangulizi wao waliohamishiwa serikalini kwa mtindo ninaoweza kuufananisha na Great Trek.

Nini kifanyike?
Mhe. Rais SSH afanye uamuzi mgumu (kama ulivyofanywa wa kuwaondoa vyuoni) wa kuwarejesha vyuoni ili nafasi zao wanazoacha serikalini zijazwe na watumishi wa kaliba nyingine kama ilivyokuwa desturi tangu uhuru. Aidha, kufanyike maboresho ya vikokotoo vya pensheni na mafao yao ili wavutiwe kuendelea kubaki huko vyuoni badala ya kukimbilia nafasi za siasa ambazo kunadhaniwa kuna mafao na pensheni nono zaidi. Aidha, serikali iongeze umri wao wa kustaafu hadi miaka 70 lkn kwa yule tu ambaye amekubali kubaki kwenye ajira ya chuo, nje ya ajira ya chuo umri huo upunguzwe.

Chanzo:
Gazeti la Mwananchi 21/10/2021.

By Jacob Mosenda

Dar es Salaam. Vyuo vikuu vya ndani vinakabiliwa na upungufu wa wahadhiri wenye sifa, kwa mujibu wa wakuu wa vyuo.

Siri hiyo imefichuliwa wakati wadau wa elimu wakieleza wasiwasi kuhusu ubora wa wahitimu hapa nchini.

Akizungumza katika mkutano ulioikutanisha Serikali, makamu wakuu wa vyuo na wadau muhimu wa elimu Dar es Salaam hivi karibuni, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka alisema shida hiyo bado haijashughulikiwa.

“Tumeshuhudia katika maeneo mengine wafanyakazi wakiajiriwa mara kwa mara, lakini inaonekana vyuo vikuu vimesahaulika kidogo. Tunaomba eneo hili pia likumbukwe,” alisema Profesa Kusiluka.

Akijibu ombi hilo, Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako aliiambia Mwananchi kuwa, changamoto hiyo inajulikana na kuna mfuko utakaotoa ufadhili wa masomo kwa wahadhiri 1,000 ili kuwawezesha kupata sifa za kufundisha vyuo kikuu.

“Hii ni moja ya hatua tunazochukua kuhakikisha elimu inayotolewa na vyuo vyetu ni bora, hivyo lazima tupate suluhisho kwa changamoto hizi,” alisema Profesa Ndalichako.

Katika miaka miwili iliyopita, takwimu za Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) zinaonyesha kuwa wafanyakazi wa vyuo vikuu wameongezeka kutoka 6,238 mwaka 2019 hadi 7,187 mwaka 2020.

Wakati huohuo, uandikishaji wa wanafunzi umekuwa ukiongezeka kwa wastani wa asilimia 4.7 kwa mwaka kutoka wanafunzi 177,963 katika mwaka wa masomo 2017/18 hadi wanafunzi 206,305 mwaka 2020/21.

Hali ya sasa kwa mujibu wa takwimu za TCU, katika programu nne za Elimu, Sheria, Sayansi ya Tiba na Afya, Sanaa pamoja na Biashara, kumekuwa na tofauti ya idadi ya wanafunzi na wahadhiri inayoelezea upungufu uliobainishwa.

Mwaka 2019, Programu ya Elimu iliandikisha wanafunzi 54,156 (wahadhiri 524), Sayansi ya Tiba na Afya ilikuwa na wanafunzi 23,374 (wahadhiri 802). Programu za Sanaa zilikuwa na wanafunzi 6,345 (wahadhiri 616), Sheria wanafunzi 12, 424 (wahadhiri 205) na Biashara ikiandikisha wanafunzi 28,300 kwa wahadhiri 466.

Kufikia mwaka 2020 Programu ya Elimu ilikuwa na wanafunzi 51,489 na wahadhiri 708, wakati Sayansi ya Tiba na Afya ilikuwa na wanafunzi 24, 642 na wahadhiri 1,134. Programu ya Biashara ilikuwa na wanafunzi 107,913 kwa wahadhiri 729.

Kwa mujibu wa TCU, hadi kufikia 2020 kulikuwa na jumla ya wahadhiri 7,187 katika taasisi za vyuo vikuu.

Kati yao 4,863 walikuwa katika vyuo vikuu vya umma na 2,324 katika vyuo vikuu binafsi. Miongoni mwao, 5,088 ni wahadhiri wa kiume na 2,099 wanawake.

Wadau wa elimu walisema kama mambo hayo hayataangaliwa na kushughulikiwa ipasavyo, ubora wa elimu nchini utaporomoka kwa kasi.

Dk Thomas Jabir ambaye ni mshauri wa masuala ya elimu, alisema kumekuwa na ongezeko la vyuo vikuu lakini ongezeko hilo halilingani na ongezeko la rasilimali watu.

Kwa mujibu wa TCU, hadi Februari 2016, Tanzania ilikuwa na jumla ya vyuo vikuu 33 vya umma na vya binafsi, idadi ambayo imeongezeka hadi kufikia vyuo vikuu 47, vya umma 19 na 28 vya binafsi.

“Kuzalisha mwenye PhD huchukua muda mrefu na ni ghali pia. Inaweza kuchukua hadi miaka 10 au 12 kupata moja,” alisema Dk Jabir.

Ripoti ya 2017 ya Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) ilikuwa imebainisha uhaba wa wafanyakazi wa masomo katika taasisi za elimu ya juu nchini kuwa asilimia 44.

Ripoti hiyo, ilibainisha kuwa, asilimia 53 ya wafanyakazi wa ngazi za juu waliokuwa wakifundisha katika vyuo vikuu walikuwa wamestaafu na walikuwa wakifanya kazi kama wafanyakazi waliopewa mikataba.
 
walete wakenya
Mkuu,
Kwani tumeishafikia awamu ya itifaki ya kazi (Labour Protocol Phase) ya EAC kwamba nchi wanachama sasa wanaweza kufungulia mipaka yao kwa raia wao kutafuta kazi nchi nyingine mwanachama?

Lakini nina wasiwasi kwamba vyuo vyetu miaka michache ijayo huenda vitaporomoka kwenye world universities ranking.
 
Yaani vyuo vikuu venye wasomi wa PhD na Prof kama wote, budget kutoka serikali kuu na mapato kutoka kwa wanafunzi na bado wana access ya kupata funds kutoka nje maana kwao ni rahisi maana ndio waandikaji wa projects mbalimbali.. wanashindwa kujitatulia tatizo la ukosefu wa wahadhiri..wanategemea wanasiasa waje wawatatulie..

Halafu kwenye majukwaa huko wanawananga vijana wajitatulie matatizo ya ajira wenyewe...

Africa bhana...tutasubili sana
 
Yaani vyuo vikuu venye wasomi wa PhD na Prof kama wote, budget kutoka serikali kuu na mapato kutoka kwa wanafunzi na bado wana access ya kupata funds kutoka nje...
Eti kweli! hili nalo neno la kutufikirisha ili tufanye kitu. Mataifa tajiri taasisi kama hizi zikiwemo majeshi zinaingiza maduhuli ya kutosha kuziendesha bila bajeti za serikali. Ndiyo maana JPM hakuona sababu ya Magereza kuomba chakula serikalini.
 
Tatizo ni hao maprofessa waliokuwepo kujifanya miungu watu na ujuaji mwingi, hawakutaka ku-recruit vijana waingie kama tutorial assistants kwa kukandamiza ufaulu ili waonekane hakuna wenye akili kama wao, saa hizi wamezeeka hawana namna vinginevyo watafia madarasani.

Cha kufanya wasomi wa kiwango cha Masters na PhD kutoka taasisi nyingine za umma na binafsi wahamie kufundisha vyuo vikuu..
 
Tatizo ni hao maprofessa waliokuwepo kujifanya miungu watu na ujuaji mwingi, hawakutaka ku-recruit vijana waingie kama tutorial assistants kwa kukandamiza ufaulu ili waonekane hakuna wenye akili kama wao, saa hizi wamezeeka hawana namna vinginevyo watafia madarasani. Cha kufanya wasomi wa kiwango cha Masters na PhD kutoka taasisi nyingine za umma na binafsi wahamie kufundisha vyuo vikuu.........
Great! ndiyo maana nimesema Rais afanye maamuzi magumu tu. Pia hoja yako hiyo inawezakuwa na mashiko kwamba kama ufaulu uliminywa ili wengi wasisome wakawa wahadhiri sasa tujiandae kwa Mabeberu kutuletea misaada ya wahadhiri weupe, tunarudi kuleeee kwenye enzi ya ukoloni ambapo jeshini maaskari weusi hawakustahili vyeo hadi pale baada ya uhuru jeshi letu likafanya uasi uliozimwa ambapo walikuwa wakidai vyeo na maslahi bora. Baghosha!
 
Back
Top Bottom