ASHA NGEDELE
JF-Expert Member
- Jul 5, 2011
- 784
- 326
Habari wakulima wenzangu,
Nimelima tikiti ekari mbili na linaendelea vizuri kwani halina ugonjwa wowote mpaka leo siku ya 34 tokea mbegu kupasuka.
Changomoto nayoipata kwa sasa ni mmea kuzalisha maua mengi sana lakini maua dume kwahio mpaka sasa matunda yalozalishwa ni machache sana. Hali ikiendelea namna hii naona hasara kubwa sana huko mbeleni. Wiki mbili zilizopita nlitumia mbolea ya Yara Nitrabor na kesho natarajia kutumia tena mbolea hio hio 10gm kila mche. Mbolea ya majani natumia Di-Grow pekee. Maji huwa naruka siku moja lakin nimeshauliwa nipige kila siku sababu kwa sasa jua ni kali sana na nalimia eneo la Kichanga sana.
Je,
1. Nifanye nini cha ziada ili nipate maua jike mengi ili matunda yazalishwe kwa wingi?
2. Matunda yakianza kutoka kwa wingi mfano siku ya 40, na kwa kawaida mbegu nayotumia matunda huwa yanakomaa kuanzia siku ya 60, hizi siku 20 zitatosha kweli matunda kunenepa na kuwa makubwa ambayo yatanipatia faida Sokoni? Au yatakomaa yakiwa na umbo dogo?
Asante