Kwanza ujue wazi kuwa taifa teule haina maana wao hawakosei au hawana mapungufu, nao ni wanadamu kama sisi tu. Pia kuna sehemu inasema wazi kwamba Israel si kwamba yeye ni mwema sana au anahaki sana ila Mungu amempenda na kumchagua, na zaidi sana imeandikwa kuwa hawa jamaa wana shingo ngumu!
Halafu pamoja na wao kuwa taifa teule, dini ya kiKristo kwao ipo kwa uchache sana ukilinganisha na huku kwetu au kwenye mataifa mengine. Wao dini ya kiyahudi ina wafuasi wengi zaidi na kwa sehemu kubwa wanaongozwa sana kwa sheria na wanafuata sana Agano la kale.
Wewe jitahidi tu kusimamia unachokijua na kukielewa, kila mtu na kiasi chake, usipate taabu na mtu mwingine sababu na yeye anayo mapungufu mengi tu. Wala usitishwe na majina ya mlokole, nabii, wa upako nk, kipimo cha mtu anaye kijua ni Mungu Mwenyewe
Sent from my SM-J110F using
JamiiForums mobile app
Hapana mkuu ukisema nisipate taabu na mtu mwingine si ndio uchoyo wa maarifa huo, mi naona ni vema kila mmoja anapochangia anachokijua kisha kufikia muafaka kwa kushauriana ama kurekebishana.
Mfano:
1. kwanini nilisema wa Africa tusiwe na dini zetu? ni kwasababu nikiangalia u Kristo hasa katika haya mataría yalioendelea na ambako ni chimbuko la u Kristo, sijaona wakiwa na IMANI kama nchi za Ki Africa zinavyo amini katika Kristo.
Nilipokuwa mgeni moja ya Nchi hizo ninamo ishi kwa keli nilijitahidi sana kuhudhuria misa mbalimbali za makanisa mbalimbali. Lengo la kwanza ni upweke siku za weekend pili nikaanza kunogewa na kujifunza kuhusu IMANI yao katika Mungu.
Mavazi-Nilienda kanisa moja la kiroho, mavazi waliovalia hadi wahubiri ni very casual wake kwa waume, pensi fupifupi maana ilikuwa msimu wa joto kali sana.Lakini pia mahuburi yalikuwa hayana vitisho vya kwenda motoni au jehanam, mahubiri mengi yalikuwa ni upendo, upendo na upendo. Ndipo nikawaza ingekuwa nyumbani Tanzania hawa waumiini hata wasingeingia hapa kanisani. Shemasi angewarudisha wakavae nguo za kumtukuza Mungu.
Nilienda kanisa la Wasabato, huku nilikuta kanisa kubwa sana, zuri mno, kuingia ndani kuna waumini wachache mno kulingana na ukubwa wa kanisa lenyewe na idadi ya watu. Nikahesabu watu pale kanisani faster faster, kulikuwa na kama watu 40, kati yao wazungu walikuwa 9, wengine wanaobakia ni mataifa ya ki Afrika....yani kanisani hakunogiiiii
Mavazi yao kama ya kanisa la mwanzo tu, nguo fupi, hereni, cheni, na mambo mengine ambayo wa Sabato wa nyumbani TZ hawafanyi. nikazidi kujiuliza sasa haya makanisa ya nyumbani mbona yana mashariti mengi sana, shida ni nini? wanapata wapi hizo sheria.
Roman, rafiki yangu nafanya nae kazi yeye ni m Roma pure, siku moja tupo kazini akaingia mama mmoja kazini, huyu rafiki yangu akanambia mwangalie yule mama ni hawala wa mume wangu. Nikashangaa kuwa kumbe hata wazungu wanakuwa na mahawala, ndipo akaniambia yeye na mumewe walishatengana kitambo, sasa wapo kwenye process za talaka! nikashangaa talaka we si m Roma akasema ndio, na talaka akipata anaruhusiwa kuolewa tena kanisani.
Badae nikajifunza mambo mengi tu, kuwa kuna hawa ma sister wa Roman, badhi yao ni wanawake ambao waliwahi kuolewa na kuzaa, badae anaona ah wacha nikamtumikie Mungu. Ibada inajaza sana watu siku za msiba au harusi ndipo watu wengi huenda kanisani. Ni mengi sana ila nifanye kufupisha ili nisitoke sana kwenye uzi wa Mshana jr