Upungufu wa kinga za kiroho

Upungufu wa kinga za kiroho

hizi kwa mara ya kwanza nimeandika kitu cha maana.... Nimeshakutana nazo sana kwenye mada zangu... Asante
Sikuumbiwa kinyongo Kwahiyo hata pale mnapojenga chuki dhidi ya post zangu najua sio nyie bali ni yule Lucifer anayewaendesha kufanya hivyo... Thanks all the way kiroho safi kabisa
Kimsingi umeelezea kitu ambacho nimekuwa nikihisi kila siku katika Imani yangu.
Kuwa mtu akujishirikisha katika masuala ya kishirikina, sana sana anakaribisha maovu mengi kumfuata na kumuangamiza kiroho na kimwili.
Mimi natoka ukoo wa kichifu, nimeona ndugu zangu wakiangamia na nisiwe na jinsi ya kuwasaidia.
Mmi Imani yangu katika Kristo imenisadia sana, ingawaje sijiiti mlokole wala mtakatifu.
 
hizi kwa mara ya kwanza nimeandika kitu cha maana.... Nimeshakutana nazo sana kwenye mada zangu... Asante
Sikuumbiwa kinyongo Kwahiyo hata pale mnapojenga chuki dhidi ya post zangu najua sio nyie bali ni yule Lucifer anayewaendesha kufanya hivyo... Thanks all the way kiroho safi kabisa
Lucifer akiwa mbinguni... Alipotupwa duniani akaitwa shetani
 
Wengi tunapoongelea neno KINGA tunapeleka mawazo yetu moja kwa moja kwenye mipira ya kufanyia ngono yaani kondomu.. Lakini wengine watadhani ni kinga dhidi ya maradhi ama kinga dhidi ya ajali barabarani na wezi majumbani huku wachache wakiwaza kinga dhidi ya watoto nknk... Akitokea mmoja akazungumzia kinga ya kiroho huyo itabidi umwangalie mara mbili kwakuwa si kawaida na si mazoea
Tumekuzwa kwenye kuulinda mwili, kulinda vile vinavyoonekana, tunauhudumia mwili wa nyama uwe na siha njema, sura ivutie, nywele zivutie, nguo zikubali, tunaunywesha na kuulisha mwili wa nyama uharibikao na kusahau kabisa msingi wa kinachoufanya huo mwili uhudumiao uuhudumie
Mwili dhaifu usio na kinga imara ni rahisi sana kushambuliwa na magonjwa mbalimbali, kuna watu haipiti mwezi kaugua hiki ama kile... Hawa automatically miili yao haina kinga thabiti... Ni watu wa spana mkononi kama gari bovu trip moja kazini, trip moja kwa fundi
Sasa mwili huohuo unaoweza kuwa na afya na siha njema usioshambuliwa na magonjwa ya mara kwa mara unaweza kuwa na upungufu mkubwa wa kinga za kiroho.... Pigo lolote likirushwa humpata yeye kama sio jini makhaba, basi ni zongo, kama sio zongo basi ni mapepo, kama sio mapepo basi ni chochote kibaya cha roho chafu kitampata
Mti mwenye upungufu wa kinga za kiroho mambo yake hayaendi kwenye stark, hayanyooki, hayasimami sawasawa, kama ni ajira inakuwa ngumu kupata, na akiipata hachelewi kuacha kuharibu ama kufukuzwa.. Kama ni biashara nuksi tupu, kama ni mahusiano balaa tupu, hakuna atakaloshika likakaa sawa...

Kuna vitu husababisha upungufu wa kinga za kiroho... Mungu (kwa wale waamini na waaminio) huleta duniani kiumbe kamili chenye kinga zote(usichanganye na wale watoto wa kichawi na majini) Lakini katikati ya harakati za maisha watu hupoteza ama kupunguza kinga zao kwa kwenda kwa waganga wa kienyeji, kuhangaika bila kuwa na msimamo wa kiimani, kufanyiwa mambo mabaya ma jirani ndugu ama rafiki
Habari za kusafishwa nyota ama kupewa Pete za bahati ni vitu vibaya kabisa kiroho..
Habari za kuhangaika kwa waganga wa kienyeji ni kuzidi kujichafua kiroho na kujiharibia kabisa.. Yani mwili wako unakuwa kama punching bag, kila mtu anajaribu hapo
Kutangatanga kiimani, mara huku mara kule unahangaisha bure roho yako na kuichosha sana mwisho inakuwa dhaifu kabisa
Jijengee msingi imara wa kinga ya kiroho kwa kubaki na imani moja bila kujali unaamini katika nini....
Pambana na hali yako kwa njia chanya... Kila mmoja wetu ana changamoto nyingi sana za maisha... Epuka nguvu hasi yoyote kwa manufaa binafsi. Unajiharibia...
Epuka epuka epuka kujihusisha na mambo ya giza huko huendi kutengeneza bali kujimaliza.... Unafuu wake ni wa muda mfupi sana.....
Wengi wanaohagaika leo wenye upungufu wa kinga za kiroho angalia historia zao wengi wamepitia hayo hapo juu...... Simama na Mungu wako ujenge kinga imara ya kiroho....

Mkuu huu uzi sikubahatika kuuona! Kuna mambo ya msingi humo umeyaekeza vizuri sana na Kifalsafa. Hongera sana!
 
@kassimneema
a7ea92da75779104a3489e6da239c5de.jpg
 
Kiukweli Mshana jr mi sikuelewagi....Wewe ni mtu wa aina gani? mganga,au muumini tu wa kawaida?...Je kanisani unaenda? au msikitin.??
 
Kiukweli Mshana jr mi sikuelewagi....Wewe ni mtu wa aina gani? mganga,au muumini tu wa kawaida?...Je kanisani unaenda? au msikitin.??
Mimi sio mganga na sijawahi kujifanya mganga nafanya kazi halali kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.. Mimi ni mkristo Mlutheri mwongofu ninayempenda Kristo Yesu... Naenda Kanisani na nisipoenda huwa sijisikiii vizuri... Asante
 
HESABU 23:23

"Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!"
 
Mimi sio mganga na sijawahi kufanya mganga nafanya kazi halali kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.. Mimi ni mkristo Mlutheri mwongofu ninayempenda Kristo Yesu... Naenda Kanisani na nisipoenda huwa sijisikiii vizuri... Asante
Safi....Mi ni miongoni mwa wasomaji wa makala zako,ni nzuri.Na leo kuna kitu umeniongezea,na kimenifaa.Mwanzo nilijua wewe na mzizimkavu ni ndugu.Unamfahamu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom