Upotoshaji : "Serikali ya Magufuli" badala ya "Serikali ya JMT"

Hakuna hatari iliyonipa kufikiria upya maana ya maisha na kuitwa binadamu zaidi ya niliposikia

".....watajidai kukimbilia mahakamani. Wanasahau kwamba Mahakama zote ni za serikali, na serikali ni ya Magufuli..".
​
Na bado watu na akili zao tena wanawatoto wakaendelea kupiga makofi na kushangilia. Ukwlei siku hiyo nilikaa peke yangu kwenye kichuguu kwa muda nikitafakari dunia hii ni kitu gani kwa binadamu na binadamu ni nini.

Wewe hukusikia? Siku njema.
mkuu,hatuna la kufanya kwa sasa,shida zitawanyoosha watu hao wanao shangilia,na iwapo hisia zitaendelea kutawala badala ya akili,mkuu,beware!sitashangaa mtu akiniambia ya kibwetere!now i can see and touch it!mkuu,wakianza kuwaambia washangiliaji kuwa sababu ya ukosefu wa mahitaji muhimu ni kwa sababu watz tuko wengi kulilo mahitaji hayo,na suluhu yake ni watu kujitosa kwenye maji ili mahitaji hayo yawe even na watu...wewe na mimi na wengineo,tukimbie!
 
Hata Uganda kwenye vielement vya udikteta huwezi kumsikia waziri anasema " Serikali ya Yoweri Museveni inaagiza hili na lile" sasa haya ya hapa yametokea wapi? Na mbona yanashika kasi na kuwa desturi? Jee ndio sababu inayochangia viongozi kuwa na tabia za kinafiki kumridhisha mtu mwenye "serikali yake?"

Mtangulizi wake aliwahi tueleza kuwa nakariri"Serikali yangu haina ubia"hapo unasemaje?
 
Aliomba kura kwa sentensi ya kauli hiyo tena kwa kusema serikari yangu itafanya hivi, itafanya vile......
Na watanzania wakampa kupitia hiyo hiyo kauli. Umechelewa mleta maada hii mbinu ingetumika kumwangusha wakati wa uchaguzi

Ikumbukwe kua ni kama raisi anapiga kampeni vile.. Hivyo watu baadp akili zetu haziamini kama ndicho anachokifanya kwani tumezoea nyimbo majukwaani uchaguzi ukiisha baasi
Sasa hivi imekua kinyume, kwa watu wabaya hawaamini
Kwa wakati kama huu ilikua ni muda
 
Labda kama hujui maana ya serikali!

Senekar this latin,

Mkuu sidhan ikiwa wewe pia unaangukia kwenye mtego wa mleta mada.

This is Magufuli adimn...
 
Sasa hivi viongozi wa serikali kuanzia mawaziri kuja chini wamejenga tabia ya kutoa maagizo huku wakitumia kauli kuwa serikali ya Magufuli inaagiza hili au lile na haitaki hili au lile.

Huu ni upotoshaji, hakuna serikali ya Magufuli popote hapa duniani zaidi ya nyumbani kwake, iliyopo ni ya Wananchi wa JMT inayoongozwa na Magufuli kama Rais aliyepewa ajira hiyo na masharti ya jinsi ya kufanya kazi na hao wananchi.

Huu mtindo wa kazi na maamuzi ya kidola haiwezekani kubinafsisha kwa mtu hali ambayo inamfanya hata akili yake ijijenge kuwa serikali hii ni mali "yangu".

Waziri akisimama kuzungumzia umeme anasema serikali ya Magufuli imeamua hivi, wakati huo ni mpango wa kitaifa. Na mikoani RC akishughulikia kisina atasema hivyohivyo wakati visima hivyovya serikali hata Magufuli havijui.

Hatari ya tabia hii itafikia hata Polisi wakizuia maandamano au fujo kujikuta wakitoa amri "Serikali ya Magufuli inatoa watu wote watawanyike mara moja kwa amani la sivyo ...."

Viongozi warudi kwenye matari, tunayo SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA pekee.
Ni sawa kabisa. Amerika nao wanapenda kuiita Obamas administration wakati waingereza wanapendelea kuita eg labours govt au conservative. Isikupe shida hiyo. Jali zaidi malengo, nia na Mafanikio ya serekali ya Magufuli.
 
You miss the point. Unaelewa hawa mawaziri, wakuu wa mikoa, wa mashirika nk nk wanaposema "serikali ya Magufuli" inataka hivi na vile wanamaanisha nini? Wao wana base katika kauli zake tuu na sio sheria na kanuni zilizowekwa na serikali ya JMT. Hata kama alichosema Rais kiko kinyume wao hawatahoji bali kusema mwenye serikali kaagiza hivyo.
Hiyo ndio hatari ya dhana ya "Serikali ya Magufuli" badala ya Serikali ya JMT iliyoko kisheria.
 
Serikali ya Magufuli maana yake ni serikali inayoongozwa na Rais Magufuli. Labda kama unataka tuingize siasa.
 
Huyo aliishia siku hiyo hiyo hakurudia tena, nafikri baada ya kuonywa!! Sasa huyu imekuwa kero, ma-VEO, WEOs, DCs, RCs and the like kila siku "Serikali ya Magufuli" waache hizo sisi tuna serikali ya JMT!
 
Serikali ya Magufuli maana yake ni serikali inayoongozwa na Rais Magufuli. Labda kama unataka tuingize siasa.

Hapo ndio pazuri kama hatuingizi siasa. Jee kisheria serikali ya Magufuli imesajiliwa kwa sheria ipi? Na kama ni serikali ya Magufuli nini kinamzuia akiota ndoto usiku na akili ikimtuma asubuhi asitangaze hayo maamuzi ya "serikali yake" kama ndoto zinavyo mtuma?
Hivi serikali yako treborx kuna mtu anahaki ya kuingilia maamuzi yako?
 
Mkuu, ni lazima tukubaliane tu. Marais wetu ni very powerful, na kaztiba zetu zimewapa nguvu hizo. Wanaposema "Serikali ya Magufuli" ni kweli kwa asilimia 100.
 
mkuu,hatuna la kufanya kwa sasa,shida zitawanyoosha watu hao wanao shangilia,na iwapo hisia zitaendelea kutawala badala ya akili,mkuu,beware!sitashangaa mtu akiniambia ya kibwetere!now i can see and touch it!mkuu,wakianza kuwaambia washangiliaji kuwa sababu ya ukosefu wa mahitaji muhimu ni kwa sababu watz tuko wengi kulilo mahitaji hayo,na suluhu yake ni watu kujitosa kwenye maji ili mahitaji hayo yawe even na watu...wewe na mimi na wengineo,tukimbie!

Ni kweli mkuu. Ni vizuri wawaambie mapema kwamba tunashida kwa sabbu tuko wengi na hivyo ili kuipa uwezo serikali kuhudumia wananchi lazima watz wapungue kwa namna namna yoyote ile. Ninajua hawa wapiga makofi wtakuwa wa kwanza kujitosa baharini. Hadi number inawiana, watakuwa wamejiondoa na hatutakuwa na sababu ya kukimbia kwa sababu watii wataenda kwa hiyari. Labda agizo liwe waanze kutukamata... hapo lazima tukimbie. Ninahakika watatii bila ktumia akili na hiyo siku si ajabu haiko mbali.

Mchana mwema kiongozi.
 
Sasa hivi viongozi wa serikali kuanzia mawaziri kuja chini wamejenga tabia ya kutoa maagizo huku wakitumia kauli kuwa serikali ya Magufuli inaagiza hili au lile na haitaki hili au lile.

Huu ni upotoshaji, hakuna serikali ya Magufuli popote hapa duniani zaidi ya nyumbani kwake, iliyopo ni ya Wananchi wa JMT inayoongozwa na Magufuli kama Rais aliyepewa ajira hiyo na masharti ya jinsi ya kufanya kazi na hao wananchi.

Huu mtindo wa kazi na maamuzi ya kidola haiwezekani kubinafsisha kwa mtu hali ambayo inamfanya hata akili yake ijijenge kuwa serikali hii ni mali "yangu".

Waziri akisimama kuzungumzia umeme anasema serikali ya Magufuli imeamua hivi, wakati huo ni mpango wa kitaifa. Na mikoani RC akishughulikia kisina atasema hivyohivyo wakati visima hivyovya serikali hata Magufuli havijui.

Hatari ya tabia hii itafikia hata Polisi wakizuia maandamano au fujo kujikuta wakitoa amri "Serikali ya Magufuli inatoa watu wote watawanyike mara moja kwa amani la sivyo ...."

Viongozi warudi kwenye matari, tunayo SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA pekee.
Serikali yake mwisho nyumbani kwake hahahaha I like this, hongera kwa ushujaa huu na ukweli huu uliowazi
 
The Obama administration..!!!
Siku zote serikali ni ya rais husika na uongozwa kwa dira na ilani ya chama kilichomuingiza madarakani

The Obama administration..!!! Hii maana yake ni utawala wa Obama na si serikali ya Obama. Ni vitu viwili tofauti hapa. Utawala unaweza kunasibishwa na kiongozi aliye madarakani lakini si serikali. Huwezi kusikia neno serikali ya Obama bali utasikia serikali ya Marekani.
 
Sasa hivi viongozi wa serikali kuanzia mawaziri kuja chini wamejenga tabia ya kutoa maagizo huku wakitumia kauli kuwa serikali ya Magufuli inaagiza hili au lile na haitaki hili au lile.

Huu ni upotoshaji, hakuna serikali ya Magufuli popote hapa duniani zaidi ya nyumbani kwake, iliyopo ni ya Wananchi wa JMT inayoongozwa na Magufuli kama Rais aliyepewa ajira hiyo na masharti ya jinsi ya kufanya kazi na hao wananchi.

Huu mtindo wa kazi na maamuzi ya kidola haiwezekani kubinafsisha kwa mtu hali ambayo inamfanya hata akili yake ijijenge kuwa serikali hii ni mali "yangu".

Waziri akisimama kuzungumzia umeme anasema serikali ya Magufuli imeamua hivi, wakati huo ni mpango wa kitaifa. Na mikoani RC akishughulikia kisina atasema hivyohivyo wakati visima hivyovya serikali hata Magufuli havijui.

Hatari ya tabia hii itafikia hata Polisi wakizuia maandamano au fujo kujikuta wakitoa amri "Serikali ya Magufuli inatoa watu wote watawanyike mara moja kwa amani la sivyo ...."

Viongozi warudi kwenye matari, tunayo SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA pekee.

LAZIMA UONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) UTUPIE MACHO KAULI HII, INATIA SHAKA, KWA MUJIBU WA KATIBA YETU YA 1977, SERIKALI ITAUNDWA NA CHAMA CHA SIASA, NA KWA KIPINDI CHOTE TANGU TUINGIE KWENYE MFUMO WA VYAMA VINGI, CCM NDIYO IMEKUWA IKIPEWA RIDHAA NA WANANCHI YA KUUNDA SERIKALI, KWA MAGUFULI KUSEMA, "...............SERIKALI YA MAGUFULI!!! NI WAZI ANAVUNJA KATIBA YA NCHI, NI BORA HATA KAMA ANGEKUWA ANATAMKA, SERIKALI YA CCM INAYOONGOZWA NA MAGUFULI, AMA SERIKALI YA AWAMU YA TANO, LAKINI KWA SASA ANAKOSEA!!!
 
ahahaha

ahahaha!
Msigwa"Mhe Kaijage Naombe Hata Kiwanda Kimoja Kilicho Jengwa na Serikali ya Awamu ya Tano Mpaka Sasa"
Yeye Msigwa anataka kuaminisha watu chadema ingekua imeshinda kwa hii miezi sita wangekua wamejenga viwanda vingapi?
 
Back
Top Bottom