Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,432
- 73,078
Sasa hivi viongozi wa serikali kuanzia mawaziri kuja chini wamejenga tabia ya kutoa maagizo huku wakitumia kauli kuwa serikali ya Magufuli inaagiza hili au lile na haitaki hili au lile.
Huu ni upotoshaji, hakuna serikali ya Magufuli popote hapa duniani zaidi ya nyumbani kwake, iliyopo ni ya Wananchi wa JMT inayoongozwa na Magufuli kama Rais aliyepewa ajira hiyo na masharti ya jinsi ya kufanya kazi na hao wananchi.
Huu mtindo wa kazi na maamuzi ya kidola haiwezekani kubinafsisha kwa mtu hali ambayo inamfanya hata akili yake ijijenge kuwa serikali hii ni mali "yangu".
Waziri akisimama kuzungumzia umeme anasema serikali ya Magufuli imeamua hivi, wakati huo ni mpango wa kitaifa. Na mikoani RC akishughulikia kisina atasema hivyohivyo wakati visima hivyovya serikali hata Magufuli havijui.
Hatari ya tabia hii itafikia hata Polisi wakizuia maandamano au fujo kujikuta wakitoa amri "Serikali ya Magufuli inatoa watu wote watawanyike mara moja kwa amani la sivyo ...."
Viongozi warudi kwenye matari, tunayo SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA pekee.