Uchaguzi 2020 Upinzani, msiende mahakamani wala msihamasishe watu kuingia barabarani. Tuacheni Wananchi tuyaone wenyewe

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,156
Sina mengine zaidi ya hayo, heading inajieleza vizuri.

Ni kweli mtakosa mapato, lakini mnaweza kujibidisha na kupata shughuli nyingine hata ikiwezekana kilimo.

Tuachieni hii miaka mitano ili tujionee wenyewe.

Msihangaike kwenda mahakamani maana huko mtapoteza fedha na muda wenu bure.

Msihangaike kuhamasisha maandamano maana police wakifyatua risasi na raia wakafa, mtalaumiwa bure!

Tuachieni miaka hii mitano tujihakikishie Kama kweli maana ya upinzani ipo kwenye vyama vya siasa au mioyoni mwa watu?

Kaeni pembeni tuone Kama kweli nyie ndio chanzo cha kukosekana kwa huduma za jamii huku kwetu?

Kaeni pembeni tuone Kama kweli nyie ndo mlikuwa sababu ya umasikini wa Watanzania wengi?

Kaeni pembeni ili wananchi waanze kufurahia maziwa na asali walivyovikosa miaka yote hiyo.

Nasema kaeni pembeni kwasababu mmejaribu kutusemea ila tumeshindwa kuwaelewa.

Haina haja ya Mmarekani na wa yuropa kuanza kutusemea! Waambieni nao watuache, tuna jambo letu miaka mitano hii.

Tena waambieni wawe wa kwanza kumpa kongole muheshimiwa kwa ushindi wake wa kishindo na madiwani na wabunge wote! Wasimseme wasije kumconfusi!

Kwa kweli mkijikalia pembeni mkaanza kufanya shughuli nyingine nje ya siasa kuanzia Leo mtakuwa mmetusaidia sana sisi wanyonge kuondoka kwenye unyonge wetu.

Mtakuwa mmetusaidia sana maana mishahara itapanda, huduma za jamii zitabireshwa, ajira zitapatikana, shule zitaboreshwa, uhuru na haki vitatamalaki na Mambo kede kede.

Msiandamane wala kulalamika lalamika ili msimconfyuzi mshindi akaanza kuloose focus na kugombana na nyie!

Muacheni na mtuache na sisi tuyaone wenyewe!

Ni hayo tu! Tanzania ni yetu watanzania, UN, USA na wengine hawawezi kutuonea huruma tusipoanza sisi kujionea huruma na hata wakituonea huruma watakuwa na jambo lao nyuma ya pazia!

Waambieni watuache tuyaone wenyewe!
 
Kabisa, ni muda wa kuyashukudia maajabu aliyoahidi jiwe, ni muda wa viwanda vyote moshi kufufuliwa, ni muda wa arusha kuwa California, ni muda wa Tanzania kuwa Ulaya.

Maendelo sasa yatakuwa kila mahali na hakika mabeberu watatukoma. kina lissu kazi yao imetosha, wametutetea sana
 
Hii hoja murua kabisa. Wapinzani na wale wanaoitwa mababeru hebu watupishe kwanza tujionee wenyewe miaka hii mitano. Watuache kama shubiri tuionje na kama ni asali tuifurahie kwa raha zetu. Kwa kweli hebu tuachieni tuisome hii namba kwanza kwa raha zetu.
 
Upinzani inabidi wasome alama za nyakati tu kwa sasa, hapa Tanzania hatuna upinzani wa ukweli ni kelele tu zisizo na tija. Mtu anakwenda bungeni kupiga kelele na kuleta bifu ili aandikwe mitandaoni lakini hana msaada wowote jimboni kwake, mfano Halima Mdee, Sugu, Zitto Kabwe, Lissu, na wapuuzi wengine. Tunataka upinzani wa ukweli hapa Tanzania.
 
Uko sahihi kabisa. Wapinzani inabidi wajipange upya, tena waje na vijana wapya, na waache masuala ya kupinga kila kitu, Kuna kupinga lakini waangalie kwnaza wanapinga nini, na wapi. Kipindi cha corona ndio chadema walipoteza watu wengi sana.
 
Upinzani inabidi wasome alama za nyakati tu kwa sasa, hapa Tanzania hatuna upinzani wa ukweli ni kelele tu zisizo na tija. Mtu anakwenda bungeni kupiga kelele na kuleta bifu ili aandikwe mitandaoni lakini hana msaada wowote jimboni kwake, mfano Halima Mdee, Sugu, Zitto Kabwe, Lissu, na wapuuzi wengine. Tunataka upinzani wa ukweli hapa Tanzania.
Okay, mko wenyewe sasa. Enjoy
 
Sina mengine zaidi ya hayo, heading inajieleza vizuri.

Ni kweli mtakosa mapato, lakini mnaweza kujibidisha na kupata shughuli nyingine hata ikiwezekana kilimo...
Mkuu twaona raha sana , si muda tutaombana chumvi mtaani, hacha tufurahi na uchaguzi huu, muda utafika tutalia wote na kuumia wote, bila kujali una chama ,huna chama au unatoka chama gani mda mwalim
 
Similar Discussions

87 Reactions
Reply
Back
Top Bottom