Uchaguzi wa mwaka huu 2020, maamuzi yalikuwa mikononi mwa wasimamizi wa vituo

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Habari za Leo wana jamvi,

Mimi bado niko na wasimamizi wa vituo vya kupigia kura mwaka huu.

Mwanzo siku mbili kabla ya uchaguzi nilisikia tetesi kwamba wasimamizi walikuwa wakiitwa mara kwa mara kupewa maelekezo maalumu na mikakati ya kufikia malengo.

Baadhi walinyong'onyea baada ya kupewa maelekezo hayo na kutokuwa na la kufanya kwasababu ya vitisho.

Baada ya uchaguzi nimepiga story na waliokuwa wasimamizi wa vituo kadhaa. Ki ukweli wao wenyewe hawana amani, hawana furaha, nafsi zinawasuta, na wanaona aibu mtaani!

Yote kwa yote uchaguzi umeshaisha na nafsi zitaendelea kuwasuta kwa kukubali kufanya walichokifanya kwa malipo ya Tsh. 355,000/- kwa 245,000/- kwa wasimamizi wasaidizi ambao wengi wao hawakujua kilichokuwa kinaendelea zaidi ya kushuhudia maajabu ya uchakachuaji na kuambiwa hawaruhusiwi kuhoji chochote.

Lengo langu sitaki kujadili mbinu walizopewa na namna walivyozitekeleza, hapana! Hili watalijadili wenyewe siku aibu zikiwashika hatamu!

Lengo langu nataka tujikite kujadili aina ya wasimamizi waliokubali kutekeleza hicho walichofanya.

Kwa asilimia kubwa wasimamizi wa vituo walikuwa walimu. Hawa walitekeleza maagizo waliyopewa chini ya usaidizi mkubwa wa askari polisi aliyekuwa na jukumu la kulinda kituo.

Hawa walimu walikuwa na kilasababu ya kusoma aina ya mgombea na kutumia mbinu zile zile walizopewa kumpitisha mgombea anayeonekana kuja kutetea maslahi yao na ya wananchi wengine.

Kwa mfano, moja ya maelekezo yalikuwa ni kuweka tick kwa mgombea wa chama tawala nyingi iwezekanavyo hasa kwa wale ambao vituo vyao wapiga kura hawakwenda wengi. Mfano kituo ambacho kina wapiga kura walioandikishwa 400+ labda mpaka saa sita wamefika chini ya 100, msimamizi alikuwa na maelekezo maalumu ya kucheza na namba namna ya kubalance angalau ionekane wamefika 300+. Sasa hapa kura 200 kwa maelekezo yale yale angeweza kuamua ampitishe nani!
Kuhusu daktari la wapiga kura usiniuluze lilifanywa nini! Hii si sehemu ya majadala wangu!

Kila siku walimu na askari polisi ndio wanaolalamika sana maslahi yao kutopewa kipaumbele na watawala walipo na waliopita.

Halafu hawa hawa walimu na askari polisi wamepewa mbinu za ushindi na Siri ya ushindi.

Ilishindikana nini kuji mobilize pembeni na wao wakafanya yao kwa kutumia siraha ile ile waliyopewa?

Hivi kweli hata Kama walipewa vitisho, inawezekana kuwatisha watu wote kwa pamoja?

Kwa mfano, Jimbo moja linaweza kuwa na wasimamizi karibu 700+ kwa vituo vyote. Ukijumlisha na askari polisi walifika karibu 900+ au hata 1000+

Wote walifanyiwa semina kwa pamoja ukumbi mmoja. Maelekezo walipewa kwa pamoja!

Yaani kweli watu 1000+ unaweza kuwatisha wakatishika kwa pamoja!?

Ndiomaana sioni mantiki ya sisi kuendelea kuilaumu serikali kwa yanayoendelea! Serikali haiwezi kutekeleza jambo lolote pasipo kuwatumia watu! Na hawa watu ndio sisi tunaolalamika kila siku

Ifikie mahali tunapoelekezwa kufanya jambo ambalo ni kinyume na uhalisia tukatae! Hasa mnapokuwa katika kundi. Ukiwa peke yako utaogopa ili mkishakuwa wawili watatu mkawa na msimamo mmoja, wanaotoa maelekezo ndio watakao ogopa

Mwisho kabisa ushauri kwa viongozi wa upinzani!

Narudia tena ushauri nilioutoa humu humu kwenye mada tofauti.

Hakuna haja ya kuhamasisha maandamano! Tuliohusika kutengeneza haya matokeo ni sisi watanzania! Hakuna mkenya wala mrundi alikuja kusimamia huu uchaguzi! TUACHIENI HII MIAKA MITANO YA KIJANI KITUPU TUYAONE WENYEWE MAANA TUMEYATAKA WENYEWE!

Haiwezekani askari anayelalamika maisha magumu atumike kupindua matokeo halafu nyie muhamasishe maandamano

Haiwezekani mwalimu anayelalamika serikali kutomjali atumike kuchakachua matokeo halafu nyie muhamasishe maandamano

Fanyeni shughuli nyingine muimarishe vyama vyenu ili mianya yote ya wizi muizibe huko mbeleni yasitokee tena

Jiimarisheni zaidi. Toeni elimu zaidi na ikiwezekana andaeni vijana imara watakaokuwa trained kuwa mawakala wa chaguzi mbalimbali ambao watakuwa aware na mbinu mbalimbali zinazotumika na wapinzani wenu kujazilizia pale kura zinapokuwa haziwatoshi

Vinginevyo kuendelea na maandamano pasipo kuweka mikakati thabiti ya mbeleni itakuwa ni kupoteza muda

Yangu ni hayo tu kwa leo. Binafsi kwa sasa sioni Kama maandamano yatasaidia chochote!
 
Back
Top Bottom