Upepo wageuka tena, Juma Duni Haji kuwa Mgombea Mwenza wa Lowassa

Naomba kuuliza...

Hivi inawezekana Mgombea na Mgombea mwenza wake wakatoka vyama tofauti???...

Mkuu hawatoki vyama tofauti maana Duni Haji amejivua uanachama wa cuf tangu jana.
Kwahiyo wataenda kama chadema na si ukawa tena maana ukawa hautambuliki kisheria hivyo basi kuachiana majimbo kwa mlengo wa ukawa ni kiini macho.
 
WATANZANIA hatutaki mabadiliko. mimi nashukuru nina mshahara wangu japo kiduchu. ila nawahurumia wakulima na wabeba kago wanaweza kuuza 0713 miaka ijayo, hali ni ngumu.
 
Kuna ssehemu nimesoma kuwa Rostam kaenda kwa Magufuli
na kama Jussa kakataa akisema haoni uwezekano wa kushinda basi
Lowassa 'amesha geukwa'....kuna kitu Rostam na Jussa wanakijua ambacho Lowassa hakijui
Ninachojua MasterMind wa michezo yote ni EL mwenyewe, Hata kipindi EL anarudi nyuma kumpisha JK Rostam aligoma ili kwasababu EL ndiye MasterMind -Alikubali.

Inawezekana ni mbinu mbadala kwa EL kumwadaa Magufuli . Ila kwa upande mwingine wa shilingi inawezekana.
 
Lizabon ni moja kati ya watu wa karibu na Padri hivyo basi maamuzi yoyote ya Ukawa ni lazima Dadri. afahamishwe na hapo ndipo anampatia lizabon pass ya kuhariri ili aitume humu ikikolezwa na viashiria vya pesa ili kumchafua Lowassa.
 
wadau amani iwe kwenu.


hii sasa pindua pindua na inaonesha jamaa wanafanya kazi kwa kubahatisha.


mtakumbuka kuwa hapo awali kulikuwa na minong'ono kwamba dr slaa ndiye angekuwa mgombea urais wa ukawa na mgombea mwenza wake angekuwa juma duni haji. Hata hivyo, kutokana na lowasa kuteuliwa kuwa mgombea urais wa chadema na ni dhahiri atakuwa mgombea wa ukawa, lowasa alimpendekeza ismail jussa ladhu kuwa mgombea mwenza wake. Hata hivyo, taarifa zilizoripotiwa jana ni kwamba, jusa alikataa pendekezo la kuwa mgombea mwenza na hivyo viongozi wa ukawa wakampendekeza aliyekuwa mwanasheria wa zanzibar, othman masoud kuchukua nafasi hiyo.


hata hivyo, taarifa mpya ni kwamba othman masoud naye amekataa pendekezo hilo kwa madai kuwa ana mambo mengi ya kitaifa na kimataifa yanamkabili. Kutokana na pendekezo hilo kugonga mwamba, ilibidi mpunga utembee. Jana muda wa mchana, maalim seif sharif hamad akitumia usafiri wa makamu wa kwanza wa rais alienda ofisi ya lowasa iliyopo masaki dar es salaam akiambatana na mwanasiasa mkongwe, juma duni haji. Kwenye ofisi ya lowasa alikuwepo apson mwang'onda, james mbatia na edward lowasa.


viongozi hao kwa pamoja walitumia muda mwingi kumshawishi juma duni haji ili awe mgombea mwenza kama ilivyopangwa hapo awali. Hata hivyo, juma duni alionekana kukataa hasa pendekezo la kumtaka ahame cuf na kujiunga chadema. Hata hivyo, viongozi hao walimhakikishia kuwa hakuna atakachopoteza na kwamba kwa vyovyote itakavyokuwa, uanachama wake wa cuf utalindwa. Lowasa alisema kuwa hawana muda zaidi wa kumtafuta mgombea mwenza na kwamba tumaini pekee limebaki kwake juma duni haji.


baada ya kutafakari kwa muda kidogo, juma duni haji alikubali pendekezo hilo kwa masharti. Kwamba, apewe shilingi milioni 500 kama malipo yake kwa kukubali kujivua uanachama wa cuf. Pia endapo ukawa hawatashinda nafasi ya urais, awe analipwa mshahara wa shilingi milioni kumi kwa mwezi kwa kipindi cha miaka 5 ambacho atakuwa nje ya siasa za zanzibar.


masharti hayo yamekubaliwa na lowasa ambapo jana juma duni haji amepewa shilingi milioni 50 kama bonus na leo atapewa shilingi milioni 500 alizoomba na hivyo kufanya jumla ya kiasi chote atakachopewa kuwa shilingi milioni 550.


kutokana na hali hiyo, juma duni haji anatarajiwa kutangazwa rasmi leo mlimani city jijini dar es salaam ambapo chadema wanafanya mkutano wa kumtangaza mgombea urais na mgombea mwenza.


kwa haya yanayoendelea, yanatukumbusha kitu kimoja cha msingi. Kwamba, chadema hawakujiandaa kwa ajili ya kusimamisha mgombea urais na mgombea mwenza. Mgombea urais katoka ccm na mgombea mwenza wamemwazima kutoka cuf. Hii inanikumbusha ya mrisho ngasa kuchezea simba na juma kaseja kusajiliwa na yanga.


kukumbusha awabahatishi n wewe kupapasa.macho story ya juma duni.iko jf siku.nyingi sana sana....humu labda uso
i tu
 
Kama kila bandiko unaloweka hapa kuhusu Lowasa na Chadema unalipwa, mpaka oktoba utakuwa umekusanya mpunga mrefu sanaa!!
Umejitahidi sana kuhangaika, in fact ni zaidi ya kuku anayetaka kutaga!!
 
Lizabon ni moja kati ya watu wa karibu na Padri hivyo basi maamuzi yoyote ya Ukawa ni lazima Dadri. afahamishwe na hapo ndipo anampatia lizabon pass ya kuhariri ili aitume humu ikikolezwa na viashiria vya pesa ili kumchafua Lowassa.
Duh! Mkuu, ni padri yupi huyo? Sina uswahiba na mapadri wala kiongozi yeyote wa CHADEMA
 
Kama kila bandiko unaloweka hapa kuhusu Lowasa na Chadema unalipwa, mpaka oktoba utakuwa umekusanya mpunga mrefu sanaa!!
Umejitahidi sana kuhangaika, in fact ni zaidi ya kuku anayetaka kutaga!!
Mkuu, hilo la kulipwa ni hoja yako. Ila mimi nawawekea humu kwa manufaa ya kila maomaji
 
anayejua sheria anijuze kuhusu mgombea mwenza kutoka chama kingine..uhalali wake ukoje??
 
anayejua sheria anijuze kuhusu mgombea mwenza kutoka chama kingine..uhalali wake ukoje??

kisheria haikubaliki na ndio maana Haji Duni kajivua kutoka cuf na kujiunga chadema ili ikidhi vigezo vya sheria ya mgombea mwenza lazima atoke chama kimoja na mgombea wa urais
 
Kuna ssehemu nimesoma kuwa Rostam kaenda kwa Magufuli
na kama Jussa kakataa akisema haoni uwezekano wa kushinda basi
Lowassa 'amesha geukwa'....kuna kitu Rostam na Jussa wanakijua ambacho Lowassa hakijui

Ngoja niwe mpiga lamli wa Kigiriki...Zanzibar na hazina zake,lol
 
Wadau amani iwe kwenu.


Hii sasa pindua pindua na inaonesha jamaa wanafanya kazi kwa kubahatisha.


Mtakumbuka kuwa hapo awali kulikuwa na minong'ono kwamba Dr Slaa ndiye angekuwa Mgombea Urais wa UKAWA na mgombea mwenza wake angekuwa Juma Duni Haji. Hata hivyo, kutokana na Lowasa kuteuliwa kuwa mgombea Urais wa CHADEMA na ni dhahiri atakuwa mgombea wa UKAWA, Lowasa alimpendekeza Ismail Jussa Ladhu kuwa mgombea mwenza wake. Hata hivyo, taarifa zilizoripotiwa jana ni kwamba, Jusa alikataa pendekezo la kuwa Mgombea Mwenza na hivyo viongozi wa UKAWA wakampendekeza aliyekuwa Mwanasheria wa Zanzibar, Othman Masoud kuchukua nafasi hiyo.


Hata hivyo, taarifa mpya ni kwamba Othman Masoud naye amekataa pendekezo hilo kwa madai kuwa ana mambo mengi ya kitaifa na kimataifa yanamkabili. Kutokana na pendekezo hilo kugonga mwamba, ilibidi mpunga utembee. Jana muda wa mchana, Maalim Seif Sharif Hamad akitumia usafiri wa Makamu wa Kwanza wa Rais alienda Ofisi ya Lowasa iliyopo Masaki Dar es Salaam akiambatana na mwanasiasa mkongwe, Juma Duni Haji. Kwenye ofisi ya Lowasa alikuwepo Apson Mwang'onda, James Mbatia na Edward Lowasa.


Viongozi hao kwa pamoja walitumia muda mwingi kumshawishi Juma Duni Haji ili awe mgombea mwenza kama ilivyopangwa hapo awali. Hata hivyo, Juma Duni alionekana kukataa hasa pendekezo la kumtaka ahame CUF na kujiunga CHADEMA. Hata hivyo, viongozi hao walimhakikishia kuwa hakuna atakachopoteza na kwamba kwa vyovyote itakavyokuwa, uanachama wake wa CUF utalindwa. Lowasa alisema kuwa hawana muda zaidi wa kumtafuta mgombea mwenza na kwamba tumaini pekee limebaki kwake Juma Duni Haji.


Baada ya kutafakari kwa muda kidogo, Juma Duni Haji alikubali pendekezo hilo kwa masharti. Kwamba, apewe shilingi milioni 500 kama malipo yake kwa kukubali kujivua uanachama wa CUF. Pia endapo UKAWA hawatashinda nafasi ya Urais, awe analipwa mshahara wa shilingi milioni kumi kwa mwezi kwa kipindi cha miaka 5 ambacho atakuwa nje ya siasa za Zanzibar.


Masharti hayo yamekubaliwa na Lowasa ambapo jana Juma Duni Haji amepewa shilingi milioni 50 kama bonus na leo atapewa shilingi milioni 500 alizoomba na hivyo kufanya jumla ya kiasi chote atakachopewa kuwa shilingi milioni 550.


Kutokana na hali hiyo, Juma Duni Haji anatarajiwa kutangazwa rasmi leo Mlimani City Jijini Dar es Salaam ambapo CHADEMA wanafanya mkutano wa kumtangaza mgombea Urais na Mgombea Mwenza.


Kwa haya yanayoendelea, yanatukumbusha kitu kimoja cha msingi. Kwamba, CHADEMA hawakujiandaa kwa ajili ya kusimamisha Mgombea Urais na Mgombea Mwenza. Mgombea Urais katoka CCM na Mgombea Mwenza wamemwazima kutoka CUF. Hii inanikumbusha ya Mrisho Ngasa kuchezea Simba na Juma Kaseja kusajiliwa na Yanga.


Hivi ndugu yangu unaushahidi wa unayoandika hapa
 
Soma UZI WA NDUGU YAKO HUU.................. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/899678-prof-lipumba-ajiuzulu-uenyekiti-cuf.html

Siwezi kununulika kirahisi

Sasa wewe kama huwezi kununulika kirahisi ina maana unaweza kununulika kwa dau kubwa. Inaonyesha ndicho unachotegemea kwa hizi threads zako. Na kama ni hivyo kwa nini akina Duni uwasingizie kununulika kirahisi? Nimegundua hapa kuna kitu unatafuta UKAWA
 
Mkuu, mbona leo unachangia kwa unyonge sana?



Mwenzako kapiga goli la mkono huko Mtama wewe unashinda hapa JF kumuongelea Lowasa.





Makada wa Chama cha Mapinduzi ambao walikuwa wagombea nafasi ya Ubunge kura za maoni Kupitia CCM kutoka katika Majimbo ya Mtama na Mchinga Lindi, wakiwa katika mkutano na waandishi wa Habari Mkoani lindi katika Hoteli ya Lindi Oceanic.


Mwenyekiti wa wagombea akiongea na Waandishi wa habari wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari baada ya kutolewa kwa Matokeo ya Chama cha Mapinduzi kwa nafasi za Ubunge na Udiwani katika Majimbo ya Mtama na Mchinga.


Mgombea wa Nafasi ya Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi Riziki Lulida akionesha Moja ya kitabu cha karatasi za Kupigia kura ambavyo alibainisha kuwa vilikuwa vimezagaa katika sehemu ya kupigiakura kinyume na Utaratibu.


Na. Mwandishi Wetu, Lindi
Wagombea waliokuwa wakiwania Kukiwakilisha Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa nafasi ya Ubunge katika Majimbo ya Mtama na Mchinga wameweza kueleza masikitiko yao dhidi ya wagombea wenzao wawili ambao wametangazwa kuwa wao ndio washindi katika maeneo hayo mawili ambao kwa Jimbo la Mtama alietangazwa ni Nape Mnauye ambaye aliweza kufuatwa kwa karibu na Mgombea Seleman Methew, Kwa jimbo la Mchinga Said Mtanda ametangazwa kuwa Mshindi Huku akifuatiwa na Mebu.
Kufuatia Matokeo hayo yaliyoweza kutangazwa na Chama hicho katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Mkoa Lindi, wagombea hao wameeleza kutoyakubali matokeo hayo kwani wamebainisha kuwa kuna Udanganyifu mkubwa umetumika, Lalamiko la kwanza lililotolewa na wagombea hao ni Kutopatiwa Akidi ya wanachama kabla ya Kupiga kura, La pili ni Mgombea kusafirisha watu kutoka eneo moja kupeleka eneo jingie kwa ajili ya kupiga kura na Jambo la tatu kuongeza karatasi za kupigia kura ambazo tayari zimesha pigwa tiki katika masanduku ya kupigia kura.
Wagombea hao wameongeza yakuwa wapiga kura wengine waliopiga kura si wa wanachama wa Chama cha Mapinduzi ni wanachama cha wananchi (C.U.F) na wamebainisha Ushahidi wanao. Hivyo kufuatia matukio hayo wagombea hao wameweza kubainisa kuwa Uleusemi wa Katibu Uenezi wa Chama hicho alioutoa siku kadhaa zilizopita kuwa CCM itashinda kwa kishindo hata kwa Goli la Mkono limeweza kutimia kwani mazingira ya Ushindi wake katika Jimbo la Mtama umegubikwa na Udanganyifu mkubwa.
Kufuatia Udanganyifu huo wa wagombea hao wameweza kubainisha kuwa hawako tayari kuwaunga mkono wagombea hao waliotangazwa na Chama hicho kama washindi na kusema kama Chama kitakuwa sikivu basi Uchaguzi huo Urudiwe la sivyo wao hawakotayari kuwaunga mkono katika Uchaguzi Mkuu.
Aidha Mgombea aliyeshika nafasi ya pili katika jimbo la Mtama ameweza kutoa rai ya kuwa CCM kama itaruhusu hali hii inayoendelea kwa sasa basi ni dhahiri kuwa chama hicho kiko mbioni kupotea kwani wanachama wake wa ngazi za juu wanatumia Udanganyifu mkubwa kupata nafasi za uongozi hususani kutoa rushwa na kutengeneza karatasi za kupigia kura zisizo rasmi.
 
Back
Top Bottom