Upepo wageuka tena, Juma Duni Haji kuwa Mgombea Mwenza wa Lowassa

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau amani iwe kwenu.


Hii sasa pindua pindua na inaonesha jamaa wanafanya kazi kwa kubahatisha.


Mtakumbuka kuwa hapo awali kulikuwa na minong'ono kwamba Dr Slaa ndiye angekuwa Mgombea Urais wa UKAWA na mgombea mwenza wake angekuwa Juma Duni Haji. Hata hivyo, kutokana na Lowasa kuteuliwa kuwa mgombea Urais wa CHADEMA na ni dhahiri atakuwa mgombea wa UKAWA, Lowasa alimpendekeza Ismail Jussa Ladhu kuwa mgombea mwenza wake. Hata hivyo, taarifa zilizoripotiwa jana ni kwamba, Jusa alikataa pendekezo la kuwa Mgombea Mwenza na hivyo viongozi wa UKAWA wakampendekeza aliyekuwa Mwanasheria wa Zanzibar, Othman Masoud kuchukua nafasi hiyo.


Hata hivyo, taarifa mpya ni kwamba Othman Masoud naye amekataa pendekezo hilo kwa madai kuwa ana mambo mengi ya kitaifa na kimataifa yanamkabili. Kutokana na pendekezo hilo kugonga mwamba, ilibidi mpunga utembee. Jana muda wa mchana, Maalim Seif Sharif Hamad akitumia usafiri wa Makamu wa Kwanza wa Rais alienda Ofisi ya Lowasa iliyopo Masaki Dar es Salaam akiambatana na mwanasiasa mkongwe, Juma Duni Haji. Kwenye ofisi ya Lowasa alikuwepo Apson Mwang'onda, James Mbatia na Edward Lowasa.


Viongozi hao kwa pamoja walitumia muda mwingi kumshawishi Juma Duni Haji ili awe mgombea mwenza kama ilivyopangwa hapo awali. Hata hivyo, Juma Duni alionekana kukataa hasa pendekezo la kumtaka ahame CUF na kujiunga CHADEMA. Hata hivyo, viongozi hao walimhakikishia kuwa hakuna atakachopoteza na kwamba kwa vyovyote itakavyokuwa, uanachama wake wa CUF utalindwa. Lowasa alisema kuwa hawana muda zaidi wa kumtafuta mgombea mwenza na kwamba tumaini pekee limebaki kwake Juma Duni Haji.


Baada ya kutafakari kwa muda kidogo, Juma Duni Haji alikubali pendekezo hilo kwa masharti. Kwamba, apewe shilingi milioni 500 kama malipo yake kwa kukubali kujivua uanachama wa CUF. Pia endapo UKAWA hawatashinda nafasi ya Urais, awe analipwa mshahara wa shilingi milioni kumi kwa mwezi kwa kipindi cha miaka 5 ambacho atakuwa nje ya siasa za Zanzibar.


Masharti hayo yamekubaliwa na Lowasa ambapo jana Juma Duni Haji amepewa shilingi milioni 50 kama bonus na leo atapewa shilingi milioni 500 alizoomba na hivyo kufanya jumla ya kiasi chote atakachopewa kuwa shilingi milioni 550.


Kutokana na hali hiyo, Juma Duni Haji anatarajiwa kutangazwa rasmi leo Mlimani City Jijini Dar es Salaam ambapo CHADEMA wanafanya mkutano wa kumtangaza mgombea Urais na Mgombea Mwenza.


Kwa haya yanayoendelea, yanatukumbusha kitu kimoja cha msingi. Kwamba, CHADEMA hawakujiandaa kwa ajili ya kusimamisha Mgombea Urais na Mgombea Mwenza. Mgombea Urais katoka CCM na Mgombea Mwenza wamemwazima kutoka CUF. Hii inanikumbusha ya Mrisho Ngasa kuchezea Simba na Juma Kaseja kusajiliwa na Yanga.


 
Naomba kuuliza...

Hivi inawezekana Mgombea na Mgombea mwenza wake wakatoka vyama tofauti???...
 
Naomba kuuliza...

Hivi inawezekana Mgombea na Mgombea mwenza wake wakatoka vyama tofauti???...
Haiwezekani. Ndo maana Mgombea Urais, Lowasa amehama CCM na kuhamia CHADEMA huku Mgombea Mwenza akiukana uanachama wake wa CUF na kujiunga na CHADEMA ili kutimiza matakwa ya kisheria. Siasa za ulaghai hizi
 
Kuna ssehemu nimesoma kuwa Rostam kaenda kwa Magufuli
na kama Jussa kakataa akisema haoni uwezekano wa kushinda basi
Lowassa 'amesha geukwa'....kuna kitu Rostam na Jussa wanakijua ambacho Lowassa hakijui
 
Kila kitu atanunua

Baada ya hapo ni kukusanya nyumbu na kuwaonyesha majani tu na viroba
Uwekezaji wa Lowasa kwenye nafasi ya urais ni mkubwa sana. Akikosa inabidi ajinyonge
 
katika kuhakikisha dhana ya UKAWA inadumishwa nadhani hayo yanayofanyika yapo sawia, suala halikuwa lazima wote watoke cdm bali maridhiano yawepo kuhakikisha kuna dhana ya ushirikishwaji wa wadau muhimu
 
Tumemkosa Yericko hapa jukwaani sasa naona Lizaboni anaziba nafasi kweli kweli, Dada angu hii taarifa ina ya kupewa hela Mil 550 na mil 10 kila mwezi kwa miaka mitano sawa na mil 600 zina mashiko kweli?
 
Back
Top Bottom