MzalendoHalisi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2007
- 4,520
- 1,368
Mkoa wa Kilimanjaro una mawaziri wanane huku ukiwa na wakazi wapatao milioni 1.2, lakini Mkoa wa Kigoma ambao una wakazi karibu milioni 1.7 hauna waziri hata mmoja mtu hupaswi kuzungumza kama huna takwimu, alisema.
Source: Mbowe- gazeti Tanzania Daima 20.12.2007
1. Ni kweli CCM inatoa upendeleo kwa kuteua mawaziri wengi zaidi toka Kilimanjaro? Wakati wa JKN, AHM, BWM hali hii ilikuwaje?
2. Katika Baraza mawaziri 60 kwa mikoa 21 angalau basi kila mkoa upewe nafasi 3. Inakuwaje Kilimanjaro wana eight Ministers yaani 14%? Je mikoa mingine hakuna wabunge wenye uwezo?
3. Ni kigezo gani JK anatumia kuteua mawaziri- je ni uwezo? Urafiki na ushkaji? Others?
Yes.... hupaswi kuzungumza kama huna takwimu...Kilimanajro haina mawaziri 8 ktk cabinet.
Tuache unfukunyuku na majungu
Masatu,
Mawaziri 8- ni data ya Mbowe- mimi nimeweka tu hapa tujadili!
Hebu tuwataje 1. Mramba 2. Maghembe 3. Chami 4. (Marehemu. Mrs. Mbatia) 5. Meghji??? 6. Rita Mlaki??? 7. ???? 8. ???? 9. ?????
Yes.... hupaswi kuzungumza kama huna takwimu...Kilimanajro haina mawaziri 8 ktk cabinet.
Tuache unfukunyuku na majungu
Kwa wale walikuwa kwenye press conference watathibitisha kuwa alichosema Mbowe ni kwamba kuna mawaziri na manaibu waziri takribani 8 wenye asili ya Kilimanjaro.
Kauli hii ni sahihi kabisa, inajumuisha wanaotoka majimbo ya Kilimanjaro na wenye asili ya Kilimanjaro hata kama hawatoki majimbo ya Kilimanjaro. Na aliweka bayana kuwa ni wakati Kikwete anatangaza baraza alipoingia madarakani.
Na ukitaka kujua kwamba Mbowe alifahamu kabisa tofauti ya mawaziri na manaibu waziri itazame habari yenyewe kwa ukamilifu wake kwamba wakati anazungumzia Kigoma alisema kabisa kwamba haina waziri hata mmoja kwenye cabinet, na akataja kuwa kuna manaibu wawili ambao pamoja na mambo mengine huishia tu kujibu maswali bungeni lakini si sehemu ya wajumbe kamili wa baraza la mawaziri.
Na Mbowe hakurupuka tu kusema hayo, alikuwa akijibu swali la Mwandishi wa Gazeti la CCM la Uhuru kwamba je, ni ukweli CHADEMA inaukabila? Je, ni kweli kuwa CHADEMA ni chama cha wachaga?
Awali Mbowe alikataa kujibu swali hilo na kumwachia Slaa kwa kuwa yeye Mbowe ni mchaga ataonekana anajitetea. Dr Slaa akaweka bayana kuhusu uteuzi wa viti maalumu ambao mwandishi alitoa kama mfano. Mbowe akaongezea ufafanuzi na katika kuzungumza ndipo alipoweka bayana kwamba wanapandikiza maneno ya ukabila ni CCM na kwamba CCM hao hao hawasemi kwamba Baraza la Kikwete lina ukabila kwa kuweka mbele wachaga lakini ni wepesi wa kusema kwamba CHADEMA ni ya wachaga. Mbowe alieleza wazi kwamba wachaga kihistoria wako mstari wa mbele na wamesambaa nchi nzima. Sasa kama taifa tunapaswa kutazama picha pana zaidi badala ya kukurupuka kunyooshea kidole CHADEMA. Na ilielezwa wazi jinsi safu ya uongozi ya CHADEMA ilivyo na sura ya kitaifa. Mbowe alifikia hatua ya kutamka kwamba kama suala la ukabila lingekuwa ni hoja basi CCM ndio chama cha kwanza kwa ukabila. Na aliweka bayana kwamba hata katika viti maalumu vya CCM asilimia kubwa ni wachaga!
CCM hupenda kuanzisha mijadala bila kujitazama kwa kweli...
JJ

Mnyika wewe na Mwenyekiti wako, nadhani silaha zimewaishia, rudini shule tena,,, mbona mna watu wazuri kama Kitila wangepitia mnayotaka kuongea kabla ya kuyatoa hadharani,,, huu ni upuuzi mtupu!!!
Rita amechagula Dar es Salaam, mambo ya kutafuta anatokea wapi ni uupuzi wa hali ya juu!!!
Hivi tunapouliza Wabunge wa Dar es Salaam,,, inamaana tutafuta wazaramo na wadengereko tu!!! are you saying Dar es Salaam haina wabunge,,, maana huenda wote wana-asili ya baraa...
Da!!! Mkumbukeni Kambarage kidogo kwenye Dhambi hii mnayotaka kufanya!!! Labda mtasahau kidogo...

Mnyika,
Hii habari ya kufuatilia mtu ana asili ya wapi wakati ni mtanzania ndiyo tunayopinga sisi. Yaani hata nikichaguliwa sehemu lazima museme asili yangu ni wapi, mbona huu ni ubaguzi wa kutisha. Kwa msingi huo, tuna mawaziri wenye asili ya Kenya (Mungai), Uganda (Karamagi), nk? Ni kigezo gani mnatumia kusema "asili" ya wapi sijui? Yaani hata mie leo nikichaguliwa kuwa diwani wa kata ya Terrat halafu kama "zali" tu nikaukwaa umeya, mtaanza kusema nina asili ya Kenya! Jamani, nini hii?
Mnajua ninyi CHADEMA matatizo yenu ni kwamba mnatumia makosa kusahihisha makosa. Hiyo hasara zake ni kubwa sana. Unapoulizwa swali linalohusu ubaguzi nawe ukalijibu kibaguzi, basi wewe ndio unaonekana mbaguzi zaidi. Mtu akakutukana nawe pia ukamjibu kwa kumtukana, basi nyote mu watukanaji. Hebu jaribuni kutumia busara zaidi.
tatizo la uchawi ni kuwa ukiloga na wewe unadhani unalogwa! kwa hiyo mnabakia kulogana!