Updates za Corona Tanzania

Updates za Corona Tanzania

.
Eti wachezaji wasishikane mikono, wakati mpira unapigwa kichwa na majasho kibao, baada ya hapo anapiga mwingine na mwingine! Wachezaji wanasukumana uwanjani n.k, ukijaribu kufikiri kwa sauti utagundua tahadhari zinazotolewa ni zaidi ya mzaha aisee!? View attachment 1390398View attachment 1390399

Sent using Jamii Forums mobile app
IMG-20200316-WA0079.jpeg


Jr
 
Mtanisamehe nina la kuwahoji mnaosema Mungu anatulinda!
Mi naona kama hamna akili mnaosema hivyo!!
Kwani nyinyi mnalindwa ila waliopo china hawalindwi!!! Okay Hivyo Mungu wenu ni mbaguzi Kuna mahali analinda watu Kuna mahali anawaacha wafe!!!

Hivi Afrika kuwaza huwa mnatumia Nini..?
Hata Kama hakuna korona haimaanishi hakuna matatizo mengine mbona yapo mengi tu! Na wengine wanaona Bora kufa kuliko kuliko kuishi!!

Acheni upuuzi huyo MUNGU hana la kufanya juu ya matatizo yetu,moja Kati ya kosa ni kumtegemea Mungu akutatulie matatizo wakati vitabu vyake vimeandikwa Mungu ndo muumba wa kila kitu means na matatizo kayaleta yeye tupambaneni wenyewe hakuna kitakacho kutetea usife isipokuwa sisi wenyewe na kufa ni lazima isipokuwa ni muda tu
Asee kweli Waafrika wengi asa wabongo washakuwa addicted na kumtaja Mungu ata Kwa kitu ambacho hausiki nacho

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Subiri na wewe tarehe nane kitafahamika kwa utabiri wako utaukimbia uzi wako ule

Tatizo sio kuamini Sasa kuamini ndo kusema Mungu anakulinda wewe huku wengine wakiumia hiyo ni akili..? Ukiona mwezako ananyolewa za kwako tia maji!!
Mtoeni Mungu kwenye hili hana la kuwasaidia isipokuwa sisi wenyewe..
Huwezi kusema huku ati hakuna ubaya upo na matatizo yapo sijaona anapolinda mbona!! Ni upuuzi kuamini Mungu anatulinda halafu unaitaka serikali ichukue hatua! Si wamuachie Mungu alinde! Kaeni mkijua binadamu atapambana kwa mikono yake mwenyewe hakuna Cha uungu wala nini na huo ndio uhalisia labda uwe na upeo mdogo ndio hautaona! Hakuna Cha nguvu ya Mungu wala nini tuacheni porojo maisha ni halisi.
Nakubali unaongea fact sana jinamizi la kutia mambo uungu inatumaliza sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nchi buana yan we bhacha buana sampuli hadi zikwende kwa wanaume wa Dar ndio tupewe mrejesho alafu buana Y hawakuzuia kuingiza wageni lakn yan sisi ambao hatujawah panda ndege tunaumia zaidi maana ni kama ni ngojwa la kitaliii buana....inatuumiza sana sahv tutakaa kwenye kantini na msosi je?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bill Gates katabiri vifo milion kumi kama virus vya huu ugonjwa vikifanikiwa kupenya Africa.. Manake hatufanyi juhudi zozote zaidi ya matamko yasiyo na tija2.. Na mengi yakiwa ni ya kisiasa zaidi

Jr

Bandiko nyingi humu, hata iliyoanzisha mjadala huu, ni kulaumu tu. Hata Mshana Jr, nguli ya JF, naye anashadidia lawama hizo.

Tutambue kuwa kinga thabiti ya maradhi, yoyote yale, ni ya mtu binafsi, kaya na jamii kwa ujumla. Isitoshe, wakati Serikali kwa ufinyu wa "resources", ikikabiliwa na majanga mengi, hasa wakati huu wa masika ambapo miundo mbinu ya barabara inaharibika, kutaka kuwepo na vituo vya kukagua na kuhudumia walioambikizwa kila sehemu, ni kukosa uelewa.

Hivyo basi, kusisitiza kila mwananchi kuchukua tahadhari, ni jambo la msingi katika kuthibiti kuenea kwa ugonjwa nchini.

Forewarned is forearmed
 
Barua kutoka Italia
___________________

Amani kwa wote,

Tunaishi Italia - Milan,
Nitashiriki nawe na kukuelezea
"Vipi maisha hapa Milan" wakati wa siku hizi ngumu, nadhani unapaswa kujifunza kutokana na makosa na matokeo ambayo tunaishi hapa.

Hivi sasa tumetengwa. Hatuwezi kwenda barabarani, polisi wanasimama kila wakati na kumkamata mtu yeyote nje ya nyumba yake.

Kila kitu kimefungwa! ... biashara, maduka makubwa, maduka madogo, mitaa yote bila mtu yoyote kutembea.

Tunahisi ndiyo mwisho wa ulimwengu !!

Italia, nchi nzuri ya kuishi, inabadilishwa kutoka wakati mmoja hadi mwingine kana kwamba ni nchi iliyo kwenye giza la vita.

Ni ukweli kwamba sikuwahi kufikiria kwamba ningeweza kuishi!

Watu wamechanganyikiwa, huzuni, wasiwasi na hawana msaada, na mara nyingi hawaelewi jinsi ukweli huu ulivyowekwa kwao na wakati gani hali hii ya usiku itamalizika.

Kosa kubwa ni kwamba mwanzoni mwa watu wa kwanza kupata ugonjwa, watu waliendelea kuishi maisha yao kama kawaida na waliingia mitaani kwa kazi, burudani na kuhisi ni kama kipindi cha likizo, kwa hivyo mikusanyiko na marafiki na karamu ziliongezeka.

Kila mtu alikosea na ndivyo pia ulivyokuwa!

Ninakuomba, kuwa mwangalifu, hii sio kichekesho wala utani.

Kinga wapendwa wako, wazazi wako, na wazee wako! Ugonjwa huo ni hatari kwao.

Karibu watu 200 hufa hapa kila siku, sio kwa sababu dawa huko Milan sio nzuri (ni moja wapo bora ulimwenguni), lakini ni kwa sababu hakuna mahali kwa kila mtu!

Madaktari huchagua nani atakufa! Hii ni kwa sababu ya utelezi wa wananchi hapo mwanzoni, ambao waliamua kuendelea na maisha yao kama kawaida, bila kujali hali mpya!

Tafadhali, jifunze kutoka kwa makosa, sisi ni nchi ndogo ambayo inaweza kuishia na janga kubwa.

Sikiliza vizuri sasa ,,,
Usitoke kwenda kwenye sehemu zenye watu.

Usijaribu kula mahali pa umma. Kaa muda mrefu nyumbani wakati huu!
Sikiliza miongozo ya Wizara ya Afya (usichezee!).

Ongea umbali wa mita kutoka kwa kila mtu, usikaribie karibu, usichanganye au ukubali.

Pata matibabu ya ziada na ya kuzuia na ujifunze kutoka kwa makosa ya wengine.

Tunapendekeza kuchukua vitamini C kuongeza mfumo wako wa kinga.( Tumia matunda jamii ya machungwa, na limao katika chakula chako )

Kusaidia wataalamu kuzuia kuenea kwa janga ...

Huko Italia, nchi nzima imetengwa, ikimaanisha watu milioni 60 wametengwa!

Hii ingezuiwa ikiwa watu wangesikia maagizo tangu mwanzo.

Jitunze na maisha ya yule umpendaye
___________________________________
Ujumbe huu unafaa kushiriki ikiwa unajali wengine

Jr
 
Back
Top Bottom