Updates za Corona Tanzania

Updates za Corona Tanzania

COVID-19 na SAIKOLOJIA

Dr. Albanie Marcossy, PhD.

Mshauri mmoja wa mambo ya saikolokjia na jamii aliyefuatilia mlipuko wa Corona unaosababishwa na Virusi vya. Covid-19 ameshauri ifuatavyo:

1. Jitenge mwenyewe usipate taarifa mbaya za ugonjwa huu kila mara (kwa kuwa mambo mengi unayohitaji kujua juu ya Corona umeshayajua, yaliyobaki ni marudio tu)

2. Usitafute habari za vifo. Huu sio mchezo wa mpira kwamba unataka kujua matokeo: mumeshinda ngapi au mmefungwa.

3. Usitafute habari za nyongeza kwenye mitandao. Zitanyong’onyeza hali yako ya afya ya akili. Kujua namna ugonjwa unavyoathiri kunakuongezea Msongo wa mawazo na woga.

4. Epuka kutuma ujumbe wenye taarifa mbaya ya corona. Wengine wana udhaifu mkubwa kwenye uwezo wao kuhimili habari mbaya (baadala ya kuwasaidia unaweza kuwasababishia madhara ikiwemo msongo wa mawazo).

5. Ikiwezekana kaa nyumbani na usikilize muziki kwa sauti laini katika hali tulivu. Tafuta michezo ya kuburidisha watoto na familia. Simulia hadithi, angalia sinema au hata vipindi vya ucheshi. Usiache kuzungumzia mipango yako ya baadae na ya kifamilia.

6. Tunza nidhamu nyumbani kwako haswa ya utaratibu wa usafi kuepuka maambukizi. Nawa mikono kwa sabuni mara kwa mara na uwafuatilie wote nyumbani wafanye hivyo.

7. Kuwa na mtazamo chanya kunaimarisha hali ya kinga ya mwili huku mtazamo hasi unaweza kuthangia msongo wa mawazo na kuharibu kinga ya mwili wako. Pia mtazamo wako chanya utawajengea matumaini unaoishi nao nyumbani kwako.

*La muhimu zaidi ni kuamini kuwa hata hili litapita!* *Na kwamba wewe na jamii yako mtakuwa salama*

*#StayPositive*
*#StaySafe* _Nawatakia usiku mwema._

Jr
 
Shida hatujui mipaka ya mungu inaishia wapi !!
Tumezoea utani na kila kitu kumuachia “Mungu” hatakama ni jukumu letu kutatua jambo utasikia ‘Mungu atuepushe’
Ukiona BBC wanavoonyesha hatua za hizo nchi zingine zinavuchukua unaweza kusema pengine sisi tuko sayari nyingine ndio maana tume relax.

Washington juzi kuna mtu alikua Diagnose na hiyo kitu walifunga Metro, Shule zilizokua Karibu na barabara ya yeye alipopita pamoja na kufanya Fumigation ya mahali pote alipokanyaga.

Kwetu sisi ni maigizo kwenye Daladala kugusana lazima bado pantoni, Kariakoo misongamano daily. Kingine ni mtu akiwa na dalili au akiwa ametoka kwenye hizi nchi zenye haya milipuko inapaswa akae Quarantines kwa siku 21 kujua kama anao au la, pale JNIA wanapima temperature tu ikiwa normal unasepa kama unao dalili utaenda kuzipata nyumbani kwako.
 
.
IMG-20200416-WA0012.jpeg


Jr
 
Shida hatujui mipaka ya mungu inaishia wapi !!
Mungu mipaka, hajawahi kuwA na mipaka haitokujaitokee akawa na mipaka!!

Pili...... Watanzania hatukosi sababu hata kama tutapewa means za kujilinda na kujikinga dhidi ya huu ugonjwa lakini tutacreate vijisababu visivyo na maana. Sasa kwa mfano hii Covid19 unaizuiaje kwa maombi?

Hii kitu sio spiritually ni physically...tutapona kiroho, labda vipi kuhusu kimwili?

Tusitafute sababu. Tufuate njia zote za kujikinga kama inavyoshauriwa na WHO na nchi zote ambazo zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kulidhibiti hili janga.

Mwili na roho ni vitu viwili tofauti katika mwili mmoja na ndo maana tukifariki, mwili una baki roho inakwenda zake.

Tujihadhari, Covid19 inaua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom