Updates za Corona Tanzania

Updates za Corona Tanzania

Screenshot_20200317-153344.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sahihi mkuu... Nafikiri hata kwenye madaladala serikali ingetoa tamko kwamba wapakie abiria level siti tu wazuie msongamano kama ilivozoeleka. Kwa mana ugonjwa huu ukiingia kwenye mji kama dsm tutaondoka kinyama..

kingine serikali ingetoa elimu juu ya aina ya mask ambazo zinatumika mana leo kwa macho yangu nimemuona trafiki amevaa maski lakin inaonekana kua ni ya kuzuia Vumbi na sio kwa ajili ya Cov19... Watu wamekua wakinunua mask bila kujua kama ni maalum kwa ajiri ya corona ama vumbi. Serikali itoe elimu juu ya hili maana kila mask leo hii imepanda bei
 
Coronavirus mpya inaweza kutoonyesha dalili za kuambukizwa kwa siku nyingi, mtu anawezaje kujua kama ameambukizwa. Mpaka wakati una homa na / au kukohoa na kwenda hospitalini, athari katika mapafu imefikia 50% na inakuwa umechelewa sana! Wataalam wa Taiwan wametoa ukaguzi rahisi wa kibinafsi ambao tunaweza kufanya kila asubuhi: Vuta pumzi kubwa na uizuie pumzi yako kwa sekunde zaidi ya 10. Ikiwa utaimaliza bila kukohoa, bila usumbufu au kubanwa nk inathibitisha kuwa hakuna athari kwenye mapafu, kimsingi inaonyesha kuwa hakuna maambukizi. Katika nyakati ngumu, tafadhali jikague kila asubuhi katika mazingira yenye hewa safi! Mapendekezo zaidi kutoka kwa madaktari wa Kijapani kuzuia kesi za COVID-19. Kila mtu anapaswa kuhakikisha kuwa anakunywa maji kidogo kila baada ya dakika 15 angalau. KWA NINI? Hata kama virusi vinaingia kinywani mwako ... kunywa maji au vinywaji vingine vitawashusha tumboni. Mara tu huko tumboni ACID iliyoko tumboni mwako itaua virusi vyote. Ikiwa hautakunywa maji ya kutosha mara kwa mara ... virusi vinaweza kuingia kwenye njia ya hewa na kuelejea mapafuni. Hiyo ni hatari sana. Pls tuma kwa familia na marafiki na kila mtu kuhusu hili!

Jr
 
Natambua umahiri wetu wa kuvifanya vitu serious kuwa mizaha. Natambua ujuzi wetu wa kuyageuza majanga kuwa manufaa ya kisiasa.

Hivi ni kipi kikubwa tumekifanya kama taifa cha serious kujikinga na hili gonjwa linalotaka kuwa janga la dunia?

Nimemsikia Waziri wa Afya akikutangazia umuhimu wa kutoshikana mikono wala kukumbatiana wakati wa kusalimiana kama ilivyo jadi yetu. Wanasiasa wakalibeba hili mzobe mzobe. Mengine yote sidhani kama yamepewa kipaumbele.

Waziri katangaza kila mkoa utenge maeneo maalum ya kuchunguza wenye dalili na viashiria vya huu ugonjwa.

Je, hili limetekelezwa?
Je, kuna vifaa ya kutosha kwenye hili?
Je, bajeti imetoka wapi?
Je, kuna wahudumu wa dharura wenye uelewa na huu ugonjwa wameandaliwa?
Je, sahihi ni kutenga vituo kila mkoa ama kila wilaya?
Je, mpaka sasa ni mikoa mingapi imelitekeleza hili?
Je, kuna changamoto yoyote?
Je, kuna kipindi maalum kwenye vyombo vya habari kutoa mapya ya kila siku kuhusiana na huu ugonjwa?

Hakika maswali ni mengi sana. Lakini nilichokiona kwenye huu ugonjwa ni mizaha na kukosa umakini. Hatuna takwimu rasmi zozote mpaka sasa za chochote kuhusiana na huu ugonjwa. Hatujaona umakini wowote kwenye maandalizi ya dharura. Chukulia mfano mkoa wa Pwani kutoka Mkuranga mpaka Bagamoyo utenge kituo kimoja tu cha ukaguzi wa corona, inawezekana kweli!?

Kinachopigiwa chepuo sasa ni kusalimiana bila kushikana mikono, eti kugongesha miguu. Mmh! Tumeiona kwa viongozi, lakini nyie msioshikana mikono sasa si mlikaa chumba kimoja kwa madakika mengi tu? Je, mlitumia viziba midomo na pua?

Hivi kwani corona ni ugonjwa wa ngozi? Iweje wachezaji uwanjani wazuiwe kusalimiana kwa kushikana mikono eti ni mojawapo ya kampeni ya kupambana na corona wakati huo huo wachezaji haohao watakuwa pamoja uwanjani kwa dakika 90+ wakishikana, wakivutana, wakiangukiana wakipumuliana? Vipi na wale mashabiki watazamani kwa maelfu walio majukwaani? Tuna abiria kwa maelfu wanasongana kwenye vyombo vya usafiri. Kwenye masoko. Kila mahali.

Bado hatuko serious na mizaha ndio imetawala kupitia siasa. Mungu pekee ndio anatubeba. Kitengo cha dharura kitaifa hakijasema chochote. Kipo kimya kabisa. Vyombo vyetu vya habari ni siasa na wanasiasa mwanzo mwisho. Viziba pua na midomo vimepanda bei maradufu. Box lilikokuwa linauzwa elfu 10 piece 50 sasa hivi linauzwa elfu 40 na hapo ugonjwa haujachanganya. Ukithibitika upo nchini na tukatakiwa kutumia hivyo vifaa tutafanyaje?

Jr
Genius mshana ....strike the iron while it hot ...give them lesson

Usiogope sema waziri, CCM imesema hatuwezi tukaziacha hela za watalii eti kuna Corona, ni kwa mujibu wa Polepole. Wachina ni rafiki zetu hatuwezi kuwazuia kuna nchini.
 
Wagonjwa wa akili ni wengi kuliko tunavyodhani

Back
Top Bottom