Updates za Corona Tanzania

Kwa wale wa moshi kuweni makini popote pale mlipo jioni hii mida ya saa 12 ambulance mbili toka kia zimeleta wageni toka kia wanasadikika wagonjwa wa corona maaana wamepelekwa lile jengo ambalo halijakamilika I mean jengo kubwa hivyo basi ....mtaarifu ndugu jamaa na rafiki popote pale alipo kama ana mgonjwa mawenzi aende kwa tahadhari ....every one kuwa makini kupigwa busu.. Kukumbatiana...na kunongonezana haswaa sisi wabongo ...corona ni hatari
Your browser is not able to display this video.


Jr[emoji769]
 
Jana nilifanya tu kuulizia Bei ya mask pharmacy za Sinza, niliambiwa mask moja elfu 2, zile za surgical(ambazo kiuhalisia hazisaidii), Nikashikwa na butwaa.. hand sanitizer niliambiwa kichupa kidogo elfu Saba (hakizidi ml 100). Yaani ni hatari..Watanzania kila kitu kwao Ni fursa.
 
Kinachonisikitisha zaidi ni pale wanaposisitiza watu kutokushikana mikono lakini wanaongea na ku badilishana hewa na ugonjwa unaambukizwa sana kwa njia ya hewa.


Bagwell
Hawashikani mikono lakini wanaenda mazungumzo chumba kimoja chenye A.C.
 
Bill Gates katabiri vifo milion kumi kama virus vya huu ugonjwa vikifanikiwa kupenya Africa.. Manake hatufanyi juhudi zozote zaidi ya matamko yasiyo na tija2.. Na mengi yakiwa ni ya kisiasa zaidi

Jr[emoji769]

Mkuu huyo katumia software ipi ili nami niwe Sheikh Yahaya?
 
To me hata Africa ikawa wiped out completely sawa tu! Tuna faida gani?
Kama una faida n wewe alone mkuu,ila mim najivunia kuwa mwafrika na Nina faida mbele za Mungu.Elimu ya wazungu imeathiri ubongo wako Hadi hujitambui who you are
 
Tuliopo Mikoa ya kaskazini nawakumbusha tu nyuzijoto ni 21-23°C halafu virusi havikai kwenye nyuzijoto 30.
Muda wa kukimbilia Dar huu
 
Ni last week tu nimejiskia hizo hali i swear huwezi hata kula,unakohoa,huku kamasi,mara mgongo unauma,pumzi inabana,kichwa inauma kooni hapo balaa.
Nikachuna siku 4 job.
Kuanzia jana niko fiti kabisa
 
Tuliopo Mikoa ya kaskazini nawakumbusha tu nyuzijoto ni 21-23°C halafu virusi havikai kwenye nyuzijoto 30.
Muda wa kukimbilia Dar huu
Usidanganywe.
Australia na Iran mbona kina joto na mdudu yupo?
Wewe zingatia maelekezo ya wizara ya afya
 
kwa wale waliotumia kiasi kikuba cha
Chloroquine wapo safe zaidi
 
ANZA KUIFIKIRIA KORONA
-kisha fikiria Daladala za mbagala
-Kisha fikiria mwendokasi
-kisha fikiria mabasi ya mikoani
-kisha fikiria msikitini siku za ijumaa
-kisha fikiria kanisani siku za jumamos na jumapil
-kisha fikiria kwenye masoko yetu
-kisha fikiria kwenye vibanda umiza
-kisha fikiria kwenye mashule yetu ya serikali
- kisha fikiria tamaduni zetu watanzania
-kisha fikiria umakini wa wasimamizi wetu

Mdomo wangu unajizuia lakini Nausikia Moyo wangu ukiniambia R. I. P

-fikiria umakini wa marekani lakini umeshindwa kuzuia korona
-fikiria teknolojia ya China lakin imeshindwa kuzuia Korona
-Fikiria nguvu ya Italy lakin nao wameshindwa kuzuia Korona

KILA MTU KWA IMANI YAKE AMUOMBE MUNGU ANAYEMUAMINI ILI NCHI YETU HII ISIGUSWE NA GONJWA HILI

Amen.

Jr[emoji769]
 
Mshana Jr,
Zaidi fikiria siku serikali itakapotamka watu kubaki majumbani ili kudhibiti kasi ya maambukizo. Wengi wanaoishi hand to mouth(asilia mia kubwa ya watanzania) watapata shida kubwa kweli kweli.
 
Zaidi fikiria siku serikali itakapotamka watu kubaki majumbani ili kudhibiti kasi ya maambukizo. Wengi wanaoishi hand to mouth(asilia mia kubwa ya watanzania) watapata shida kubwa kweli kweli.
Tuombe Mungu hili lisitokee.. Watz hatuna utamaduni wa kuhifadhi chakula ndani ama kuwa na hakiba ya dharura

Jr[emoji769]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…