Updates: VodaCom Premier League 2009/2010

Updates: VodaCom Premier League 2009/2010

TIMU GANI ITAKUWA BINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA(Vodacom Premier League)


  • Total voters
    72
  • Poll closed .
Ratiba ya ligikuu ya VODACOM imetolewa ligi itaanza tarehe 24/08/2013

Young Africans vs Ashanti United- Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam

Rhino Ranger Vs Simba - Ali Hassan Mwinyi Tabora

Mtibwa vs Azam - Manungu Morogoro

chanzo Shaffih Dauda in Sports.
 
"Viwanja 10 vitakavyotumika Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu mpya - 2013/14 kuanzia leo Jumamosi Agosti 24, 2013"
=

=
Ligi Kuu msimu wa 2013/14 itaanza leo Agosti 24 na itashirikisha timu 14.
Timu hizo ni mabingwa watetezi

- Yanga,
- Simba,
- Azam FC,
- Ashanti United,
- Tanzania Prisons,
- Rhino Rangers,
- Kagera Sugar,
- Mtibwa Sugar,
- JKT Ruvu,
- Ruvu Shooting,
- Mgambo Shooting,
- Mbeya City,
- JKT Oljoro na
- Coastal Union.
Vifuatavyo ni viwanja 10 vitakavyotumika kwa ajili ya mechi mbalimbali za Ligi Kuu msimu huu:
01. Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Sifa za uwanja huu:
Uwanja huu ulianza kutumika mwaka 2007. Uwanja huu una vipimo vya mita 105 kwa meta 68 na una milango 35 kwa ajili ya watazamaji kuingia na kutoka uwanjani. Una uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 50,000.
Klabu zitakazoutumia uwanja huu kama uwanja wake wa nyumbani ni:

- Simba SC na Yanga SC.
02. Uwanja wa Ali Hassani Mwinyi, Tabora.
Sifa za Uwanja huu:
Ulijengwa mwaka 1987 chini ya usimamizi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Lawrence Gama.
Una uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000 na una milango minane kwa ajili ya kuingia na kutoka uwanjani.
Uwanja huu unamilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Klabu itakayoutumia uwanja huu kama uwanja wake wa nyumbani ni:

-Rhino Rangers.
03. Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Uwanja huu ulijengwa mwaka1957 na unamilikiwa na Chamacha Mapinduzi (CCM).
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid una uwezo wa kuingiza watazamaji 25,000 kwa wakatimmoja.
Klabu ya JKT Oljoro inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),itautumia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kama uwanja wake wa nyumbani.
04.Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Sifa za uwanja huu:
Unapatikana katikati ya jiji la Mbeya na ulijengwa mwaka 1977. Uwanja wa Sokoine una uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000 na unamilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Klabu za Tanzania Prisons na Mbeya City zitautumia uwanja huu kama uwanja wao wa nyumbani.
05. Azam Complex- Chamazi, Dares Salaam.

Sifa uwanja huu:
Ujenzi wake ulianza mwaka 2010 chini ya mkandarasi Kampuni ya Salehe Msahala Contractors Limited.
Uwanja wa Azam Complex una vipimo vya mita 110 kwa mita 71, pia una milango minne na una uwezo wa kuingiza watazamaji 7, 000 kwa mara moja.
Klabu zitakazoutumia uwanja huu kama uwanja wake wa nyumbani ni:

- Ashanti United,
- Azam FC na
- Ruvu Shooting.

Mmiliki wa uwanja huu ni klabu ya Azam FC.
6. Uwanja wa Mabatini, Pwani.
Uwanja wa Mabatini

unapatikana katika mji wa Mlandizi uliopo Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani. Ni uwanja unaomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya Ruvu.
Klabu ya Ruvu Shooting itautumia uwanja huu kwa ajili ya mechi zake za nyumbani isipokuwa zile itakazocheza dhidi ya Simba SC na Yanga SC.
07. Uwanja wa Kaitaba-Bukoba, Kagera.
Sifa za uwanja huu:
Una vipimo vya ukubwa wa mita 110 kwa mita 50. Ulijengwa mwaka 1957 na unamilikiwa na Manispaa ya mji wa Bukoba. Uwanja wa Kaitaba
Una milango minne na una uwezo wa kubeba watazamaji5, 000 kwa wakati mmoja.
Klabu ya Kagera Sugar ndiyo itakayoutumia uwanja huu kama uwanja wake wa nyumbani.

08. Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Sifa za uwanja huu:
Ulijengwa mwaka 1975 na Kampuni ya Amboni Plantation. Uwanja wa Mkwakwani una vipimo vya ukubwa wa mita 105 kwa mita 68, pia una milango saba na uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000.
Mmiliki wa uwanja huu ni Chama cha Mapinduzi (CCM).
Klabu za Coastal Union na Mgambo Shooting zitautumia uwanja huu kama uwanja waowa nyumbani.
09. Uwanja wa Manungu, Morogoro.
Sifa za uwanja huu:
Ulijengwa mwaka 1988 ukiwa na vipimo vya ukubwa wa mita 100 kwa75. Uwanja wa Manungu una milango minne na uwezo wa kubeba watazamaji 8,000.
Mmiliki wa uwanja huu ni Kampuni ya Mtibwa Sugar. Klabu ya Mtibwa itautumia uwanja huu kama uwanja wa nyumbani, lakini itakapokabiriana na Simba SC au Yanga SC itatumia uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ulijengwa mwaka 1978 na unamilikiwa na CCM na una uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000.
LIGI KUU VODACOM 2013/2014:-RATIBA YA MECHI ZA UFUNGUZI:
Jumamosi Agosti 24,2013.
YANGA v ASHANTI UNITED
UWANJA WA TAIFA
DSM
=

MTIBWA SUGAR v AZAM FC
MANUNGU
MOROGORO
=


JKT OLJORO v COASTAL UNION
SH. AMRI ABEID
ARUSHA
=

MGAMBO JKT v JKT RUVU
MKWAKWANI
TANGA
=

RHINO RANGERS v SIMBA
A.H. MWINYI
TABORA
=

MBEYA CITY v KAGERA SUGAR
SOKOINE
MBEYA
=

RUVU SHOOTINGS v PRISONS
MABATINI
PWANI
=

...Karibu wote "WanaJF" tupeane [LIVE! & UPDATES] matukio yanayo ijili kutoka sehemu mbalambali ya mpira wa miguu katika taifa la Tanzania.

Asanteni.
 
Thanks bro, nimependa details kuhusu viwanja kwa kuwa hazipatikani popote kwingine. Senkyu vere mach kbm...
 
Last edited by a moderator:
RATIBA YA MECHI ZA LEO LIGI KUU TANZANIA BARA

Mtibwa Sugar vs Kagera sugar
Rhino Rangers vs Azam Fc
JKT Ruvu vs Prisons
Mbeya City vs Ruvu Shooting
Mgambo vs Ashanti United
JKT Oljoro vs Simba SC
Yanga vs Coastal Union
...... Mechi zote zinataraji kuanza saa 10 na nusu
 
"Wengi wanasubiri kuona nini mabingwa watetezi, Klabu ya Yanga watafanya dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa"

YANGA KUJIULIZA MBELE YA RUVU SHOOTING KESHO, NGASSA DIMBANI, SIMBA YAKAZA, HAITAKI KULIPWA MILIONI 45 ZAKE KWA MAFUNGU KAMA ILIVYOKUWA KWA TWITE, NAO RHINO, MBEYA CITY, MGAMBO KIBARUANI!!
 
MIKIKIMIKIKI ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 inatarajiwa kuendelea kushika kasi wikiendi hii (Jumamosi na jumapili), huku macho ya mashabiki wengi wa soka wakisubiri kuona nini mabingwa watetezi, Klabu ya Yanga watafanya dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-2 wiki iliyopita kutoka kwa Azam Fc.
Yanga wanatarajiwa kushuka dimbani hapo kesho (septemba 28) katika dimba lao la nyumbani dhidi ya vijana wa Charles Boiface Mkwasa `Master`, huku wakiwa na pointi 6 tu katika nafasi ya 8 ya msimamo.
Wanajangwani wataingia uwanjani wakiwa na machungu ya kufanya vibaya mechi za nyuma na tayari mwenyekiti wa klabu hiyo, Yufus Manji amewataka wachezaji kutulia na kuwasisitiza kuwa hana tatizo nao kutoakana na matokeo mabaya.

1222.jpg

Katika mechi ya kesho, winga machachari wa klabu hiyo aliyekuwa akitumikia adhabu ya kifungo cha mechi sita za mashindano kwa kosa la kusaini Mikataba na timu mbili, Simba na Yanga SC , Mrisho Halfan Ngassa `Anko` anatarajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza baada ya uongozi wa klabu hiyo kukubali kulipa deni la milioni 45 kwa watani zao wa jadi Simba Sc.

DSC_0153.jpg

Ngassa alisaini mikataba na timu mbili, Simba na Yanga na kufungiwa mechi 6 na faini ya milioni 45
Yanga imekubali kulipa deni hilo na sasa Ngassa ataendelea kuitumikia klabu yake na kuachana na mpango wake wa kwenda Oman ambako kuna klabu moja ambayo haikutajwa jina ilikuwa inamhitaji kwa dau la milioni 100.
Lakini mpaka sasa haijulikani nyota huyo atailipaje Yanga fedha hizo, kwani awali ilielezwa namna mbili, kwanza kukatwa mshahara wake na pili kuongeza mkataba mwingine mbali na aliosaini.
Sakata la Ngassa lilianzia Agosti mwaka jana alipoupandisha hasira uongozi wa iliyokuwa klabu yake, Azam FC kwa kwenda kubusu jezi ya Yanga SC baada ya kufunga bao la ushindi katika Nusu Fainali ya Kombe la Kagame dhidi ya AS Vita ya DRC, Uwanja wa Taifa.
 
51e4Ismail-Aden-Rage.jpg

Mwenyekiti wa Simba Sc, Aden Rage hataki fedha za mafungu mafungu kutoka kwa Ngassa
Wakati huo huo, Uongozi wa Simba Sc kupitia kwa mwenyekiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage umetoa msimamo wake kuwa Ngassa anatakiwa kulipa fedha zote na hawako tayari kupokea kwa mafungu mafungu kama walivyofanya wakati wa sakata la Mbuyu Twite.
Rage ametoa tahadhari hiyo huku akisema wao wanapenda nyota huyo acheze soka, lakini wanataka mzigo wote na si nusu nusu, vinginevyo hawatakubali.
Lakini amesisitiza kuwa Ngassa hajaomba kulipa kwa mafungu, ila wamelazimika kutoa msimamo huo kwani fedha ya mafungu mafungu huwa zinatibua bajeti yao kama ilivyotokea kwa mzigo waliolipwa na Yanga wakati wa sakata la beki Mbuyu Twite aliyekula fedha za Simba na kisha kusaini Yanga.
 
DSC000681.jpg

Kikosi cha Mbeya City

Mbali na mechi hiyo, kipute kingine cha kuvutia kitakuwepo katika dimba la Sokoine hapa jijini Mbeya ambapo wakali wanaotikisa na kugonga akili za wapenzi wengi wa soka nchini, klabu ya Mbeya City itakuwa kibaruani kumenyana na Wagosi wa Kaya, Coastal Union ya Tanga.
City waliopo nafasi ya 7 wakijikusanyia pointi 7 watashuka dimbani mbele ya Wagosi wa Kaya wenye pointi 9 katika nafasi ya 5 ili kusaka ushindi wa pili uwanja wa nyumbani.
Ikumbukwe kuwa hiyo itakuwa mechi ya nne kwa Mbeya City kucheza nyumbani, ambapo alianza mechi ya ufunguzi na Kagera Sugar, ikacheza na Ruvu Shooting na hatimaye na Yanga kabla ya kwenda Manungu kucheza na Mtibwa Sugar na kuingia Dar es salaam kukipiga na Simba.
Kati ya mechi hizo za nyumbani ilishinda moja tu dhidi ya Ruvu shooting kwa mabao 2-1 na nyingine iliambulia suluhu na sare.
Huko uwanja wa A.H. Mwinyi, Maafande wa jeshi la wananchi (JWTZ), Rhino Rangers watakuwa wenyeji wa `Wanankulukumbi`, Kagera Sugar.
Mechi nyingine itawakutanisha Mgambo JKT katika dimba la Mkwakwani dhidi ya Maafande wa jeshi la kujenga Taifa, JKT Oljoro kutoka mjini Arusha.
Mitanange ya Ligi hiyo itaendelea jumapili kwa mechi tatu kupigwa katika viwanja Tofauti.
Vinara wa ligi hiyo wenye pointi 11, wekundu wa Msimbazi Simba watakuwa ugenini katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam kukabiliana na maafande wa JKT Ruvu FC waliopo nafasi ya pili wakiwa na pointi 9 kibindoni.
 
mwombeki1.jpg

Nao vibonde Ashanti United watakuwa kibaruani kupepetana na Mtibwa Sugar uwanja wa Azam Complex.
Maafande wa Tanzania Prisons `Wajelajela` watakuwa mzigoni kusaka pointi tatu muhimu mbele ya wana Lambalamba, Azam C katika uwanja wa Soine jijini Mbeya.
 
WACHAMBUZI WANASEMAJE KUHUSU YANGA:

...Defence ya Yanga msimu huu 2013/2014 imekuwa hairidhishi (mbovu).

Wadau wengine wanasema mbele (forward) inapotea mara kwa mara (inakuwa butu).

Wadau wengine watoa maoni kuwa labda kurejea kwa Hamisi Kiiza kutawasaidia, na Labda na huyu mdaiwa wa 45milioni, inaweza kuleta angalau.

Yanga imeishacheza mechi 5,
Imefungwa goli 7,

Na mara nyingi kila mechi Yanga wanaruhu magoli,

Magoli mengi yamefungwa kipindi cha pili.
 
Ndugu zangu wana JF, Tupia updates za game unayoifuatilia ktk ligi kuu bara, game za leo jumamosi, hapa uwanja wa Ally hassan mwinyi TABORA, game kati ya Kikosi cha faru weusi RYHNO RANGERS vs KAGERA SUGAR ndo mtanange unaelekea kuanza hapa.
 
Leo mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania bara unaanza, ambapo mabingwa watetezi wanaanza kwa kukipiga na Ashanti kwenye dimba la taifa. Wale wadau wa VPL tuwepo kwa updates. watu8, Masuke, Fidel80, ndetichia na wengine wote wanaohusika.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom