Ni maumivu tu...tutatimua kochaAhsante kwa updates za haraka (mara baada ya mchezo) za msimamo wa ligi. Ila hesabu za hapo nilipoweka bold and underline bado sijayaelewa. Ni makosa ya kutoa (kutafuta the difference) au kumbukumbu za magoli ya kufunga na kufungwa hayako sawa au ni bado maumivu ya matokeo ya jioni ya leo? Niko mbali na nyumbani hivyo sina takwimu sahihi (ndiyo maana nauliza).
Unamjua Victor Costa Nyumba ndiyo dawa ya minyoo aina ya Asamoah...natumaini hutokimbia kwenye jukwaa la Yanga VS Simba na baadae hapa
Leo zamu yenu kupayuka.....huyo jamaa sio tu kibanda bali ni kiduku kabisa tena cha majani 'full suit'
What a weekend........Hahaaaaaaaaaaa
Hongereni zana wana Yanga wenzangu kwa ushindi huu mtamu....Poleni sana watani
PrN-kazi asante kwa kuwa mwaminifu kwakufuata kauli mbiu ya fifa 'my game is fair play maana wengine wametokomea. utahitaji kinywaji gani kama hutajali agiza na mishikaki tani yako
Thanx for updates I appreciate!
Nipo mkuu.....mkuu upo..
Nipo mkuu.....
Nasikitika kwamba tangu ijumaa niki safarini na sikuwa na access ya internet wala TV na nimeingia mjini jioni hii so sijafuatilia derby ya Dsm ya Yanga na Simba wala ile ya derby ya London ya Chelsea na Arsenal.....
Nimefurahi kuona timu zangu zote leo zimeshinda katika derby zao so weekend yangu inaenda barabara kabisa.....
Nampa tu pole mtani wangu Crashwise kwa kipigo hiki ambacho kinauma sana kwa kweli maana mtani wangu alianza majigambo mapema sana(nimeikuta PM yake leo) kiasi cha kusahau kwamba mpira ni dakika 90.......
Chonde chonde watani msimtimue Basena.......Ni kocha mzuri sana huyu mkimtimua mtajuta hapo baadae,kufungwa na Yanga wala sio mwisho wa ligi,mchukulie tu kama vile mmefungwa na Mtibwa ama Azam ama Police Dodoma...
Yanga: Daima mbele, Nyuma mwiko....
Bala.