Wana Yanga ikitokea Manji akafa au akakataa kabisa kudhamini timu inamaana Yanga haitaendelea? Inaumiza sana kuona Manji anapokelewa kwa shangwe kisa kakubali kudhamini tena Yanga.Yanga ni timu kongwe na ifike muda itafute mbinu za kujiendesha kuliko kumtegemea mtu mmoja.
Font na rangi vinaumiza macho kweli mkuu....
Manji kaikuta Yanga na ataiacha....Ni sawa na Simba ilivyokuwa chini ya ufadhili/udhamini wa MO.....Ama Man City na
Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan...........Ama Man Utd na akina Glazer.....
Mwaka jana Manji alijiondoa lakini Yanga ilichukua ubingwa.......Yanga haitegemei mtu mmoja mkuu,kuna TBL.....hawa wanalipia mishahara kwa wachezaji wote wa Simba na Yanga pamoja na vikorombwezo vingine ikiwa ni pamoja na mabasi(usafiri),vifaa n.k...
Yanga ni zaidi ya Manji sawa ilivyo kwa Simba kuwa zaidi ya Malinzi(Dioniz) ,MO,friends of Simba etc....
Cha msingi ni timu za Simba na Yanga kuanza kuiendesha kibiashara/kikampuni zaidi badala ya kutegemea ufadhili wa watua aina ya Manji,Malinzi,MO,friends of Simba,Yanga family n.k.....Timu hizi zinapaswa kuwa kampuni ili zitafute wadhamini(kama ilivyo kwa Emirates,bwin,Ettihad n.k wanavyodhamini timu za ulaya na kwingineko kulikoendelea kisoka),iwe kama TBL wanavyofanya sasa...