Lissu aendelea kumuhoji shahidi
Shahidi anapewa hati ya kiapo
Lissu: Ni yenyewe si ndio?
Shahdi anakagua
Lissu: Kesi ya uhaini sio rahisi haijawahi kuwa rahisi, ni kiapo chako kweli si kweli
Shahidi: Ni kweli
Lissu: Kuna mahali popote umesema shahidi alitishiwa kupigwa Shahidi: Ipo
Lissu: Isome tafadhali.
Shahidi: Naona hii hapa “body harm”
Lissu: Body harm inaweza kuwa na namna nyingi, je, kwenye kiapo chako kuna mtu alipigwa aliambiwa tutakuua tutachoma nyumba tutashambulia familia yako?
Shahidi: hiyo haipo
Lissu: Sasa shahidi kuhusiana na hii habari ya mashahidi kutishiwa, waliletwa mashahidi niliwauliza swali je ulitishiwa kupigwa, ndugu zako au kudhuriwa wote walisema hapana sasa wewe unadai walitishiwa Je mahakama ifuate ushahidi wa nani?
Shahidi: Wakwangu
Lissu: Shahdi angalia hicho kielelezo chako mwanzo kabisa... Makazi Goba njia Nne kata ya Matosa waeleze majaji kama kweli si kweli Goba iko halmashauri ya manispaa ya Ubungo.
Shahidi: Sijui
Lissu: Hujui, Goba iko manisapaa ya Ubungo?..nataka nimsomee shahidi aelewe maeneo.
Anamsomea maneo yote ya ubungo.
Lissu: Waeleze majaji wewe umeandika kata gani
Shahidi: Kata ya matosa.
Lissu: Shahidi twende kwenye kielezo D15 waeleze majaji nani ameandika hayo maelezo.
Shahidi: Nimeandika mwenyewe.
Lissu: Hayo ni maelezo waeleze majaji kama shahidi ana uwezo wa kujiandikia maelezo yake mwenyewe kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai.
Shahidi: Shahidi yeyote maelezo yake yanachukuliwa na afisa wa polisi.
Lissu: Kwenye hayo maelezo aliyekupa onyo kama shahidi ni nani?
Shahidi: Nimetoa tamko
Lissu: Hilo tamko umelitoa mbele ya nani mbele ya afisa gani wa polisi?
Shahidi anajieleza
Lissu: Wewe si umesema ni polisi mimi mwanasheria
Lissu: Hilo tamko umetoa mbele ya nani?
Shahidi: Nimeandika mwenyewe
Lissu: Kuna sehemu ya saini ya mtoa maelezo hapo amesaini nani?
Shahidi: Mwenyewe
Lissu: Na hapo chini sehemu ya afisa aliyeandika maelezo
Shahidi: Nimesaini mwenyewe.
Lissu: Kwenye maelezo yako D15 umesema majukumu yako ni kulinda raia na mali zao.
Shahidi: Ndio
Lissu: Na ulisema uko kwenye kitengo x
Shahidi: Ndio
Lissu: Waleze majaji kama kazi za kitengo X ni pamoja na kulinda raia na mali zao
Shahidi: Ndio
Lissu: Unafahamu PGO
Shahidi: Ndio
Lissu: Waheshimiwa majaji naomba shahidi apewe nakala yangu ya PGO sidhani kama wanayo.
Shahidi anapokea..
Lissu: Waeleze majaji kama hayo yaliyotajwa ni sehemu ya majukumu ya kitengo X kwenye kulinda raia na mali zao. Nimekuwekea alama order 6/8
Shahidi: Swali ni nini?
Lissu: Je, kitengo X kina wajibu wa kulinda raia na mali zao?
Shahidi: Ni sehemu ya majukumu yetu.
Lissu: Soma yote yako manne
Shahidi anasoma
Lissu: Waeleze majaji kama polisi kuna kitengo Y
Shahidi: Ndio kipo.
Lissu: Waeleze majaji kazi zake ni nini
Shahidi: Vyote vinalinda raia na mali zao kama jukumu letu polisi.
Lissu: Waeleze majaji kama umewahi kuwa RCO Singida.
ShahIdi: Sijawahi kufanya kazi Singida.
Lissu: Hujawahi, waeleze majaji katika Jeshi la Polisi kipindi ambacho umekuwa RCO maafisa wa polisi wanaoitwa Amini Mahamba ni wangapi kati ya mwaka 2006 hadi mwaka 2009, mtu anayeitwa Super intendent of Police, Amini Mahamba
Shahidi:Alikuwepo afisa kama huyo lakini alikua anaitwa Amini said Mahamba
Lissu: Waheshimiwa majaji hii ni muhimu iko kwenye kesi ya mahakama ya rufani mwaka 2007 anaidanganya mahakama chini ya kiapo
Lissu anamsomea hukumu ya kesi anayoitumia kama rejea.
Shahidi anakataa sio yeye anasema Amini huyo anayetajwa ni mtu mwingine.
Lissu: Tuendelee.. unasema kama kazi ya kitengo X ni kushughulikia usalama wa nchi, waeleze majaji kama ulimshirikisha Regional Security Officer
Shahidi: Hapana
Lissu: Waeleze majaji kama uliwashirikisha TIS.
Shahidi: Sikuwashirikisha
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu kitu kinaitwa Kamati ya Ulinzi na Usalama na. kama uliijulisha kamati hiyo ya mkoa wa Dar es salaam....
ITAENDELEA....
REPOST