Uozo wa CHADEMA Hadharani

O


Mkuu mathius, kashongo na wenzake ndo aina ya viongozi wanaoiongoza Tz. Huo ndo ukomo wa vikra zao, hawafikirii kuboresha huduma za jamii, wanafikiri kuchafua chama pinzani kwa hoja dhaifu kama hizi pamoja na kuwagawa wanTz kwa hoja za udini na ukabila.
Inauma sana.

Ufisadi wa viongozi wa Chadema ukianikwa unasema huko ni kuchafua upinzani?

Ukweli lazima usemwe siku zote.

Chadema wanachelewa kujivua gamba...na kodi yetu mrudishe haraka.
 
wangeandika CCM wizi basi wote mgelisifia hilo gazeti. Slaa ajitokeze na kukanusha hizo shutuma.
 
TRA hawezi kumjua kila anayekwepa kulipa kodi.
Ni jukumu letu Watz kuwaumbua watu hawa kama alivyofanya Nape.
Sasa TRA wamejjua na watachukua hatua.
Wakwepa kodi, mafisadi, wezi wa mali za umma, wahujumu uchumi, etc etc washtakiwe na wapelekwe mahakamani kujibu mashtaka. Hii ni kuanzia mafisadi wa EPA, Richmond, Kagoda, Meremeta, IPTL, etc etc....
 
Hili linatakiwa likuhuzunishe hata wewe.
Wanaokwepa kulipa kodi ni maadui wakubwa wa nchi.
Washughulikiwe ili liwe fundisho.

Chama cha mayenu,hii ndio song yenu mpya mmezindua?malizieni ya magamba kwanza ndio muanze na hii mpya.
 
Jamani huyu ni Nape yule yule mropokaji tuliyemzoea, ni yule yule anayekaa meza kuu UVCCM na kutoa matamko yaliyokuwa na maana dhidi ya chama chake..ni yule yule aliyekuwa mstari wa mbele kuanzisha CCJ. Leo amekuja na hii ya CDM na kodi. Ni jambo ambalo si rahisi kuamini kwamba chama kinaaingiza nchini vyombo kwa ajili ya uchaguzi kwa gharama ya mil.288 bila TRA kujua. Kinachoshangaza zaidi hata huko Holili TRA wapo. Suala la TRA kukosa risiti hiyo ni juu yao kuweka kumbukumbu na si CDM. Sheria ya gharama za uchaguzi ziko wazi iweje zisifuatwe kama ni kweli. PCCB wako wapi muda wote huo wasifanye uchunguzi..? Hoja nyingine zinatia karaha sana kutokufanyiwa uchunguzi kabla ya kusemwa hadharani. Ndo mambo ya magazeti ya ushenzj haya
 
hongera kaka nape kwa kumwumbua mnafiki daktari wa wakatoliki slaa.

ccm imepata msemaji wa chama mwenye data. uwiiiiiiiiiiiiiiiii watu watakimbia tra kulipa
 
jumla ya hasara ya ufisadi mnaosema chadema wameufanya katika hiyo mipasho ya nape haijafika hata milioni 500, haya atuambie ccm imeshaleta hasara kiasi gani toka ilivyoanza kutawala hadi leo, meremeta, tangold, kagoda, iptl, kiwira, richmond, dowans, madini, ndege, rada, misamaha ya kodi, epa, endeleeni kutaja....
 
^500 milion kwa muda wa miezi tena chama bado hakina uwezo, je wakipewa ufunguo wa benki kuu? Si itakua balaa
 
wangeandika CCM wizi basi wote mgelisifia hilo gazeti. Slaa ajitokeze na kukanusha hizo shutuma.
Akanushe mara ya ngapi? Slaa haongei na mtu kama Nape. Kama mngekuwa wakweli mngeweka na evidence za hayo mnayosema mfanno salary slip au bank statements. Sasa CCM inaelekea kuwa chama cha upinznai kwanini TRA wasichukue hatua mapema?
 
* Wakwepa kodi ya mamilioni ya fedha TRA



* Ni ya kuingiza vifaa vya uchaguzi, mishahara



* Mbowe, Ndesamburo kukifilisi kwa madeni



* Slaa abainika kujilipa posho ya nyumba mara mbili



* Nape amkaba koo, asema ajibu hoja sio uzushi


SIRI zaidi za ufisadi unaofanywa na viongozi wa juu wa CHADEMA zimezidi kufichuka baada ya kufanikiwa kupatikana kwa waraka mzito unaohusiana na tuhuma hizo. Miongoni mwa vitendo hivyo ni CHADEMA kukwepa kulipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kuamua kupitisha kwa kutumia njia za panya, vifaa vya uenezi vya chama hicho ambavyo ni kofia, fulana na bendera zilizoingizwa nchini kutoka China. Vifaa hivyo vilinunuliwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kupitishiwa eneo la Holili, mkoani Kilimanjaro, baada ya kupata sh. milioni 100 kutoka kwa mfanyabiashara Mustapha Sabodo. Hata hivyo, ununuzi wa vifaa hivyo unadaiwa kughubikwa na ufisadi kutokana na uamuzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kudai kuwa aliongeza sh. milioni 188 ili kununua vifaa hivyo na kufanya kiasi cha fedha kilichotumika kuwa sh. milioni 288.


Utata kuhusiana na ununuzi huo unaothibitishwa na habari za kuaminika kutoka ndani ya CHADEMA, unaanza kujitokeza pale Mbowe aliposema anakidai chama hicho sh. milioni 188 ambazo aliongeza ili kununua vifaa, lakini ameshindwa kuonyesha risiti aliyotumia kulipa wakati wa kuviingiza nchini ili kuthibitisha madai yake.



Vifaa hivyo havina risiti halali ya kulipia mapato na hata leo hii mtu akienda TRA kudai risiti ya vifaa hivyo hawezi kuipata kwa kuwa viongozi wetu walivileta na kuviingiza nchini kupitia njia za panya...hawa viongozi wetu kwa hilo wamecheza mchezo mchafu," kilisema chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya chama hicho. Kiliongeza kuwa: Hata sh. milioni 188 anazosema Mbowe anazidai kwenye chama, hazionyeshi zimetoka wapi, kwenye fungu gani au kwenye akaunti gani, lakini amekuwa akisisitiza kuwa aliziongeza akiwa China ili kununua mzigo huo." Ilielezwa kuwa kitendo cha kukwepa kodi ni jambo la kawaida kwa viongozi wa CHADEMA, kwani hata mishahara yao haikatwi kodi.


MZALENDO limebaini kuwa fedha zinazodaiwa na Mbowe ni sehemu ya mikakati yake na Katibu Mkuu, Dk.Wilbroad Slaa ambaye ndiye mtendaji mkuu wa chama hicho kutaka kujinufaisha kwa kutumia chama kama taasisi binafsi. Wiki hii, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwalipua viongozi wa CHADEMA baada kubainisha jinsi wanavyojipatia mishahara minono huku kwenye mikutano ya hadhara wakiwahadaa wananchi kuwa wanapambana na vitendo vya ufisadi. Ilifichuliwa kuwa mshahara wa Dk. Slaa ni zaidi ya sh. milioni saba ambazo ni nyingi kuliko za wabunge alizowahi kuzipigia kelele akidai kuwa ni kufuru.


Siku moja baada ya kulipuliwa na Nape, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa CHADEMA, Anthony Komu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando waliitisha mkutano na waandishi wa habari kukanusha taarifa hizo, jambo ambalo baadhi ya viongozi wa chama hicho wamefichua kuwa ufafanuzi uliotolewa wao ni wa uongo. Komu kudai Dk. Slaa analipwa mshahara wa sh. 1,725,000 na lita 1,000 za mafuta kila mwezi ni uongo wenye lengo la kutaka kuficha jinsi baadhi ya viongozi waandamizi walivyounda mtandao wa kutumba fedha za CHADEMA, chanzo hicho kilisema. MZALENDO limefanikiwa kupata waraka ambao unaonyesha kuwa mapendekezo ya posho ya Dk. Slaa kama Azimio la Kamati Kuu iliyokaa Januari 29 hadi 30, mwaka huu, Dar es Salaam ni tofauti na maelezo waliyotoa Komu na Marando. Kwa mujibu wa waraka huo, posho ya Dk. Slaa imegawanywa katika sehemu sita ambazo ni posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi. Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi. Mshahara wa Slaa haukatwi kodi. Kwa upande wa posho, Slaa analipwa fedha za mafuta sh. 1,387,500 kwa lita 750 kwa mwezi huku fedha za majukumu zikiwa ni sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. 1,000,000. Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa ni maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo.


Dk. Slaa akiungwa mkono na Mbowe anadaiwa kujipatia posho ya nyumba mara mbili, kwani ilishapendekezwa alipwe sh. milioni 40 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Licha ya kupewa fedha hizo, Dk. Slaa ameendelea kupewa posho nyingine ya nyumba ya sh. 1,000,000 kila mwezi.
Analipwa fedha za nyumba wakati Mbowe alishakitaka chama kimpe sh, milioni 40 kumalizia nyumba yake iliyopo Mbweni ambayo sasa anaishi,kilidai chanzo chetu.


Katika hatua nyingine, baadhi ya viongozi wa CHADEMA Makao Makuu wamelalamika kitendo cha ufujaji fedha kinachofanywa na vigogo wa chama katika maandamano na mikutano ya hadhara inayofanyika mikoani ambapo wastani wa sh. milioni 100 hutumika katika kila mkoa.
Kila maandamano yanapofanyika mikoani, takriban sh. milioni 100 zinatumika huku madeni yasiyo na msingi yakiongezwa na baadhi ya viongozi na kuongezeka kila baada ya ziara, alisema mmoja wa viongozi hao.


Alidai kuwa Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo ambaye pia ni mdhamini wa chama hicho anadai zaidi sh. milioni 296 kwa ajili helikopta zake zilizotumika kwenye uchaguzi uliopita.
Kutoka mkoani Singida, Bashir Nkoromo anaripoti kuwa, Nape amemtaka Dk. Slaa kwenda haraka TRA kulipa kodi ya mshahara wake wa mamilioni ya fedha ili apunguze doa la ufisadi linalomkabili.


Nape alitoa kauli hiyo, jana, mjini hapa katika mkutano wa hadhara wa kutambulisha Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, akirejea kauli yake aliyoitoa juzi.
Alisisitiza kwamba kwa kufanya hivyo, Slaa atakuwa ametimiza wajibu wake wa kulipa kodi kama Mtanzania, kwani amehujumu nchi kwa kukwepa kodi kwa muda mrefu.


Alidai bado ana tuhuma nyingi za ufisadi dhidi ya Dk. Slaa, lakini anamtaka kwanza kulipa kodi ya mshahara huo.


Alirejea kauli yake kwamba Dk. Slaa kujipatia kwake mshahara huo ni dalili ya wazi kwamba, kilio chake ambacho amekuwa akikitoa katika kupiga vita kuhusu kuwepo pengo kati ya walio nacho na wasio nacho ni unafiki.


"Inafahamika wazi ndani ya CHADEMA hakuna mkurugenzi hata mmoja anayepata mshahara unaozidi sh. 600,000 kwa mwezi achilia mbali wafanyakazi wa kawaida ambao hawapati zaidi ya sh. 300,000, alisema na kuwa wanaopata zaidi ya hapo ni wachache sana.


"Kama kweli Slaa angekuwa anakerwa kwa dhati ndani ya moyo wake na pengo hilo kwa nini asianzie kuchukua hatua kwenye ofisi za chama chake?," alihoji Nape.


Akijibu tuhuma zilizotolewa na viongozi wa CHADEMA, juzi, na kuripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari jana, Nape alisema viongozi wa chama hicho wanaweweseka kwa kuwa hawajazoea kusemwa.


Alisema kauli kwamba Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama anapata mshahara wa sh. milioni 11 ni ishara ya kuweweseka huko kwa sababu madai hayo hayakufanyiwa utafiti, hivyo ni ya uongo.


Nape alisema, licha ya kwamba Katibu Mkuu wa CCM ni kiongozi wa Chama tawala tena chenye vyanzo vingi vya fedha ikiwemo ruzuku kubwa kuliko CHADEMA, mshahara wake ni sh. milioni 1.5 na unakatwa kodi, ambao ni kiasi kidogo ukilinganishwa na ule wa Slaa ambao analipwa na chama ambacho ruzuku yake ni ndogo sana.


Pia Nape alimshangaa msemaji wa CHADEMA kumtuhumu kwamba anapokea mishahara miwili na ni miongoni mwa walionufaika na uchotwaji wa fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) na kwamba aliomba kugombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho.


Akijibu shutuma hizo, Nape alisema, huko ni kuishiwa hoja kwa viongozi wa CHADEMA kwa sababu, wakati uchotwaji wa fedha za EPA ukifanywa na mafisadi, alikuwa masomoni nchini India, 2005 na 2008.


"Je wanataka kusema kwamba fedha hizo zilinifuata huko?," Nape alihoji.
Kuhusu mishahara miwili, alisema hakuna ukweli kwani tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo, hajaanza kupata hata mshahara mmoja na kwamba, mara tu alipoteuliwa kushika wadhifa huo aliacha mshahara, nyumba ikiwa na kila kitu hadi vijiko na gari aliyokuwa akitumia akiwa mkuu wa wilaya.

Source: GAZETI LA MZALENDO

Comment
: Shutuma hizi ni nzito kwa mtu anayeheshimika katika jamii kama Dr Slaa.
Ili kutunza heshma yake iliyobaki, na kwa maslahi ya chama chake, ashauriwe ajiuzulu mara moja.

Upupuuuu!!!
 
SASA hizi kashfa wanazozitoa chama cha magamba ndio zitawafanya wafe kabisa. Nasubiri kwa hamu nishuhudie hicho kifo.
 
watachoka tu,wanadhani wakieleza mabaya ya chadema hata kama
ni kweli watanzania ndo wataona kuwa "bora ccm"?

Damn
 
TRA hawezi kumjua kila anayekwepa kulipa kodi.
Ni jukumu letu Watz kuwaumbua watu hawa kama alivyofanya Nape.
Sasa TRA wamejjua na watachukua hatua.

hv huo mshahara mpya wa dk kaanza kulipwa lin? Au anazungumzia mshahara upi?, kod ip anazungumzia?,. CDM ni chama kinachotambulika kisheria hv TRA walikua wap kujua kua mshahara wa ktb mkuu haukatwi kodi?, je ni ktb mkuu pekee halipi kod au kuna wengne?.
 
TRA hawezi kumjua kila anayekwepa kulipa kodi.
Ni jukumu letu Watz kuwaumbua watu hawa kama alivyofanya Nape.
Sasa TRA wamejjua na watachukua hatua.

hv huo mshahara mpya wa dk kaanza kulipwa lin? Au anazungumzia mshahara upi?, kod ip anazungumzia?,. CDM ni chama kinachotambulika kisheria hv TRA walikua wap kujua kua mshahara wa ktb mkuu haukatwi kodi?, je ni ktb mkuu pekee halipi kod au kuna wengne?.
 
This is what we call politics of desperation. CCM wameishiwa, wanabaki kujivua magamba na kusahau kuwa ukianza kumrushia mwenzako tope unabaki nazo mikononi na nguoni mwako.
 
Nakumbuka kuna wakati nilikuwa naenda Nairobi nikawa na gazeti la Mzalendo, Makarao wakaniuliza na wewe ni mukora! Nikauliza WHY wkanambia mbona unajifunika na karatasi kubwa hivyo? MZALENDO gazeti litumiwalo na wakora kujificha maovu yao!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom