Uozo wa CHADEMA Hadharani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uozo wa CHADEMA Hadharani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kishongo, May 15, 2011.

 1. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  * Wakwepa kodi ya mamilioni ya fedha TRA  * Ni ya kuingiza vifaa vya uchaguzi, mishahara  * Mbowe, Ndesamburo kukifilisi kwa madeni  * Slaa abainika kujilipa posho ya nyumba mara mbili  * Nape amkaba koo, asema ajibu hoja sio uzushi


  SIRI zaidi za ufisadi unaofanywa na viongozi wa juu wa CHADEMA zimezidi kufichuka baada ya kufanikiwa kupatikana kwa waraka mzito unaohusiana na tuhuma hizo. Miongoni mwa vitendo hivyo ni CHADEMA kukwepa kulipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kuamua kupitisha kwa kutumia njia za panya, vifaa vya uenezi vya chama hicho ambavyo ni kofia, fulana na bendera zilizoingizwa nchini kutoka China. Vifaa hivyo vilinunuliwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kupitishiwa eneo la Holili, mkoani Kilimanjaro, baada ya kupata sh. milioni 100 kutoka kwa mfanyabiashara Mustapha Sabodo. Hata hivyo, ununuzi wa vifaa hivyo unadaiwa kughubikwa na ufisadi kutokana na uamuzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kudai kuwa aliongeza sh. milioni 188 ili kununua vifaa hivyo na kufanya kiasi cha fedha kilichotumika kuwa sh. milioni 288.


  Utata kuhusiana na ununuzi huo unaothibitishwa na habari za kuaminika kutoka ndani ya CHADEMA, unaanza kujitokeza pale Mbowe aliposema anakidai chama hicho sh. milioni 188 ambazo aliongeza ili kununua vifaa, lakini ameshindwa kuonyesha risiti aliyotumia kulipa wakati wa kuviingiza nchini ili kuthibitisha madai yake.  “Vifaa hivyo havina risiti halali ya kulipia mapato na hata leo hii mtu akienda TRA kudai risiti ya vifaa hivyo hawezi kuipata kwa kuwa viongozi wetu walivileta na kuviingiza nchini kupitia njia za panya...hawa viongozi wetu kwa hilo wamecheza mchezo mchafu," kilisema chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya chama hicho. Kiliongeza kuwa: “Hata sh. milioni 188 anazosema Mbowe anazidai kwenye chama, hazionyeshi zimetoka wapi, kwenye fungu gani au kwenye akaunti gani, lakini amekuwa akisisitiza kuwa aliziongeza akiwa China ili kununua mzigo huo." Ilielezwa kuwa kitendo cha kukwepa kodi ni jambo la kawaida kwa viongozi wa CHADEMA, kwani hata mishahara yao haikatwi kodi.


  MZALENDO limebaini kuwa fedha zinazodaiwa na Mbowe ni sehemu ya mikakati yake na Katibu Mkuu, Dk.Wilbroad Slaa ambaye ndiye mtendaji mkuu wa chama hicho kutaka kujinufaisha kwa kutumia chama kama taasisi binafsi. Wiki hii, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwalipua viongozi wa CHADEMA baada kubainisha jinsi wanavyojipatia mishahara minono huku kwenye mikutano ya hadhara wakiwahadaa wananchi kuwa wanapambana na vitendo vya ufisadi. Ilifichuliwa kuwa mshahara wa Dk. Slaa ni zaidi ya sh. milioni saba ambazo ni nyingi kuliko za wabunge alizowahi kuzipigia kelele akidai kuwa ni ‘kufuru’.


  Siku moja baada ya kulipuliwa na Nape, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa CHADEMA, Anthony Komu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando waliitisha mkutano na waandishi wa habari kukanusha taarifa hizo, jambo ambalo baadhi ya viongozi wa chama hicho wamefichua kuwa ufafanuzi uliotolewa wao ni wa uongo. “Komu kudai Dk. Slaa analipwa mshahara wa sh. 1,725,000 na lita 1,000 za mafuta kila mwezi ni uongo wenye lengo la kutaka kuficha jinsi baadhi ya viongozi waandamizi walivyounda mtandao wa kutumba fedha za CHADEMA,” chanzo hicho kilisema. MZALENDO limefanikiwa kupata waraka ambao unaonyesha kuwa mapendekezo ya posho ya Dk. Slaa kama Azimio la Kamati Kuu iliyokaa Januari 29 hadi 30, mwaka huu, Dar es Salaam ni tofauti na maelezo waliyotoa Komu na Marando. Kwa mujibu wa waraka huo, posho ya Dk. Slaa imegawanywa katika sehemu sita ambazo ni posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi. Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi. Mshahara wa Slaa haukatwi kodi. Kwa upande wa posho, Slaa analipwa fedha za mafuta sh. 1,387,500 kwa lita 750 kwa mwezi huku fedha za majukumu zikiwa ni sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. 1,000,000. Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa ni maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo.


  Dk. Slaa akiungwa mkono na Mbowe anadaiwa kujipatia posho ya nyumba mara mbili, kwani ilishapendekezwa alipwe sh. milioni 40 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Licha ya kupewa fedha hizo, Dk. Slaa ameendelea kupewa posho nyingine ya nyumba ya sh. 1,000,000 kila mwezi.
  “Analipwa fedha za nyumba wakati Mbowe alishakitaka chama kimpe sh, milioni 40 kumalizia nyumba yake iliyopo Mbweni ambayo sasa anaishi,’’kilidai chanzo chetu.


  Katika hatua nyingine, baadhi ya viongozi wa CHADEMA Makao Makuu wamelalamika kitendo cha ufujaji fedha kinachofanywa na vigogo wa chama katika maandamano na mikutano ya hadhara inayofanyika mikoani ambapo wastani wa sh. milioni 100 hutumika katika kila mkoa.
  “Kila maandamano yanapofanyika mikoani, takriban sh. milioni 100 zinatumika huku madeni yasiyo na msingi yakiongezwa na baadhi ya viongozi na kuongezeka kila baada ya ziara,” alisema mmoja wa viongozi hao.


  Alidai kuwa Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo ambaye pia ni mdhamini wa chama hicho anadai zaidi sh. milioni 296 kwa ajili helikopta zake zilizotumika kwenye uchaguzi uliopita.
  Kutoka mkoani Singida, Bashir Nkoromo anaripoti kuwa, Nape amemtaka Dk. Slaa kwenda haraka TRA kulipa kodi ya mshahara wake wa mamilioni ya fedha ili apunguze doa la ufisadi linalomkabili.


  Nape alitoa kauli hiyo, jana, mjini hapa katika mkutano wa hadhara wa kutambulisha Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, akirejea kauli yake aliyoitoa juzi.
  Alisisitiza kwamba kwa kufanya hivyo, Slaa atakuwa ametimiza wajibu wake wa kulipa kodi kama Mtanzania, kwani amehujumu nchi kwa kukwepa kodi kwa muda mrefu.


  Alidai bado ana tuhuma nyingi za ufisadi dhidi ya Dk. Slaa, lakini anamtaka kwanza kulipa kodi ya mshahara huo.


  Alirejea kauli yake kwamba Dk. Slaa kujipatia kwake mshahara huo ni dalili ya wazi kwamba, kilio chake ambacho amekuwa akikitoa katika kupiga vita kuhusu kuwepo pengo kati ya walio nacho na wasio nacho ni unafiki.


  "Inafahamika wazi ndani ya CHADEMA hakuna mkurugenzi hata mmoja anayepata mshahara unaozidi sh. 600,000 kwa mwezi achilia mbali wafanyakazi wa kawaida ambao hawapati zaidi ya sh. 300,000,” alisema na kuwa wanaopata zaidi ya hapo ni wachache sana.


  "Kama kweli Slaa angekuwa anakerwa kwa dhati ndani ya moyo wake na pengo hilo kwa nini asianzie kuchukua hatua kwenye ofisi za chama chake?," alihoji Nape.


  Akijibu tuhuma zilizotolewa na viongozi wa CHADEMA, juzi, na kuripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari jana, Nape alisema viongozi wa chama hicho wanaweweseka kwa kuwa hawajazoea kusemwa.


  Alisema kauli kwamba Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama anapata mshahara wa sh. milioni 11 ni ishara ya kuweweseka huko kwa sababu madai hayo hayakufanyiwa utafiti, hivyo ni ya uongo.


  Nape alisema, licha ya kwamba Katibu Mkuu wa CCM ni kiongozi wa Chama tawala tena chenye vyanzo vingi vya fedha ikiwemo ruzuku kubwa kuliko CHADEMA, mshahara wake ni sh. milioni 1.5 na unakatwa kodi, ambao ni kiasi kidogo ukilinganishwa na ule wa Slaa ambao analipwa na chama ambacho ruzuku yake ni ndogo sana.


  Pia Nape alimshangaa msemaji wa CHADEMA kumtuhumu kwamba anapokea mishahara miwili na ni miongoni mwa walionufaika na uchotwaji wa fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) na kwamba aliomba kugombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho.


  Akijibu shutuma hizo, Nape alisema, huko ni kuishiwa hoja kwa viongozi wa CHADEMA kwa sababu, wakati uchotwaji wa fedha za EPA ukifanywa na mafisadi, alikuwa masomoni nchini India, 2005 na 2008.


  "Je wanataka kusema kwamba fedha hizo zilinifuata huko?," Nape alihoji.
  Kuhusu mishahara miwili, alisema hakuna ukweli kwani tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo, hajaanza kupata hata mshahara mmoja na kwamba, mara tu alipoteuliwa kushika wadhifa huo aliacha mshahara, nyumba ikiwa na kila kitu hadi vijiko na gari aliyokuwa akitumia akiwa mkuu wa wilaya.

  Source: GAZETI LA MZALENDO

  Comment
  : Shutuma hizi ni nzito kwa mtu anayeheshimika katika jamii kama Dr Slaa.
  Ili kutunza heshma yake iliyobaki, na kwa maslahi ya chama chake, ashauriwe ajiuzulu mara moja.
   
 2. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chooni kwangu nina magazeti kibao ya uhuru, mzalendo, tazama. huwa nachambiaga.
   
 3. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Source: GAZETI LA MZALENDO

  Hivi hili gazeti bado lipo jamani?
   
 4. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Alidai badyo ana tuhuma nyingi za ufisadi dhidi ya Dk. Slaa, lakini anamtaka kwanza ku MAMA YANGU ANAFUNGIA SAMBUSA NA BAGIA
   
 5. i411

  i411 JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  kweli siasa mchezo mbaya, huko 2015 nazani mambo yatakuwa super bora tusirudi mambo ya ujamaa
   
 6. Nditu

  Nditu Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi ni kwa nini CCM wanazidi kujiumbua mbele ya kadamnasi namna hii? Hoja dhaifu zisizo na mpangilio, za kihuni na muflisi kama hizi si ndizo zinazowapunguzia sympathizers wengi? Au ndiyo tuseme kuwa kada wa CCM nilazima uwe mropokaji na msema ovyo kama hivi? Nasema hivi mchawi wa CCM ni wao wenyewe, na inasikitisha sana kama hii ndiyo strategy ya Mukama na Nape! Ama kweli sikio lakufa halisikii dawa. Sishangai siku hizi magazeti ya Uhuru na Mzalendo yamegeuka dili kwa matumizi ya kufungia maandazi na vitumbua!
   
 7. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Wapi evidence, naona chai tupu as usual.
   
 8. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #8
  May 15, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  malizieni kwanza kuvua magamba yenu ndo muanze kuwasingizia na wengine!
   
 9. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,973
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Sio kila source inafaa kuwa kama reference baadhi ya source eg. Mzalendo wanatumiwa. Kama TRA wanajua kuwa CHADEMA wanakwepa kulipa kodi na wamekaa kimya, nao pia wana matatizo!!!!!
   
 10. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #10
  May 15, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Ushahidi upo wapi sasa Kama wanao wautoe,Ila hilo gazeti lililoandika hizo habari ni zaidi ya kiroja
   
 11. eliesikia

  eliesikia JF-Expert Member

  #11
  May 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  puuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuh magazeti mengine hata kutunga stori hawawezi achilia mbali kuwa gazeti kama toilet paper.... Haya huwa yanabaki mengi kweli hakuna anaenunua... basi ukienda dukani unapata kakipande fulani hivi basi unachambia tuu
   
 12. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #12
  May 15, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Naona kishongo,kama kawaida yako,na kama lilivyo jina lako
   
 13. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #13
  May 15, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  TRA hawezi kumjua kila anayekwepa kulipa kodi.
  Ni jukumu letu Watz kuwaumbua watu hawa kama alivyofanya Nape.
  Sasa TRA wamejjua na watachukua hatua.
   
 14. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #14
  May 15, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  ha ha ha ha ha huyo muasisi wa CCJ bado anaendelea na siasa zake za kipumbavu?

  mwambieni CDM ni V8 atapasua hiyo engine yake ya Duet!!
   
 15. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #15
  May 15, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hili linatakiwa likuhuzunishe hata wewe.
  Wanaokwepa kulipa kodi ni maadui wakubwa wa nchi.
  Washughulikiwe ili liwe fundisho.
   
 16. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #16
  May 15, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  tunahitaji kusikia hatua zilizochukuliwa dhidi ya magamba
   
 17. e

  englibert Member

  #17
  May 15, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi chadema wakikwepa kodi kesho yake vyombo vyote vya dola mpaka jwtz ingelizunguka jengo la makao makuu ya chadema na ingekuwa breaking news,mpaka mwenyekiti wa ccm taifa ,angelihutubia taifa,maana maandamano tu mwenyekiti alihutubia taifa.
   
 18. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #18
  May 15, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  CCM, acheni kuhangaika na CDM, mmeshaprove failure tayari! Jikiteni kwenye kuleta maisha bora kwa kila mtanzania!
   
 19. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #19
  May 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  wana chadema hawakuhongwa kofia wala tshirt,walijinunulia wenyewe mitaani! MBONA MPAKA LEO CCM HAWAJATAMKA KTK UCHAGUZI WALIFUJA KIASI GANI vs KURA WALIZOPATA na waweke hadharani vyanzo vyake?PIA SISHAURI MTANZANIA YEYOTE ALIPE KODI TRA KWA KUWA WANAOLIPA NI WALALAHOI,WAHINDI HAWALIPI PIA CCM HAMNA UWEZO WA KUTULETEA MAENDELEO KUTOKANA NA KODI ZETU!
   
 20. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #20
  May 15, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,584
  Likes Received: 849
  Trophy Points: 280
  Nukama na Mape ni ma-rapper wa bendi ya ccm tena wazuri kushinda hata Maa-kamba, Captain K, aka mzee wa kusinzia bungeni hebu waazime vyombo hawa jamaa waanzishe CCM JAZZ BAND
   
Loading...