Uozo wa CHADEMA Hadharani

Uozo wa CHADEMA Hadharani

mie hapo ndio nape ananichosha kabisa.Alijifanya kupambana na ufisadi ndani ya chama,akapewa ukuu wa wilaya, kwa nini asikatae kama ni msafi?hata mafisadi na uchafu wao wamesema hawawezi kumnunua kwenye kambi yao,kwa sababu hajui anachokifanya.sasa subiri kabali yake inakuja.Cheap politician.
 
Kishongo wewe ni miongoni mwa wanoimaliza nchi hii watu kama nyinyi mngekua China tungekua tumekusahau kabisa! Jirekebishe.
 
Mnalalamika nini! na nyie ndio wenye dola.
Oh Cdm nao ni mafisadi. nawashangaa kiukweli!
kwani hivyo nyie ccm mmesha kubali kuwa ni mafisadi na mnataja wengine. au!
Hivi mnaionaje Cdm wangekuwa ndio wenye dola mngeishia jela.
Kama mnacho ongea ni kweli washitakini sio kuchonga mitaani.
 
source mzalendo pumbavuu, nape ukitoka singida pitia mirembe ndo stahili yako pale, kichwa yako imepata hitilafu. mzalendo, uhuru hivi haya magazeti bado yapo na kama yapo naomba kujuzwa yanasomwa na watu wa sampuli gani. shame nape, shame kishongo, shame m/kiti and shame ccm. pu
 
blah blah.....ccm have mountain to climb ,is this how u want to justify your ufisadi ? ,we want to hear how do u tackle overwhelming corruption in ur government,how do u improve the life of common people and how u impliment community development project, we want implimentation not blah blah......people are tired
 
Kishongo wewe ni miongoni mwa wanoimaliza nchi hii watu kama nyinyi mngekua China tungekua tumekusahau kabisa! Jirekebishe.

Ubaya wangu ni kuanika jinsi Dr Slaa anavyohujumu uchumi wetu kwa kukwepa kulipa kodi?
Kama ndiyo, niko tayari kwa unayodai yanafanywa kwa watu kama mimi kule China.
 
Source: GAZETI LA MZALENDO yanawahusu nyie mnaosoma magazeti ya magamba vueni kwanza ggamba acheni porojo
 
* Wakwepa kodi ya mamilioni ya fedha TRA

* Ni ya kuingiza vifaa vya uchaguzi, mishahara

* Mbowe, Ndesamburo kukifilisi kwa madeni

* Slaa abainika kujilipa posho ya nyumba mara mbili

* Nape amkaba koo, asema ajibu hoja sio uzushi

SIRI zaidi za ufisadi unaofanywa na viongozi wa juu wa CHADEMA zimezidi kufichuka baada ya kufanikiwa kupatikana kwa waraka mzito unaohusiana na tuhuma hizo. Miongoni mwa vitendo hivyo ni CHADEMA kukwepa kulipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kuamua kupitisha kwa kutumia njia za panya, vifaa vya uenezi vya chama hicho ambavyo ni kofia, fulana na bendera zilizoingizwa nchini kutoka China. Vifaa hivyo vilinunuliwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kupitishiwa eneo la Holili, mkoani Kilimanjaro, baada ya kupata sh. milioni 100 kutoka kwa mfanyabiashara Mustapha Sabodo. Hata hivyo, ununuzi wa vifaa hivyo unadaiwa kughubikwa na ufisadi kutokana na uamuzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kudai kuwa aliongeza sh. milioni 188 ili kununua vifaa hivyo na kufanya kiasi cha fedha kilichotumika kuwa sh. milioni 288.

Utata kuhusiana na ununuzi huo unaothibitishwa na habari za kuaminika kutoka ndani ya CHADEMA, unaanza kujitokeza pale Mbowe aliposema anakidai chama hicho sh. milioni 188 ambazo aliongeza ili kununua vifaa, lakini ameshindwa kuonyesha risiti aliyotumia kulipa wakati wa kuviingiza nchini ili kuthibitisha madai yake.

“Vifaa hivyo havina risiti halali ya kulipia mapato na hata leo hii mtu akienda TRA kudai risiti ya vifaa hivyo hawezi kuipata kwa kuwa viongozi wetu walivileta na kuviingiza nchini kupitia njia za panya...hawa viongozi wetu kwa hilo wamecheza mchezo mchafu," kilisema chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya chama hicho. Kiliongeza kuwa: “Hata sh. milioni 188 anazosema Mbowe anazidai kwenye chama, hazionyeshi zimetoka wapi, kwenye fungu gani au kwenye akaunti gani, lakini amekuwa akisisitiza kuwa aliziongeza akiwa China ili kununua mzigo huo." Ilielezwa kuwa kitendo cha kukwepa kodi ni jambo la kawaida kwa viongozi wa CHADEMA, kwani hata mishahara yao haikatwi kodi.

MZALENDO limebaini kuwa fedha zinazodaiwa na Mbowe ni sehemu ya mikakati yake na Katibu Mkuu, Dk.Wilbroad Slaa ambaye ndiye mtendaji mkuu wa chama hicho kutaka kujinufaisha kwa kutumia chama kama taasisi binafsi. Wiki hii, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwalipua viongozi wa CHADEMA baada kubainisha jinsi wanavyojipatia mishahara minono huku kwenye mikutano ya hadhara wakiwahadaa wananchi kuwa wanapambana na vitendo vya ufisadi. Ilifichuliwa kuwa mshahara wa Dk. Slaa ni zaidi ya sh. milioni saba ambazo ni nyingi kuliko za wabunge alizowahi kuzipigia kelele akidai kuwa ni ‘kufuru’.

Siku moja baada ya kulipuliwa na Nape, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa CHADEMA, Anthony Komu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando waliitisha mkutano na waandishi wa habari kukanusha taarifa hizo, jambo ambalo baadhi ya viongozi wa chama hicho wamefichua kuwa ufafanuzi uliotolewa wao ni wa uongo. “Komu kudai Dk. Slaa analipwa mshahara wa sh. 1,725,000 na lita 1,000 za mafuta kila mwezi ni uongo wenye lengo la kutaka kuficha jinsi baadhi ya viongozi waandamizi walivyounda mtandao wa kutumba fedha za CHADEMA,” chanzo hicho kilisema. MZALENDO limefanikiwa kupata waraka ambao unaonyesha kuwa mapendekezo ya posho ya Dk. Slaa kama Azimio la Kamati Kuu iliyokaa Januari 29 hadi 30, mwaka huu, Dar es Salaam ni tofauti na maelezo waliyotoa Komu na Marando. Kwa mujibu wa waraka huo, posho ya Dk. Slaa imegawanywa katika sehemu sita ambazo ni posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi. Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi. Mshahara wa Slaa haukatwi kodi. Kwa upande wa posho, Slaa analipwa fedha za mafuta sh. 1,387,500 kwa lita 750 kwa mwezi huku fedha za majukumu zikiwa ni sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. 1,000,000. Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa ni maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo.

Dk. Slaa akiungwa mkono na Mbowe anadaiwa kujipatia posho ya nyumba mara mbili, kwani ilishapendekezwa alipwe sh. milioni 40 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Licha ya kupewa fedha hizo, Dk. Slaa ameendelea kupewa posho nyingine ya nyumba ya sh. 1,000,000 kila mwezi.
“Analipwa fedha za nyumba wakati Mbowe alishakitaka chama kimpe sh, milioni 40 kumalizia nyumba yake iliyopo Mbweni ambayo sasa anaishi,’’kilidai chanzo chetu.

Katika hatua nyingine, baadhi ya viongozi wa CHADEMA Makao Makuu wamelalamika kitendo cha ufujaji fedha kinachofanywa na vigogo wa chama katika maandamano na mikutano ya hadhara inayofanyika mikoani ambapo wastani wa sh. milioni 100 hutumika katika kila mkoa.
“Kila maandamano yanapofanyika mikoani, takriban sh. milioni 100 zinatumika huku madeni yasiyo na msingi yakiongezwa na baadhi ya viongozi na kuongezeka kila baada ya ziara,” alisema mmoja wa viongozi hao.

Alidai kuwa Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo ambaye pia ni mdhamini wa chama hicho anadai zaidi sh. milioni 296 kwa ajili helikopta zake zilizotumika kwenye uchaguzi uliopita.
Kutoka mkoani Singida, Bashir Nkoromo anaripoti kuwa, Nape amemtaka Dk. Slaa kwenda haraka TRA kulipa kodi ya mshahara wake wa mamilioni ya fedha ili apunguze doa la ufisadi linalomkabili.

Nape alitoa kauli hiyo, jana, mjini hapa katika mkutano wa hadhara wa kutambulisha Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, akirejea kauli yake aliyoitoa juzi.
Alisisitiza kwamba kwa kufanya hivyo, Slaa atakuwa ametimiza wajibu wake wa kulipa kodi kama Mtanzania, kwani amehujumu nchi kwa kukwepa kodi kwa muda mrefu.

Alidai bado ana tuhuma nyingi za ufisadi dhidi ya Dk. Slaa, lakini anamtaka kwanza kulipa kodi ya mshahara huo.

Alirejea kauli yake kwamba Dk. Slaa kujipatia kwake mshahara huo ni dalili ya wazi kwamba, kilio chake ambacho amekuwa akikitoa katika kupiga vita kuhusu kuwepo pengo kati ya walio nacho na wasio nacho ni unafiki.

"Inafahamika wazi ndani ya CHADEMA hakuna mkurugenzi hata mmoja anayepata mshahara unaozidi sh. 600,000 kwa mwezi achilia mbali wafanyakazi wa kawaida ambao hawapati zaidi ya sh. 300,000,” alisema na kuwa wanaopata zaidi ya hapo ni wachache sana.

"Kama kweli Slaa angekuwa anakerwa kwa dhati ndani ya moyo wake na pengo hilo kwa nini asianzie kuchukua hatua kwenye ofisi za chama chake?," alihoji Nape.

Akijibu tuhuma zilizotolewa na viongozi wa CHADEMA, juzi, na kuripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari jana, Nape alisema viongozi wa chama hicho wanaweweseka kwa kuwa hawajazoea kusemwa.

Alisema kauli kwamba Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama anapata mshahara wa sh. milioni 11 ni ishara ya kuweweseka huko kwa sababu madai hayo hayakufanyiwa utafiti, hivyo ni ya uongo.

Nape alisema, licha ya kwamba Katibu Mkuu wa CCM ni kiongozi wa Chama tawala tena chenye vyanzo vingi vya fedha ikiwemo ruzuku kubwa kuliko CHADEMA, mshahara wake ni sh. milioni 1.5 na unakatwa kodi, ambao ni kiasi kidogo ukilinganishwa na ule wa Slaa ambao analipwa na chama ambacho ruzuku yake ni ndogo sana.

Pia Nape alimshangaa msemaji wa CHADEMA kumtuhumu kwamba anapokea mishahara miwili na ni miongoni mwa walionufaika na uchotwaji wa fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) na kwamba aliomba kugombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho.

Akijibu shutuma hizo, Nape alisema, huko ni kuishiwa hoja kwa viongozi wa CHADEMA kwa sababu, wakati uchotwaji wa fedha za EPA ukifanywa na mafisadi, alikuwa masomoni nchini India, 2005 na 2008.

"Je wanataka kusema kwamba fedha hizo zilinifuata huko?," Nape alihoji.
Kuhusu mishahara miwili, alisema hakuna ukweli kwani tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo, hajaanza kupata hata mshahara mmoja na kwamba, mara tu alipoteuliwa kushika wadhifa huo aliacha mshahara, nyumba ikiwa na kila kitu hadi vijiko na gari aliyokuwa akitumia akiwa mkuu wa wilaya.

Source: GAZETI LA MZALENDO

Comment: Shutuma hizi ni nzito kwa mtu anayeheshimika katika jamii kama Dr Slaa.
Ili kutunza heshma yake iliyobaki, na kwa maslahi ya chama chake, ashauriwe ajiuzulu mara moja.

wewe ni ****** tena wa nyani maana watu wanaongelea ufisadi kwenye serikali wewe habari za uongo nenda kakojolewe
 
Comment
: Shutuma hizi ni nzito kwa mtu anayeheshimika katika jamii kama Dr Slaa.
Ili kutunza heshma yake iliyobaki, na kwa maslahi ya chama chake, ashauriwe ajiuzulu mara moja.

Nina mashaka na hilo gazeti lako la MZALENDO sitashangaaa mhariri mkuu akawa Salva!!
 
Mzalendo nia aina nyingine ya toiletpaper,kishongo ni wakala wa hizo toiletpaper brand new.nyambafu!
 
WanaJF, msisahau kwamba miezi michache iliyopita UVCCM walikuwa wakiandaa mkakati wa kupambana na wapinzani na mbinu yao kubwa ni kutumia magazeti. Sasa ndio wanaanza, lakini, uongo utajitenga na ukweli kwa sababu viwili hivyo huwa havichangamani HATA KIDOGO. No sawa na "maji" na "mafuta." Ni sawa na "nuru" na giza" hivi kamwe havikai pamoja na utamu wake ni kwamba "nuru" iking'aa giza linakimbia na maana yake ni kwamba "nuru" ina nguvu kuliko "giza." UKWELI una nguvu kuliko uongo. Propaganda hizi za kuchafuana bila ukweli ndani yake utawagharimu waongo. Mimi nilidhani Chama Tawala kingechukua hatua ya zaidi ya "kujivua gamba" yaani kuondokana na "sumu" ambayo ni hatari kuliko gamba wanalokazana kujivua! CCM, inabakia kuwa ile ile kama haitaondokana na sumu na kinachidhihirisha kwamba CCM ni ile ile ni huu uzandiki unaoendelezwa na wapiga debe wake. Badala ya kushughulika ili kupata ufumbuzi wa ugumu wa maisha unaowakabili wananchi wanakaa kujadili mambo ambayo ukiyasikiliza kwa makini yanawahusu wao kuliko hao wanaowatuhumu! Sumu mbaya kuliko gamba. Wajivue sumu za ukitimbakwiri (ufisadi), rushwa, tamaa ya mali, ubinafsi na sasa huu UONGO uliokithiri.

Kinachonifurahisha mimi ni kwamba wakiendelea hivi tutajua mengi maana sasa wapiga debe wanaropoka kama watu waliokunywa pombe iliyowekwa kitu wachagga wanachokiita "kimangano" ambacho ukinyweshwa hiyo kama wewe mchawi utaanza kuweweseka na kuwataja watu uliowaua na uliokuwa unapanga kuwaua. Chadema msijibu hoja za kipumbavu ila zile tu zitakazohatarisha usalama wa Chama na nchi yetu tunayoipenda. Peoples' Power is the only and true way to true liberty.
 
mimi siungi mkono ufisadi popote pale being in CCM, CDM, Serikalini au nyumbani kwangu ila pia nakereka na propaganda za kingese!! kuna gazeti (nafikiri ni Mwanahalisi) wakileta ishu kama hizi wanaleta na photocopy za hizo nyaraka!! sasa hawa wanasema wana nyaraka lakini wanakaa nazo, za nini sasa??? ili iwe nini?? pyuuu!!! mshahara wa Slaa na madeni ya CDM yananiathiri nini mimi kapuku/lofa wa huku Lushoto?? najua CDM hawatakuwa na muda wa kujibu hii crap. Habari kama hii isiyo na ushahidi wa nguvu wanajua haina athari zaidi zaidi inawshushia hadhi hili gazeti.
 
Tunashukuru kwa taarifa hii ambayo naamini si rasmi hivi kweli chama cha upinzani kiingize vifaa kwa njia za panya??? Inaingia akilini?, Usalama wa Taifa na dola kwa ujumla walikuwa likizo??? Kama walikamata visu fafe wakajitia ni vya CUF 2005 walishindwaje kukamata vifaa vya CHADEMA???? Jamani acheni hizo andikeni mambo yenye mashikooooo
 
Sio kila source inafaa kuwa kama reference baadhi ya source eg. Mzalendo wanatumiwa. Kama TRA wanajua kuwa CHADEMA wanakwepa kulipa kodi na wamekaa kimya, nao pia wana matatizo!!!!!

Ndugu yangu nakuunga mkono kwani serikali ya ccm iliyopo madarakani ktk kitengo hicho cha TRA walikuwa wapi mpaka leo hii wanajiwashia utambi pasipo kujua utawalipukia wao!
Kweli ccm wote vilaza wanakurubuka kama tumbo la kuumwa.
CHADEMA songeni mbele kwani washindani wenu wanaongozwa na nguvu za giza kwani wanachofikiria ni pumba tu!
 
Mkuu Kishongo
Nafikiri, sio jukumu letu kufuatilia nani analipa kodi na nani alipi, TRA wapo kwa ajili iyo, wanachukua mshahara kuhakikisha kuwa kila mtu anawajibika kwa kulipa kodi, kama wameshindwa hakuna mbadala niwao wawajibike. Tukisema kuhusu tuhuma kwa Dr Slaa, nafikiri aliyetakiwa kuwajibika kwanza kabla ya yeyote ni JK na chama chake, wizi wa EPA, Kagoda, Richmond, Rada, BoT, yote ayo ni dhahiri kuna uozo mkubwa. Anza na hao kwanza ndo urukie kwa watendaji wengine wasio serikalini na kwenye chama tawala. Kwa sababu wizi unaofanyika ndani ya Serikali (mfano BoT ) una athari ya moja kwa moja katika maisha ya mtanzania.

Kuna ishu muhimu za kujadili, kama vile ni namna gani tunaweza kusonga mbele kama taifa kutoka kwenye ili dimbwi la umasikini tulilinonalo na tuungane na wenzetu kwenye karne ya 21. Nchi haina maji wala umeme wa kuaminika, aya ndo mambo ya kujadili, na waliotufikisha hapa bado tunao mtaani. Kama bado una mtizamo wa kutumia bajaji kama ambulance na zimamoto, wakati wenzentu wanaongelea kuweka electrical car milioni moja barabarani mwishoni mwa mwaka 2015 sidhani kama utakuwa unafikiri sawasawa.

Hili linatakiwa likuhuzunishe hata wewe.
Wanaokwepa kulipa kodi ni maadui wakubwa wa nchi.
Washughulikiwe ili liwe fundisho.
 
this is just neologism,i am sad that the country is lead by this bunch of short sighted ******! CHADEMA IS A VIRGIN!
 
O
Mkuu Kishongo
Nafikiri, sio jukumu letu kufuatilia nani analipa kodi na nani alipi, TRA wapo kwa ajili iyo, wanachukua mshahara kuhakikisha kuwa kila mtu anawajibika kwa kulipa kodi, kama wameshindwa hakuna mbadala niwao wawajibike. Tukisema kuhusu tuhuma kwa Dr Slaa, nafikiri aliyetakiwa kuwajibika kwanza kabla ya yeyote ni JK na chama chake, wizi wa EPA, Kagoda, Richmond, Rada, BoT, yote ayo ni dhahiri kuna uozo mkubwa. Anza na hao kwanza ndo urukie kwa watendaji wengine wasio serikalini na kwenye chama tawala. Kwa sababu wizi unaofanyika ndani ya Serikali (mfano BoT ) una athari ya moja kwa moja katika maisha ya mtanzania.

Kuna ishu muhimu za kujadili, kama vile ni namna gani tunaweza kusonga mbele kama taifa kutoka kwenye ili dimbwi la umasikini tulilinonalo na tuungane na wenzetu kwenye karne ya 21. Nchi haina maji wala umeme wa kuaminika, aya ndo mambo ya kujadili, na waliotufikisha hapa bado tunao mtaani. Kama bado una mtizamo wa kutumia bajaji kama ambulance na zimamoto, wakati wenzentu wanaongelea kuweka electrical car milioni moja barabarani mwishoni mwa mwaka 2015 sidhani kama utakuwa unafikiri sawasawa.

Mkuu mathius, kashongo na wenzake ndo aina ya viongozi wanaoiongoza Tz. Huo ndo ukomo wa vikra zao, hawafikirii kuboresha huduma za jamii, wanafikiri kuchafua chama pinzani kwa hoja dhaifu kama hizi pamoja na kuwagawa wanTz kwa hoja za udini na ukabila.
Inauma sana.
 
Back
Top Bottom