Uozo wa CHADEMA Hadharani

Uozo wa CHADEMA Hadharani

* Wakwepa kodi ya mamilioni ya fedha TRA

* Ni ya kuingiza vifaa vya uchaguzi, mishahara

* Mbowe, Ndesamburo kukifilisi kwa madeni

* Slaa abainika kujilipa posho ya nyumba mara mbili

* Nape amkaba koo, asema ajibu hoja sio uzushi

SIRI zaidi za ufisadi unaofanywa na viongozi wa juu wa CHADEMA zimezidi kufichuka baada ya kufanikiwa kupatikana kwa waraka mzito unaohusiana na tuhuma hizo. Miongoni mwa vitendo hivyo ni CHADEMA kukwepa kulipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kuamua kupitisha kwa kutumia njia za panya, vifaa vya uenezi vya chama hicho ambavyo ni kofia, fulana na bendera zilizoingizwa nchini kutoka China. Vifaa hivyo vilinunuliwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kupitishiwa eneo la Holili, mkoani Kilimanjaro, baada ya kupata sh. milioni 100 kutoka kwa mfanyabiashara Mustapha Sabodo. Hata hivyo, ununuzi wa vifaa hivyo unadaiwa kughubikwa na ufisadi kutokana na uamuzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kudai kuwa aliongeza sh. milioni 188 ili kununua vifaa hivyo na kufanya kiasi cha fedha kilichotumika kuwa sh. milioni 288.

Utata kuhusiana na ununuzi huo unaothibitishwa na habari za kuaminika kutoka ndani ya CHADEMA, unaanza kujitokeza pale Mbowe aliposema anakidai chama hicho sh. milioni 188 ambazo aliongeza ili kununua vifaa, lakini ameshindwa kuonyesha risiti aliyotumia kulipa wakati wa kuviingiza nchini ili kuthibitisha madai yake.

“Vifaa hivyo havina risiti halali ya kulipia mapato na hata leo hii mtu akienda TRA kudai risiti ya vifaa hivyo hawezi kuipata kwa kuwa viongozi wetu walivileta na kuviingiza nchini kupitia njia za panya...hawa viongozi wetu kwa hilo wamecheza mchezo mchafu," kilisema chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya chama hicho. Kiliongeza kuwa: “Hata sh. milioni 188 anazosema Mbowe anazidai kwenye chama, hazionyeshi zimetoka wapi, kwenye fungu gani au kwenye akaunti gani, lakini amekuwa akisisitiza kuwa aliziongeza akiwa China ili kununua mzigo huo." Ilielezwa kuwa kitendo cha kukwepa kodi ni jambo la kawaida kwa viongozi wa CHADEMA, kwani hata mishahara yao haikatwi kodi.

MZALENDO limebaini kuwa fedha zinazodaiwa na Mbowe ni sehemu ya mikakati yake na Katibu Mkuu, Dk.Wilbroad Slaa ambaye ndiye mtendaji mkuu wa chama hicho kutaka kujinufaisha kwa kutumia chama kama taasisi binafsi. Wiki hii, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwalipua viongozi wa CHADEMA baada kubainisha jinsi wanavyojipatia mishahara minono huku kwenye mikutano ya hadhara wakiwahadaa wananchi kuwa wanapambana na vitendo vya ufisadi. Ilifichuliwa kuwa mshahara wa Dk. Slaa ni zaidi ya sh. milioni saba ambazo ni nyingi kuliko za wabunge alizowahi kuzipigia kelele akidai kuwa ni ‘kufuru’.

Siku moja baada ya kulipuliwa na Nape, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa CHADEMA, Anthony Komu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando waliitisha mkutano na waandishi wa habari kukanusha taarifa hizo, jambo ambalo baadhi ya viongozi wa chama hicho wamefichua kuwa ufafanuzi uliotolewa wao ni wa uongo. “Komu kudai Dk. Slaa analipwa mshahara wa sh. 1,725,000 na lita 1,000 za mafuta kila mwezi ni uongo wenye lengo la kutaka kuficha jinsi baadhi ya viongozi waandamizi walivyounda mtandao wa kutumba fedha za CHADEMA,” chanzo hicho kilisema. MZALENDO limefanikiwa kupata waraka ambao unaonyesha kuwa mapendekezo ya posho ya Dk. Slaa kama Azimio la Kamati Kuu iliyokaa Januari 29 hadi 30, mwaka huu, Dar es Salaam ni tofauti na maelezo waliyotoa Komu na Marando. Kwa mujibu wa waraka huo, posho ya Dk. Slaa imegawanywa katika sehemu sita ambazo ni posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi. Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi. Mshahara wa Slaa haukatwi kodi. Kwa upande wa posho, Slaa analipwa fedha za mafuta sh. 1,387,500 kwa lita 750 kwa mwezi huku fedha za majukumu zikiwa ni sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. 1,000,000. Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa ni maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo.

Dk. Slaa akiungwa mkono na Mbowe anadaiwa kujipatia posho ya nyumba mara mbili, kwani ilishapendekezwa alipwe sh. milioni 40 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Licha ya kupewa fedha hizo, Dk. Slaa ameendelea kupewa posho nyingine ya nyumba ya sh. 1,000,000 kila mwezi.
“Analipwa fedha za nyumba wakati Mbowe alishakitaka chama kimpe sh, milioni 40 kumalizia nyumba yake iliyopo Mbweni ambayo sasa anaishi,’’kilidai chanzo chetu.

Katika hatua nyingine, baadhi ya viongozi wa CHADEMA Makao Makuu wamelalamika kitendo cha ufujaji fedha kinachofanywa na vigogo wa chama katika maandamano na mikutano ya hadhara inayofanyika mikoani ambapo wastani wa sh. milioni 100 hutumika katika kila mkoa.
“Kila maandamano yanapofanyika mikoani, takriban sh. milioni 100 zinatumika huku madeni yasiyo na msingi yakiongezwa na baadhi ya viongozi na kuongezeka kila baada ya ziara,” alisema mmoja wa viongozi hao.

Alidai kuwa Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo ambaye pia ni mdhamini wa chama hicho anadai zaidi sh. milioni 296 kwa ajili helikopta zake zilizotumika kwenye uchaguzi uliopita.
Kutoka mkoani Singida, Bashir Nkoromo anaripoti kuwa, Nape amemtaka Dk. Slaa kwenda haraka TRA kulipa kodi ya mshahara wake wa mamilioni ya fedha ili apunguze doa la ufisadi linalomkabili.

Nape alitoa kauli hiyo, jana, mjini hapa katika mkutano wa hadhara wa kutambulisha Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, akirejea kauli yake aliyoitoa juzi.
Alisisitiza kwamba kwa kufanya hivyo, Slaa atakuwa ametimiza wajibu wake wa kulipa kodi kama Mtanzania, kwani amehujumu nchi kwa kukwepa kodi kwa muda mrefu.

Alidai bado ana tuhuma nyingi za ufisadi dhidi ya Dk. Slaa, lakini anamtaka kwanza kulipa kodi ya mshahara huo.

Alirejea kauli yake kwamba Dk. Slaa kujipatia kwake mshahara huo ni dalili ya wazi kwamba, kilio chake ambacho amekuwa akikitoa katika kupiga vita kuhusu kuwepo pengo kati ya walio nacho na wasio nacho ni unafiki.

"Inafahamika wazi ndani ya CHADEMA hakuna mkurugenzi hata mmoja anayepata mshahara unaozidi sh. 600,000 kwa mwezi achilia mbali wafanyakazi wa kawaida ambao hawapati zaidi ya sh. 300,000,” alisema na kuwa wanaopata zaidi ya hapo ni wachache sana.

"Kama kweli Slaa angekuwa anakerwa kwa dhati ndani ya moyo wake na pengo hilo kwa nini asianzie kuchukua hatua kwenye ofisi za chama chake?," alihoji Nape.

Akijibu tuhuma zilizotolewa na viongozi wa CHADEMA, juzi, na kuripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari jana, Nape alisema viongozi wa chama hicho wanaweweseka kwa kuwa hawajazoea kusemwa.

Alisema kauli kwamba Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama anapata mshahara wa sh. milioni 11 ni ishara ya kuweweseka huko kwa sababu madai hayo hayakufanyiwa utafiti, hivyo ni ya uongo.

Nape alisema, licha ya kwamba Katibu Mkuu wa CCM ni kiongozi wa Chama tawala tena chenye vyanzo vingi vya fedha ikiwemo ruzuku kubwa kuliko CHADEMA, mshahara wake ni sh. milioni 1.5 na unakatwa kodi, ambao ni kiasi kidogo ukilinganishwa na ule wa Slaa ambao analipwa na chama ambacho ruzuku yake ni ndogo sana.

Pia Nape alimshangaa msemaji wa CHADEMA kumtuhumu kwamba anapokea mishahara miwili na ni miongoni mwa walionufaika na uchotwaji wa fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) na kwamba aliomba kugombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho.

Akijibu shutuma hizo, Nape alisema, huko ni kuishiwa hoja kwa viongozi wa CHADEMA kwa sababu, wakati uchotwaji wa fedha za EPA ukifanywa na mafisadi, alikuwa masomoni nchini India, 2005 na 2008.

"Je wanataka kusema kwamba fedha hizo zilinifuata huko?," Nape alihoji.
Kuhusu mishahara miwili, alisema hakuna ukweli kwani tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo, hajaanza kupata hata mshahara mmoja na kwamba, mara tu alipoteuliwa kushika wadhifa huo aliacha mshahara, nyumba ikiwa na kila kitu hadi vijiko na gari aliyokuwa akitumia akiwa mkuu wa wilaya.

Source: GAZETI LA MZALENDO

Comment
: Shutuma hizi ni nzito kwa mtu anayeheshimika katika jamii kama Dr Slaa.
Ili kutunza heshma yake iliyobaki, na kwa maslahi ya chama chake, ashauriwe ajiuzulu mara moja.

BADO haijanishawishi niache kudai mabilioni ya EPA, RICHMOND, DOWANS, RADAR etc. Ninasema majambazi wa CCM rudisheni pesa za walipa kodi. Sitaki kusoma wala kusikia chochote eti magamba ngozi na uzushi kama huu. Ninataka kodi yangu mliyoniibia BOT ili kuingia madarakani. CHONDE!!!!CHONDE!!!CHONDE!!CHONDE!! TUSIJEONANA WABAYA NITAKAPOWAFUKUZA AJIRA NILIYOWAPA. ACHANA NA CDM NIPENI CHANGU KWANZA.

WATZ huu ni mchezo na wizi unaendelea kwa fujo. UKICHEZA NA KIMA ATAKUACHIA MABUA SHAMBANI!!!!!!!!!!! haya
 
nape acha uongo kwani ww ni msemaji wa tra?, ni kosa jinai kutolipa kodi hata kama walikopa walikuwa na vyanzo gani vya mapato kipind kile, ka nape kameanza kuwa kaongo na kazush sana. Yaani uongo live.
 
Ndugu yangu Mnauye kwa nini unapenda/kukubali kutumiwa kama Condom? Ngoja wamalize kazi yao ndo utajua huwa unatupwa wapi baada ya kutumika....
 
Wananchi wa tunduru wamewatuma wabunge wa chadema,wawakilishe matatizo yao sugu bungeni la barabara na pembejeo za kilimo.wanasema wanajuta kuifahamu ccm!baada ya uchaguzi hawajamuona tena mbunge wao!
 
* Wakwepa kodi ya mamilioni ya fedha TRA

* Ni ya kuingiza vifaa vya uchaguzi, mishahara

* Mbowe, Ndesamburo kukifilisi kwa madeni

* Slaa abainika kujilipa posho ya nyumba mara mbili

* Nape amkaba koo, asema ajibu hoja sio uzushi

SIRI zaidi za ufisadi unaofanywa na viongozi wa juu wa CHADEMA zimezidi kufichuka baada ya kufanikiwa kupatikana kwa waraka mzito unaohusiana na tuhuma hizo. Miongoni mwa vitendo hivyo ni CHADEMA kukwepa kulipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kuamua kupitisha kwa kutumia njia za panya, vifaa vya uenezi vya chama hicho ambavyo ni kofia, fulana na bendera zilizoingizwa nchini kutoka China. Vifaa hivyo vilinunuliwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kupitishiwa eneo la Holili, mkoani Kilimanjaro, baada ya kupata sh. milioni 100 kutoka kwa mfanyabiashara Mustapha Sabodo. Hata hivyo, ununuzi wa vifaa hivyo unadaiwa kughubikwa na ufisadi kutokana na uamuzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kudai kuwa aliongeza sh. milioni 188 ili kununua vifaa hivyo na kufanya kiasi cha fedha kilichotumika kuwa sh. milioni 288.

Utata kuhusiana na ununuzi huo unaothibitishwa na habari za kuaminika kutoka ndani ya CHADEMA, unaanza kujitokeza pale Mbowe aliposema anakidai chama hicho sh. milioni 188 ambazo aliongeza ili kununua vifaa, lakini ameshindwa kuonyesha risiti aliyotumia kulipa wakati wa kuviingiza nchini ili kuthibitisha madai yake.

"Vifaa hivyo havina risiti halali ya kulipia mapato na hata leo hii mtu akienda TRA kudai risiti ya vifaa hivyo hawezi kuipata kwa kuwa viongozi wetu walivileta na kuviingiza nchini kupitia njia za panya...hawa viongozi wetu kwa hilo wamecheza mchezo mchafu," kilisema chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya chama hicho. Kiliongeza kuwa: "Hata sh. milioni 188 anazosema Mbowe anazidai kwenye chama, hazionyeshi zimetoka wapi, kwenye fungu gani au kwenye akaunti gani, lakini amekuwa akisisitiza kuwa aliziongeza akiwa China ili kununua mzigo huo." Ilielezwa kuwa kitendo cha kukwepa kodi ni jambo la kawaida kwa viongozi wa CHADEMA, kwani hata mishahara yao haikatwi kodi.

MZALENDO limebaini kuwa fedha zinazodaiwa na Mbowe ni sehemu ya mikakati yake na Katibu Mkuu, Dk.Wilbroad Slaa ambaye ndiye mtendaji mkuu wa chama hicho kutaka kujinufaisha kwa kutumia chama kama taasisi binafsi. Wiki hii, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwalipua viongozi wa CHADEMA baada kubainisha jinsi wanavyojipatia mishahara minono huku kwenye mikutano ya hadhara wakiwahadaa wananchi kuwa wanapambana na vitendo vya ufisadi. Ilifichuliwa kuwa mshahara wa Dk. Slaa ni zaidi ya sh. milioni saba ambazo ni nyingi kuliko za wabunge alizowahi kuzipigia kelele akidai kuwa ni ‘kufuru'.

Siku moja baada ya kulipuliwa na Nape, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa CHADEMA, Anthony Komu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando waliitisha mkutano na waandishi wa habari kukanusha taarifa hizo, jambo ambalo baadhi ya viongozi wa chama hicho wamefichua kuwa ufafanuzi uliotolewa wao ni wa uongo. "Komu kudai Dk. Slaa analipwa mshahara wa sh. 1,725,000 na lita 1,000 za mafuta kila mwezi ni uongo wenye lengo la kutaka kuficha jinsi baadhi ya viongozi waandamizi walivyounda mtandao wa kutumba fedha za CHADEMA," chanzo hicho kilisema. MZALENDO limefanikiwa kupata waraka ambao unaonyesha kuwa mapendekezo ya posho ya Dk. Slaa kama Azimio la Kamati Kuu iliyokaa Januari 29 hadi 30, mwaka huu, Dar es Salaam ni tofauti na maelezo waliyotoa Komu na Marando. Kwa mujibu wa waraka huo, posho ya Dk. Slaa imegawanywa katika sehemu sita ambazo ni posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi. Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi. Mshahara wa Slaa haukatwi kodi. Kwa upande wa posho, Slaa analipwa fedha za mafuta sh. 1,387,500 kwa lita 750 kwa mwezi huku fedha za majukumu zikiwa ni sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. 1,000,000. Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa ni maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo.

Dk. Slaa akiungwa mkono na Mbowe anadaiwa kujipatia posho ya nyumba mara mbili, kwani ilishapendekezwa alipwe sh. milioni 40 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Licha ya kupewa fedha hizo, Dk. Slaa ameendelea kupewa posho nyingine ya nyumba ya sh. 1,000,000 kila mwezi.
"Analipwa fedha za nyumba wakati Mbowe alishakitaka chama kimpe sh, milioni 40 kumalizia nyumba yake iliyopo Mbweni ambayo sasa anaishi,''kilidai chanzo chetu.

Katika hatua nyingine, baadhi ya viongozi wa CHADEMA Makao Makuu wamelalamika kitendo cha ufujaji fedha kinachofanywa na vigogo wa chama katika maandamano na mikutano ya hadhara inayofanyika mikoani ambapo wastani wa sh. milioni 100 hutumika katika kila mkoa.
"Kila maandamano yanapofanyika mikoani, takriban sh. milioni 100 zinatumika huku madeni yasiyo na msingi yakiongezwa na baadhi ya viongozi na kuongezeka kila baada ya ziara," alisema mmoja wa viongozi hao.

Alidai kuwa Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo ambaye pia ni mdhamini wa chama hicho anadai zaidi sh. milioni 296 kwa ajili helikopta zake zilizotumika kwenye uchaguzi uliopita.
Kutoka mkoani Singida, Bashir Nkoromo anaripoti kuwa, Nape amemtaka Dk. Slaa kwenda haraka TRA kulipa kodi ya mshahara wake wa mamilioni ya fedha ili apunguze doa la ufisadi linalomkabili.

Nape alitoa kauli hiyo, jana, mjini hapa katika mkutano wa hadhara wa kutambulisha Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, akirejea kauli yake aliyoitoa juzi.
Alisisitiza kwamba kwa kufanya hivyo, Slaa atakuwa ametimiza wajibu wake wa kulipa kodi kama Mtanzania, kwani amehujumu nchi kwa kukwepa kodi kwa muda mrefu.

Alidai bado ana tuhuma nyingi za ufisadi dhidi ya Dk. Slaa, lakini anamtaka kwanza kulipa kodi ya mshahara huo.

Alirejea kauli yake kwamba Dk. Slaa kujipatia kwake mshahara huo ni dalili ya wazi kwamba, kilio chake ambacho amekuwa akikitoa katika kupiga vita kuhusu kuwepo pengo kati ya walio nacho na wasio nacho ni unafiki.

"Inafahamika wazi ndani ya CHADEMA hakuna mkurugenzi hata mmoja anayepata mshahara unaozidi sh. 600,000 kwa mwezi achilia mbali wafanyakazi wa kawaida ambao hawapati zaidi ya sh. 300,000," alisema na kuwa wanaopata zaidi ya hapo ni wachache sana.

"Kama kweli Slaa angekuwa anakerwa kwa dhati ndani ya moyo wake na pengo hilo kwa nini asianzie kuchukua hatua kwenye ofisi za chama chake?," alihoji Nape.

Akijibu tuhuma zilizotolewa na viongozi wa CHADEMA, juzi, na kuripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari jana, Nape alisema viongozi wa chama hicho wanaweweseka kwa kuwa hawajazoea kusemwa.

Alisema kauli kwamba Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama anapata mshahara wa sh. milioni 11 ni ishara ya kuweweseka huko kwa sababu madai hayo hayakufanyiwa utafiti, hivyo ni ya uongo.

Nape alisema, licha ya kwamba Katibu Mkuu wa CCM ni kiongozi wa Chama tawala tena chenye vyanzo vingi vya fedha ikiwemo ruzuku kubwa kuliko CHADEMA, mshahara wake ni sh. milioni 1.5 na unakatwa kodi, ambao ni kiasi kidogo ukilinganishwa na ule wa Slaa ambao analipwa na chama ambacho ruzuku yake ni ndogo sana.

Pia Nape alimshangaa msemaji wa CHADEMA kumtuhumu kwamba anapokea mishahara miwili na ni miongoni mwa walionufaika na uchotwaji wa fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) na kwamba aliomba kugombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho.

Akijibu shutuma hizo, Nape alisema, huko ni kuishiwa hoja kwa viongozi wa CHADEMA kwa sababu, wakati uchotwaji wa fedha za EPA ukifanywa na mafisadi, alikuwa masomoni nchini India, 2005 na 2008.

"Je wanataka kusema kwamba fedha hizo zilinifuata huko?," Nape alihoji.
Kuhusu mishahara miwili, alisema hakuna ukweli kwani tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo, hajaanza kupata hata mshahara mmoja na kwamba, mara tu alipoteuliwa kushika wadhifa huo aliacha mshahara, nyumba ikiwa na kila kitu hadi vijiko na gari aliyokuwa akitumia akiwa mkuu wa wilaya.

Source: GAZETI LA MZALENDO

Comment
: Shutuma hizi ni nzito kwa mtu anayeheshimika katika jamii kama Dr Slaa.
Ili kutunza heshma yake iliyobaki, na kwa maslahi ya chama chake, ashauriwe ajiuzulu mara moja.

- Duh! mwaka huuu tutasikia mengi sana!

Es!
 
^500 milion kwa muda wa miezi tena chama bado hakina uwezo, je wakipewa ufunguo wa benki kuu? Si itakua balaa
<br />
<br />

Crap,hapo mwenyewe ndiyo umejitahidi ku-reason,hayo anayoyasema huyo mjakazi wenu Nape yangekuwa kweli mtu wa kwanza kujua angekuwa Jk!!
Pole sana!!
 
Mbona siwaoni viongozi wa cdm humu kama ilivyokuwa huko nyuma?Ni muhimu wakatoa ufafanuzi kuhusu hili.Kama ni uongo waseme ni uongo na sababu ni so and so.Al Gore alipokuwa akipiga debe kuhusu global warming.Walimponda kutokana na maisha yake aliyokuwa akiishi kutofautiana na yale aliyoyapreach.Mifano ya ya ndege alizokuwa akitumia,energy kwenye nyumba zake nk vilikuwa scrutinized,i mean you got talk the talk and walk the walk...Kama ni kweli katibu mkuu wa cdm analipwa zaidi ya katibu mkuu wa ccm,then there are some serious questions.
 
Wewe ulie leta hii, na hao CCM, CHAMA CHA MAGAMBA ndio mmeoza kunuka. hamjioni? Wenyewe mnaziba pua kwa harufu mlio nayo ya ufisadi na rushwa! Mtanzania wa leo si yule wa juzi.😛ound:
 
Tunashukuru kwa taarifa hii ambayo naamini si rasmi hivi kweli chama cha upinzani kiingize vifaa kwa njia za panya??? Inaingia akilini?, Usalama wa Taifa na dola kwa ujumla walikuwa likizo??? Kama walikamata visu fafe wakajitia ni vya CUF 2005 walishindwaje kukamata vifaa vya CHADEMA???? Jamani acheni hizo andikeni mambo yenye mashikooooo

Sasa naona Wananchi tunaanza kupewa mashtaka ambayo hata vifaa vya kiutendaji hatuna.

Ninavyofahamu CDM wanaanika uozo wa CCM ili tuwatoe madarakani tuwape CDM wakarekebishe hayo wanayoyaona, hainiingii akilini kwa sasa tunakoelekea kwa CCM nao ambao wana dola na mamlaka yote kuzuia uovu nao wanakuja kushtaki kwetu badala ya kuchukua hatua za utekelezaji na kutupa taarifa.

Hapa ndio naona CCM kupoteza muelekeo kwa kufuata mkumbo wa CDM kuibua uozo badala ya wao kuondoa huo uozo.

Rais ana lalamika, ccm wanalalamika, serikali ina lalamika, wananchi tuna lalamika, CDM wana lalamika - sasa tuna mlalamikia nani atakae kuja kututatulia haya matatizo yetu??

Sasa naona Nchi ndio imepoteza muelekeo jamani na sijui inaelekea wapi.

Napita tu tutakutana badae!
.
 
TRA hawezi kumjua kila anayekwepa kulipa kodi.
Ni jukumu letu Watz kuwaumbua watu hawa kama alivyofanya Nape.
Sasa TRA wamejjua na watachukua hatua.

naona unazidi kuanika kushindwa kazi kwa jk na tra yake. Kumbe cdm wanakwepa kodi mbele ya jk,alaf kwenye mikutano wanampa mikombora kibao,du jk ana gundu safari hii. Ila siwezi kuamini uzembe huu wa Tra kwa kuwa source ni jarida la matapeli. Lete kitu kingne ndo utaweza kuiharibia Tra!
 
Jamani waliambia na mkuu wa Magamba wawe wanajibu tuhuma. Matunda ya semina elekezi (teketezi). Tatizo ni kwamba hawana tangible issues, wanachomoka na chochote kile! Wacha waendelee kufunua upumbavu wao wananchi wajue.
 
Sasa naona Wananchi tunaanza kupewa mashtaka ambayo hata vifaa vya kiutendaji hatuna.

Ninavyofahamu CDM wanaanika uozo wa CCM ili tuwatoe madarakani tuwape CDM wakarekebishe hayo wanayoyaona, hainiingii akilini kwa sasa tunakoelekea kwa CCM nao ambao wana dola na mamlaka yote kuzuia uovu nao wanakuja kushtaki kwetu badala ya kuchukua hatua za utekelezaji na kutupa taarifa.

Hapa ndio naona CCM kupoteza muelekeo kwa kufuata mkumbo wa CDM kuibua uozo badala ya wao kuondoa huo uozo.

Rais ana lalamika, ccm wanalalamika, serikali ina lalamika, wananchi tuna lalamika, CDM wana lalamika - sasa tuna mlalamikia nani atakae kuja kututatulia haya matatizo yetu??

Sasa naona Nchi ndio imepoteza muelekeo jamani na sijui inaelekea wapi.

Napita tu tutakutana badae!
.

maneno yako mazito ndugu! Inawezekana nchi haina kiongozi!?!
 
hivi kuna gazeti linaitwa mzalendo??!nakumbuka mwaka 1988 ndo mara ya mwisho kulisoma gazeti hilo nikiwa darasa la 3.tokea wakati huo sijawahi sikia kuwa lipo.kuuumbe bado lipo!!! linauzwa wapi?!
 
CCM, acheni kuhangaika na CDM, mmeshaprove failure tayari! Jikiteni kwenye kuleta maisha bora kwa kila mtanzania!

Hilo lilishawashinda, ahadi zinafika Trilioni 90 hela ya mishahara ya watumishi wanakopa, ni wazi kuwa kilichobaki wameona bora wapige porojo porojo tu
 
MIMI NAHISI CCM MMECHANGANYIKIWA, CHANZO CHENYEWE GAZETI LA MZALENDO??? MIMI NAONA CCM MNGEWACHUKULIA HATUA KWANZA HAO AKINA RA NA LOWASA NDIPO MUWAGEUKIE CHADEMA. Mbona kibanzi chako hujakitoa unawezaje kuona boriti kwenye jicho la mwenzako.
Kwanza huo mmshahara wa Slaa kwani aliuomba au chama ndo kiliona anastahili alipwe kulingana na kazi yake?? Hawa CCM Kutimiza waliyoahidi kuwafanyia wananchi wameshindwa kazi kuuza sura tu huko mikoani. Ngojeni tu kwani kiama yenu sio mbali ni 2015 tu.

Nawe mtoa hoja(KISHONGO) Naona hoja yako haina msingi na hukuifanyia analysis badala yake uli copy na kupaste gazeti, cku nyingine jaribu kufanya analysis then tuanze kushusha comments kulingana na analysis yako. Haya magazeti yako kisiasa zaidi, so wewe kama critical thinker unatakiwa ufanye analysis
 
Mbona siwaoni viongozi wa cdm humu kama ilivyokuwa huko nyuma?Ni muhimu wakatoa ufafanuzi kuhusu hili.Kama ni uongo waseme ni uongo na sababu ni so and so.Al Gore alipokuwa akipiga debe kuhusu global warming.Walimponda kutokana na maisha yake aliyokuwa akiishi kutofautiana na yale aliyoyapreach.Mifano ya ya ndege alizokuwa akitumia,energy kwenye nyumba zake nk vilikuwa scrutinized,i mean you got talk the talk and walk the walk...Kama ni kweli katibu mkuu wa cdm analipwa zaidi ya katibu mkuu wa ccm,then there are some serious questions.

Kwa sababu hanuna cha ku-clarify au wewe unakiona? Viongozi hao walishasema kama kuna tuhuma zozote basi wapelekwe mahakamani. CCM ndio wenye dola - waitumie kama wana ushahidi; otherwise ni propaganda dhaifu.
 
jamvi hili sasa limeingiliwa na mamluki wa chama cha magamba. hizo tuhuma ni uozo mtupu.
 
Yani hii chama cha mapapa naona wamewa2ma wale wa**&+** humu ndani waandike thread sisizo na fikra. ILA HAWA NASHAURI WAPITIWE NA BAN bila ya kukosa kabisa. Wana2test mi naona.
 
Back
Top Bottom