Uovu mkubwa CHADEMA, ni kuhusu vyanzo vya mapato!

Uovu mkubwa CHADEMA, ni kuhusu vyanzo vya mapato!

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,830
WanaJF!

Viongozi wa CHADEMA, tofauti na vyama vingine, hawana desturi na utamaduni wa kuweka mambo wazi kuhusu vyanzo vya mapato na matumizi ya chama.

Usiri huo wa vyanzo vya mapato haufanywi tu kwa wanachama, bali pia ufanywa mpaka kwa msajili wa vyama vya siasa nchini, ambapo ni kinyume cha sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992.

Kuliweka sawa hili, ningependa ukione kifungu cha sheria kinacho eleza haya;

Kifungu cha 13 kifungu kidogo cha 1 (a-e) kinaeleza namna ambazo chama kinapata mapato.

Pia katika kifungu hiki hiki cha 13 kifungu kidogo cha 2 kinasomeka ;

...Every party shall disclose to the registrar information relating to any funds or other resources obtained by the party;

a) From sources outside United Republic, whether obtained directly or through the sources within the United Republic;

b) From foreign organizations stationed within the United Republic;

c) From any person resident in the United Republic who is not the citizen of the United Republic.

Kifungu mahususi chenye kuhitaji taarifa juu ya vyanzo vya mapato ya chama cha siasa (kama nilivyo orodhesha hapo juu) ni kifungu cha 13 kifungu kidogo cha 3, kinasomeka kama ifuatavyo;

…Any official of any party or other person liable to disclose information to the Registrar on behalf of any party relating to the funds or other resources of the party who fails to disclose such information or gives false information in relation to such funds or resources obtained by a party from sources outside the United Republic , commits an offence and shall be liable on conviction to a fine equal to the amount of the value of the resources not disclosed or in relation to which false information was given or to imprisonment for a term not exceeding twelve months or to both such fine and imprisonment…

Baada ya kuangalia vifungu vya sheria vinavyo onyesha namna ambavyo chama kinapata mapato na namna ambavyo chama kinahitajika kupeleka taarifa kwa msajili wa vyama vya siasa juu ya vyanzo vyake vya mapato, ningependa tuiangalie CHADEMA inavyo tekeleza hili.


CHADEMA imekuwa na usiri uliokithiri wa kuhusu vyanzo vyake vya mapato ndio inapelekea shutuma mbalimbali kuibuliwa dhidi ya viongozi wa makao makuu wa chama hicho hasa katika matumizi mabaya ya fedha.


Baadhi ya vyanzo vya mapato ambavyo ‘msajili’ hajapewa taarifa yoyoye na CHADEMA juu ya upokeaji wa mapato hayo ambayo ni kinyume cha sheria ni vifuatavyo;


Misaada kutoka kwa wafadhili na marafiki wa chama; fedha zinazotolewa kwa namna hii, taarifa zake hazifikishwa kwa msajili, lakini pia matumizi ya pesa hizi yamejaa urasimu, ukiritimba na ubadhilifu mkubwa;


a.
Fedha za Sabodo za kuchimba visima, visima vilivyo chimbwa idadi yake ni vinne tu kutokana na fedha hizo na vyote vimechimbwa kwenye majimbo ambayo CHADEMA wameshikilia. Huu ni ubaguzi na ukiritimba wa viongozi wa CHADEMA.

sabodo.JPGMbowe akiwa ameambatana na Dr Slaa akiwa anapokea hundi ya shillingi millioni 100 kutoka kwa Sabodo, pesa ambayo ililenga kujengea visima.

b.
Fedha za wadhamini kutoka nje ya nchi, kuna tabia ya viongozi wa CHADEMA kutembeza bakuli na kuomba omba wafadhili fedha ili wafanikishie mambo kama semina elekezi kwa makamanda na matumizi mengineyo.

kaga.JPGmakamanda wakiwa makini kusikiliza Semina elekezi ikiwa inafanyika kwenye hotel jijini Mbeya.


kigaila.JPGBenson Kigaila ambae ni mkufunzi akiwa anatoa semina kwa makamanda jijini Mbeya.

hotel.JPGHotel iliyopo jijini Mbeya ambayo kwa anasa za CHADEMA ndipo mahala ambapo wanafanyia semina zao.

Ila ukweli ni kwamba kwa wingu zito lililo funika upatikanaji wa fedha hizi, hakuna anae fahamu mapato ni kiasi gani yanapatikana kwa utaratibu huu wa kutembeza bakuli. Aidha, hata wafanyapo semina elekezi, gharama kubwa utumika kufanya anasa kuliko fedha kuelekezwa kuliko kusudiwa.


c. Operesheni za chama, CHADEMA imekuwa ikifanya opereshi rukuki, ila kikubwa ni usanii tu maana mantiki ya operesheni hizo ni moja tu, wameamua wawe wanatoa majina tofauti tofauti ili iwe rahisi kuwa rubuni watu ili kuweza kupata michango zaidi. Msajili wa vyama hajui kama kuna mapato makubwa yana patikana kwa utaratibu huu.

d.
Zawadi kwa chama, CHADEMA imekuwa ikipokeazawadi mbalimbali kutoka kwa wapenzi na marafiki wa chama, moja ikiwa ni eneo lenye thamani ya Tshs million 500 alilopewa bwana Mbowe kwa niaba ya chama na hayati Mawalla, ili eneo lipo Arusha na Mbowe alipewa siku nyingi tu na kutokana na siasa zake misibani alidai kuwa atajenga kituo kikubwa cha afya, ila mpaka leo eneo hilo ni chaka kubwa na kuna uwezekano limeanza kugaiwa kwa ‘’GIANTS’ wa chama.

Kwa usiri wa aina hii unao fanywa na viongozi wa CHADEMA dhidi ya msajili wa vyama vya siasa kinyume cha sheria, CHADEMA bado kitakuwa na uhalali wa kuaminiwa na watanzania? CHADEMA kitakuwa na uhalali wa kuinyooshea CCM kidole? CHADEMA itakuwa na uhalali wa kuunda serikali?


Kama wewe ni mzalendo, mkweli na muwazi, haya ni baadhi tu ya maswali ambayo unapaswa kujiuliza kuhusiana na ‘umafia’ wa kimaslahi unaofanywa na viongozi wa CHADEMA tena kwa kuvunja sheria za nchi. Ni imani yangu kwamba wengi mtakuwa mmeanza kupata picha ya kwanini CHADEMA hakiaminiwi na baadhi ya watu.


Angalizo: USHABIKI WA KISIASA NI HATARI KWA MAENDELEO YA TAIFA. KUWA MAZALENDO. KEMEA MAOVU. TANZANIA ISTAWI.
 
Umejitahidi kujenga hoja,lakini wewe si mkweli kwa sababu hakuna ushahidi wa kile unachotuhumu."nawasilisha"
 
Kama nimeelewa mchawi ni anayetakiwa kuhakikisha wanatenda hayo kwa mujibu wa sheria!!!!Nzi akitua kwenye chakula halaumiwi nzi ila amabaye hakufunika chakula

Zimewekwa sheria na msimamizi,ofisi na analipwa huyu ndo mchawi!!!!
 
Ngoma leo imeibukia huku? pole mkuu na uchaguzi wa Ausha!!! je umejifunza nini?
 
HAMY-D Njaa imeanza? umeanza mipasho, wenzako karibia ajira zinaota mbawa jiandae kukosa makombo ya rushwa posho kutoka Arusha haipo tena!
 
Sikuwahi kusikia hayo unayoyataka Chadema afanye yamefanywa na CCM, CUF, TLP, NCCR na kadhalika!!

Unachokifanya bila kujua ni kuhitaji maboresho kwa Chadema tu, ninahisi umeshatambua mabresho kwa CCM hayawezekani tena!! Au ni rahisi kuibadilisha Chadema na kuleta ufanisi kuliko kutaka kuibadilisha CCM na kupoteza vyote, fedha na muda!!

Ukituliza akili kidogo kabla hujapost, you will see a bigger picture and you will save us time and resources.
 
Pole sana ndugu yangu, mtatapatapa sana kabla ya kufa kabisa, wakati unaandika uchafu kama huo, fikilia wanyonge watanzania wanaokandamizwa na uongozi dharimu wa kifisadi wa ccm, tafakari na chukua hatua. Acha kutumika hivyo, ungana na wazalendo kupigania haki za watanzania. Tamaa yako ya vijicent isikupelekee kuingia kwenye dhambi itakayo kugharimu maishani mwako. HATUDANGANYIKI
 
Siku hizi kila kitu Chadema imefanya hivi, mara vile, kwanini Chadema tu,

Mkuu, hiyo imani ambayo vijana wanayo kwa CHADEMA wakati kwa uozo huu haipaswa tuisifu wala kuwa na imani na CHADEM, ila kama kweli mnakipenda chama chenu wahusika wa huu uovu wawajibishwe.
 
Hang Over za Arusha hizi.Ushenzi huu haukuwasaidia japo kushinda hata kituo kimoja kati ya vituo 136
 
Pole sana ndugu yangu, mtatapatapa sana kabla ya kufa kabisa, wakati unaandika uchafu kama huo, fikilia wanyonge watanzania wanaokandamizwa na uongozi dharimu wa kifisadi wa ccm, tafakari na chukua hatua. Acha kutumika hivyo, ungana na wazalendo kupigania haki za watanzania. Tamaa yako ya vijicent isikupelekee kuingia kwenye dhambi itakayo kugharimu maishani mwako. HATUDANGANYIKI

Wanyonge nawafikiria pia huku kwenye vyama naangaza, siwezi kuacha kuangaza huku kwenye vyama kisa tu Tanzania ina wanyonge. Mkuu, kuwa huru ushabiki ni hatari kwa maendeleo ya taifa.
 
Uchaguzi wa Kata ya Sombetini nimesikia utafanyika mwezi August 2013. Vipi, HAMY-D na wenzako mtatia timu tena?
 
HAMY-D Njaa imeanza? umeanza mipasho, wenzako karibia ajira zinaota mbawa jiandae kukosa makombo ya rushwa posho kutoka Arusha haipo tena!
Nashangaa sana kusema CDM inatembeza bakuli wakati hata CCM nayo inatembeza bakuli. Mimi naona alikuwa anataka kujifurahisha nafsi yake.
 
Mkuu, hiyo imani ambayo vijana wanayo kwa CHADEMA wakati kwa uozo huu haipaswa tuisifu wala kuwa na imani na CHADEM, ila kama kweli mnakipenda chama chenu wahusika wa huu uovu wawajibishwe.

CCM mmeshawajibisha mafisadi??? Vipi mkataba wa Serengeti hotel kwa miaka 99 mwekezaji atabakiza nini na kodi hailipi???..... Vipi waliotakiwa kujivua gamba..... Ondoa kwanza boriti ndani ya jicho lako ndipo utazame la mwenzako.....mfyuuuuu
 
Mkuu, hiyo imani ambayo vijana wanayo kwa CHADEMA wakati kwa uozo huu haipaswa tuisifu wala kuwa na imani na CHADEM, ila kama kweli mnakipenda chama chenu wahusika wa huu uovu wawajibishwe.
HAMY-D tangu juzi baada ya kichapo cha Arusha ulikuwa haujapata posho yako ya buku saba kwakuwa ulishindwa kupost. Naona leo umeamua kuingia mzigoni mapema ili angalau "watoto" wasilale njaa tena.

Kama ungekuwa unatumia akili yako sawasawa ungegundua kuwa Chadema ndio chama cha siasa pekee kilichokuwa wazi na mapato yake, si kwa kupeleka taarifa kwa msajili wa fvyama bali hata kwa wadau/wanachama/wananchi. Hata siku moja hatujawahi kusikia ama kusoma mapato na matumizi ya ccm au cuf yakiwa yamepelekwa kwa msajili ama yametolewa hadharani kwa wadau/wanachama/wananchi.

Kwa jinsi kada wenu Tendwa alivyokuwa na kisebusebu kama Chadema wangeshindwa kumpa taarifa ya mapato na matumizi yao bila shaka angeshatumia akili ya ukada kukiadhibu ama kukifuta kama anavyobwata kila akisikia jambo lolote la Chadema.
 
Last edited by a moderator:
We HAMY-D kama unavyojiita!!
Hivi wewe unaota ndoto gani, usiri mkubwa wa mapato upo CCM, hiki chama kinatumia billion and billions kwa chama. EPA etc etc
Cha ajabu zaidi hata mali ambazo zilikuwa za umma wakati wa chama kimoja zimekuwa za CCM.

Tuache democracy iendelee kukomaa, tusianze U-CCM Taifa kwanza.

CCM and followers, you cannot prevent change, you had this country for the past 50 years, people are poor, education has dwindled in standard, human resources are at their lowest, people are not motivated, corrupt, hungry, etc etc The motto should be change or die! We need change!
 
Back
Top Bottom