Uovu mkubwa CHADEMA, ni kuhusu vyanzo vya mapato!

Uovu mkubwa CHADEMA, ni kuhusu vyanzo vya mapato!

bado tunasherekea ushindi wa 4-0 hizo post tuletee baada ya mwezi mmja labda tutakuwa na nafasi ya kujadili... Sasa hivi tuache kwanza
 
  • Thanks
Reactions: Pai
Mkuu HAMY-D,

Hivi unalipwa Shilingi Ngapi kila utajapo Jina CHADEMA ?
 
Last edited by a moderator:
Kuna mengine umeongea vizuri hatuwezi kukupuuza, ya kijanja tutayachukua ila yale ya kijinga tutayaacha ufe nayo,
 
Hamy juz hukupatikana kabsaaa viwanja hiv, baada ya kugaragazwa vbaya kwa 4-0 leo unatuletea mashairi yako ya taarabu.In short no customer will deal with it.Jipangeeee!!!!
 
Wanyonge nawafikiria pia huku kwenye vyama naangaza, siwezi kuacha kuangaza huku kwenye vyama kisa tu Tanzania ina wanyonge. Mkuu, kuwa huru ushabiki ni hatari kwa maendeleo ya taifa.

Wee piga warawara zako wenzio wanaondoka
 
Wanyonge nawafikiria pia huku kwenye vyama naangaza, siwezi kuacha kuangaza huku kwenye vyama kisa tu Tanzania ina wanyonge. Mkuu, kuwa huru ushabiki ni hatari kwa maendeleo ya taifa.

Unafikiria wanyonge ama namna ya kushibisha tumbo lako. Soon mgawo wa BK7 unafutwa sijui utaishi vipi ilhal ulishaitangazia familia yako kuwa umepata kazi nzuri yenye mshahara mnono.

Shughulisha kichwa chako, acha kuiota CDM muda wote, unajiabisha
 
Hamy-D jaribu kuona aibu kidogo, wewe sio mwanachadema unatakaujue pesa za chadema kwanini? Wanachadema ambao huwa wanahudhuria vikao vya ndani vya chama wanajua. Wewe ukitaka kujua jiunge na chadema, SIO kuleta umbea na uchonganishi. Mbona mimi sijui pesa za CCM zinatumikaje pamoja na kuwa ccm ina majumba mengi ya kufanyia biashara hata parking zipo nyingi lakini mapato jijihangaishi kujua wala matumizi yake, je wewe mwana ccm UNAJUA YANAPATIKANA SHILINGI NGAPI na ZINATUMIKAJE? Pilipili ya shamba inakuwashia nini?

Jaribu kuwa mkweli usilete Majungu.
 
WanaJF!

Viongozi wa CHADEMA, tofauti na vyama vingine, hawana desturi na utamaduni wa kuweka mambo wazi kuhusu vyanzo vya mapato na matumizi ya chama.

Angalizo: USHABIKI WA KISIASA NI HATARI KWA MAENDELEO YA TAIFA. KUWA MAZALENDO. KEMEA MAOVU. TANZANIA ISTAWI.

.....sidhani kama mfupa ulomshinda FISI, mbwa koko atauweza.....alianza NEPI sembuse wewe HAMIDA???.....
 
Umejitahidi kujenga hoja,lakini wewe si mkweli kwa sababu hakuna ushahidi wa kile unachotuhumu."nawasilisha"

Mkuu, take it from me, hakuna jambo la uongo hapo. Tujifunze kukubali makosa ya viongozi wetu ili tuweze kuwakosoa.
 
Hamy-D jaribu kuona aibu kidogo, wewe sio mwanachadema unatakaujue pesa za chadema kwanini? Wanachadema ambao huwa wanahudhuria vikao vya ndani vya chama wanajua. Wewe ukitaka kujua jiunge na chadema, SIO kuleta umbea na uchonganishi. Mbona mimi sijui pesa za CCM zinatumikaje pamoja na kuwa ccm ina majumba mengi ya kufanyia biashara hata parking zipo nyingi lakini mapato jijihangaishi kujua wala matumizi yake, je wewe mwana ccm UNAJUA YANAPATIKANA SHILINGI NGAPI na ZINATUMIKAJE? Pilipili ya shamba inakuwashia nini?

Jaribu kuwa mkweli usilete Majungu.

Mkuu, raia mwema yeyote akiona uovu unafanyika ni wajibu kwake kupiga makelele ili uovu huo ukome. Ndio maana unaona hata mashirika binafsi serikali na watu wengine wanaingilia baadhi ya mambo. UFISADI ni adui yetu sote, hatuna budi kupambana nae.
 
Uchaguzi kunakushinda na kushindwa!
Cc:Nape Nauye,Hammy D,Ritz, buku7 team!!
 
Mbona unatokwa mapovu si usubiri uchaguzi uone km cdm ni halali au si halali.
 
Siasa za MACCM vichekesho kweli, kwa propaganda hizi za kiwendawazimu sijui mtamshawishi nani awe upande wenu na kwa hali sitoshangaa 2015 mkakosa hata mbunge 1 maana wananchi hivi sasa wamechoshwa na majitaka yenu bali wanataka maendeleo.
 
Waulize CCM ambao wanakula kodi zako na kunyanganya viwanja vyetu tulivyojenga kwa nguvu zetu, majengo mengi tulifyotaifisha pesa wanazipeleka wapi? haitoshi wameshiba sasa wanatuibia pesa kwenye mabank kama BOT-EPA. wauulize kodi zetu wanazipelaka wapi? katika uchaguzi wa 2005 waliiba kila kona walitaka kuuza shamba la mitiki pale mtibwa kwa bei ya kutupa shilingi bilioni 5 badala ya shilingi bilioni 12. kinara wa kuuza mitiki ile alikuwa zakhia megji akiwa waziri wa maliasili na utalii kipindi hicho. kama siyo ushujaa wa Dr Kilahama CCM tulishaibiwa. ona aibu.
 
Hammy D, maandiko yanasema toa kwanza kibanzi kwenye jicho lako ndio uweze kuona boriti kwenye jicho la mwenzako. Mapato na matumizi ya CDM umeyaona, yakwenu lini yaliwekwa wazi? Ukitaka kuwa kuanzisha hoja yenye mashiko sio lazima iihusu CDM pekee. Kosoa na umaamuma wenu pia.
 
Mkuu, take it from me, hakuna jambo la uongo hapo. Tujifunze kukubali makosa ya viongozi wetu ili tuweze kuwakosoa.

Hamy
Kwa kuwa wewe si msemaji wa CCM na kwa kuwa wajibu na cheo chako Lumumba unakijua mwenyewe (kufuta viatu) sitathubutu kukujibu. Ila tukuambie tu kwamba tuna folder lililojaa taarifa za mahusiano baina ya CCM na SPD ya Ujerumani na mambo waliokwishashirikiana, tuna taarifa za mashirikiano baina ya CCM na China kama serikali, tuna taarifa za ushirikiano baina ya hiyo CCM yako na Cuba kuhusu Green Guards. Tuna taarifa kuhusu USA, Canada, Doha, India, ANC South Africa, nk.

Tutakapofungua folder hilo nina uhakika watanzania watajua kwa nini nchi yetu ni masikini na bado tunatetewa sana na hawa CCM inaowaita nchi marafiki.

Usiwarushie waponda kokoto mawe"
 
Tunakushukuru kwa kuifanyia kampeni Chadema

Namshangaa mtoa mada, serikali iliyoko madarakani ni ya CCM na ndiyo yenye machinaries zote za kujua vyanzo vya mapato vya watu binafsi (wafanyabiashara), vyama vya siasa, NGOs, makampuni ya ndani na ya nje lakini bado wanalalamika na kupost threads kama hii. Kama serikali ya CCM haina uwezo wa kudhibiti vyanzo vya mapato katika nchi hii nani mwigine mwenye jukumu hilo?

John Tendwa ambaye ni hasimu mkubwa wa CDM iweje aitunzie siri CDM kama siyo uzuzu wa mtoa mada?! Au ndiyo namna ya kumpigia chepuo Twendwa kufuta CDM kwa madai ya kuwa na vyanzo vya pesa yasiyoeleweka? Shame on you magamba.
 
Hongera sana Chadema kwa mafanikio makubwa yaliyofikiwa,Sasa watu wote wanaifikiria Chadema,bila Chadema hakuna habari....haijawahi kutokea tangu mfumo wa vyama vingi kurejeshwa mwaka 1992.....Hongera sana sana Chadema!!!!!
 
Kipimo cha mapato ya chama kinapimwa na matokeo, fedha zinatumika mwisho wa siku tunaona wananchi wanawaelewa pamoja na changamoto ya kutupiwa mzigo wa lawama, juzi wamechukua viti vya udiwani wa Arusha ni mifano tosha ya matokeo mazuri ya kile walicho-invest hata bila kuleta mahesabu wananchi wana imani. Watz wanapenda utamaduni huu wa mapato na matumizi na ukiwasomea tu hata kama umechakachua watakusifia kweli wewe ni muwazi kumbe kuna vitu kibao vimechakachuliwa
 
Back
Top Bottom