Uongozi wa UDART, hivi kuondoa basi Kivukoni mpaka Kimara mwisho bila abiria kiuchumi ikoje?

Mpira wa kona

JF-Expert Member
Nov 25, 2016
350
338
Leo nikiwa kivukoni basi la mwendokasi limeondoka kivukoni huku Dereva wake akipaza sauti kuwa hasimami kituo chochote mpaka Kimara Mwisho huku akiacha abiria wengi kituoni. Najiuliza kiuchumi imekaaje.

1.Je angebeba abiria nini kingetokea?

2. Mafuta aliyotumia kwenda Kimara bila abiria.

3 Mafuta aliyotumia kwenda Kimara na abiria.

Viongozi wa UDART hebu tumieni elimu japo kidogo katika maamuzi yenu vinginezo hii ni hujuma kwa kampuni. Pia kumbukeni abiria wanataka kuwahi katika harakati za ujenzi wa Taifa.
 
Mtoa mada, nadhani tafiti kwanza utendaji kazi wa hizi gari. Nafahamu kidogo kuwa baadhi ya gari ni semi na express....ikitoka kimara kwenda kivukoni..kama ni asbh ikishashusha abiria kivukoni inageuka kurudi kimara bila kupakia kituo chochote hadi kimara...wakati zipo zingine zitapitia kila kituo...kuna wakati kadri ya muda, inaweza ikashusha na kurudi yard bila abiria,,,,jamani mfumo wa hizi si kama daladala, kwamba lazima ijaze ndo iondoke, kwakuwa zinapishana kwa muda fulani, basi kila dereva kapingiwa namna ya kufanya na wamewekewa tracking system gari zote, pale jangwani wanazimonita; hivyo kuna wakati wanaziamuru baadhi ya gari zilirudi yard, wakati mwingine kuziongeza barabarani nk....pia kila kituo kimefungwa camera system inayoonekana kule jangwani...hivyo hata yale malalamishi ya kuwa tunajaa sana vituoni bila gari kuja wanazidi kutatua mdogo mdogo...changamoto niliwahi sikia kuwa ni kwenye makutano ya barabara hasa ubungo na magomeni wakati Askari wanapoongoza kuliko Taa zinapo ongoza; ndio maana kuna wakati gari zinajazana mataa...hivyo kuaharibu ile interval ya hizi gari vituoni....

Kwao wao si hasara kutembeza gari bila abiria hasa kama wameamulu lirudi yard au liende haraka kituo fulani cha mwisho...ingekuwa daladala si mpaka wajae..sababu hesabu ni kwenda na kurudi....hawa kazi yao ni kubeba abiria ambao wameshalipia tayari...sio wanaongoja kulipia..ndio maana hakuna nauli ya kubargain, wala kumngoja mtu kituoni...
 
Kituo cha Gerezani kwa gari za Kimara ni pasua kichwa. Wanapaswa kuongeza magari kwa route ya Kimara kwa kweli. Ni zaidi ya mateso hasa jioni. Pia kituo hakiko user friendly maana msongamano ni mkubwa mno.

Mfumo wa kupanga foleni ungekuwa ni suluhisho kwa abiria kama ilivyo kwa gari za kwenda Mbezi. Waliangalie na hili.
 
Back
Top Bottom