Uongozi wa Mbezi Luis utumbuliwe haraka

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,308
6,884
Naandika haya wakati vijana wamachinga wakianza kujenga mabanda yao upya pembezoni mwa barabara.

Ni ukaidi kwa maelekezo ya Rais. Ni uvunjaji sheria uliopitiliza kwa watu kuonywa na kutolewa eneo husika kwa sababu husika na kukaidi.

Je, wamachinga wa maeneo mengine waliotolewa sio wa muhimu kama wa Mbezi Luis?

Kulikuwa na sababu gani ya kuvunja vibanda vya awali?

Tusipofanya maamuzi thabiti na kuchukulia hatua wazembe hatutapiga hatua hata moja mbele.
 
NASHANGAA HATA MIMI NIMEPITA MBEZI NIMEKUTA WAMACHINGA WANAREJESHA MABANDA ,,,nawapa pingezi viongozi wa Kibo,Baruti,Kona
 
Nasikia ni maelekezo ya mkuu wa wilaya Henry James, nimeshangaa sana hata mimi. Huku ni kukosa ujasiri kabisa wa kisiasa. Hakuna kauli thabiti katika hili, kila mtu anataka aonekane sio yeye anayetaka watu wafuate taratibu... WANASIASA NI WANAFIKI
NASHANGAA HATA MIMI NIMEPITA MBEZI NIMEKUTA WAMACHINGA WANAREJESHA MABANDA ,,,nawapa pingezi viongozi wa Kibo,Baruti,K
 
Dawa ya wamachinga ni kuwatambua kwanza kisha kuwarasimisha kwa kutoa leseni ya biashara ambayo kwayo inaonyesha aina ya biashara, sehemu ilipo biashara, jengo la biashara liwe la kupanga au binafsi....

Hii habari ya kuwadogosha wamachinga eti mitaji yao ni midogo ndio chanzo cha biashara holera.... Biashara haina udogo, ukiamua kufanya biashara, fuata kanuni zake na mambo yataenda tu.
 
Nasikia ni maelekezo ya mkuu wa wilaya Henry James, nimeshangaa sana hata mimi. Huku ni kukosa ujasiri kabisa wa kisiasa. Hakuna kauli thabiti katika hili, kila mtu anataka aonekane sio yeye anayetaka watu wafuate taratibu... WANASIASA NI WANAFIKI

Kwahiyo anampinga Rais?
 
Dawa ya wamachinga ni kuwatambua kwanza kisha kuwarasimisha kwa kutoa leseni ya biashara ambayo kwayo inaonyesha aina ya biashara, sehemu ilipo biashara, jengo la biashara liwe la kupanga au binafsi....

Hii habari ya kuwadogosha wamachinga eti mitaji yao ni midogo ndio chanzo cha biashara holera.... Biashara haina udogo, ukiamua kufanya biashara, fuata kanuni zake na mambo yataenda tu.

Yeah walipe kodi stahiki na wafuate sheria zote
 
Naandika haya wakati vijana wamachinga wakianza kujenga mabanda yao upya pembezoni mwa barabara.

Ni ukaidi kwa maelekezo ya Rais. Ni uvunjaji sheria uliopitiliza kwa watu kuonywa na kutolewa eneo husika kwa sababu husika na kukaidi.

Je, wamachinga wa maeneo mengine waliotolewa sio wa muhimu kama wa Mbezi Luis?

Kulikuwa na sababu gani ya kuvunja vibanda vya awali?

Tusipofanya maamuzi thabiti na kuchukulia hatua wazembe hatutapiga hatua hata moja mbele.
Nilikuwa hapo juzi nikawa napiga story na mfanyabiashara mmoja mwenye frem , akawa anakiri kuondolewa hao jamaa at least nao wameanza kupata kidogo maana wengine walijenga mbanda mbele ya frem za watu
 
Kuna taarifa DC ndio kawarudisha, Mkuu wa Mkoa tembelea huku mbezi lois uone namna huyu DC asie na adabu anakugeuka wewe pamoja na Rasi Samia, mchongee huyu mtu atimuliwe hana adabu kwa wakubwa zake.
 
DC wa ubungo aliwaruhusu warudi baada ya wamachinga kufunga barabara na kulala kwenye barabara kuu ya morogoro road

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Vijana waliomaliza vyuo walale barabarani? Wakulima wa korosho walale barabarani? Wafanyakazi mishahara haijapanda 6 years walale barabarani?
 
Back
Top Bottom