Stendi ya Mawasiliano vs Stendi ya Mbezi Luis

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,308
6,884
Kama ni mkazi wa Dar hizi stand mbili bila shaka utakuwa unazifahamu.

Ukizitazama hizi stendi utaona utofauti mkubwa wa uwezo wa kiutawala kati ya sehemu hizi mbili. Stendi ya Mawasiliano wamachinga wamekaa kimpangilio mzuri sana. Kuna vibanda vimejengwa pembezi ya hifadhi za barabara lakini vina hali nzuri. Wameacha njia za watembea kwa miguu na mazingira yao ni masafi, mitaro haijaziba na kiukweli panapendeza.Abiria wana mahali pa kukaa chini ya vivuli wakisubiri magari.

Eneo la soko limetengwa pembeni ya stand napo bidhaa zipo kwa mpangilio hazitandazwi chini soko ni safi muda wote.
Stendi ya Mbezi Luis ni mpya kuliko ya Mawasiliano lakini inauongozi mmbovu sijawahi kuona.

Haina mpangilio wa kueleweka wapi wakae wamachinga wapi wakae bodaboda na daladala zipark kwa utaratibu gani. Mabanda ya wamachinga yamejengwa juu ya mitaro, mitaro ni michafu, barabara ni chafu, hakuna maeneo ya abiria kukaa zaidi ya wa mwendokasi tu. Abiria wanapigwa na jua na mvua muda wote.

Hapaeleweki soko ni lipi, barabara ni ipi na stend ni ipi. Ni vurumai muda wote kuna wapiga debe na vibaka wengi wanaohatarisha usalama wa raia.

Naomba serikali iuangalie kwa karibu sana uongozi wa stendi ya Mbezi Luis kwa ukaribu sana stendi ni mpya lakini imekuwa kama dampo.
 
Hata gharama za huduma ya choo mbezi 500 na makumbusho 300 ila vyoo vya stendi ya mbezi viko HOVYO KABISA VINATOA HARUFU KALI SANA. Niliwahi kuwauliza mbona mawasiliano vyoo nj visafi na bei ya huduma iko chini? WALINIANGALIA KWA KUNIPENDA SANA
 
Japo kule kuna watu na mzunguko mkubwa kuliko Mawasiliano.
Unategemea kila kitu kiwe bora sana lakini sivyo
 
Kuna ripoti moja alitoaga cag akisema stand ya mbezi mahali ilipojengwa haikustaili kujengwa,eneo ni finyu sana na gaharama zake za ujenzi ni kubwa sana.....hapa ni siasa ndio iliyochangiwa na awamu iliyopita
 
Stendi ya Mawasiliano - chini ya Manispaa ya Ubungo (Mkurugenzi wa Manispaa)

Stendi ya Mbezi Luis - chini ya TANROADS (Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam)
 
Yaani iko hovyo hovyo
 
Stendi ya Mawasiliano - chini ya Manispaa ya Ubungo (Mkurugenzi wa Manispaa)

Stendi ya Mbezi Luis - chini ya TANROADS (Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam)

Basi hawa TANROADS ni wazembe sana
 
Ni stand ya Mbezi Luis au Magufuli terminal, huenda sijaelewa...
 
Kama ni mkazi wa Dar hizi stand mbili bila shaka utakuwa unazifahamu.

Ukizitazama hizi stendi utaona utofauti mkubwa wa uwezo wa kiutawala kati ya sehemu hizi mbili. Stendi ya Mawasiliano wamachinga wamekaa kimpangilio mzuri sana. Kuna vibanda vimejengwa pembezi ya hifadhi za barabara lakini vina hali nzuri. Wameacha njia za watembea kwa miguu na mazingira yao ni masafi, mitaro haijaziba na kiukweli panapendeza.Abiria wana mahali pa kukaa chini ya vivuli wakisubiri magari.

Eneo la soko limetengwa pembeni ya stand napo bidhaa zipo kwa mpangilio hazitandazwi chini soko ni safi muda wote.
Stendi ya Mbezi Luis ni mpya kuliko ya Mawasiliano lakini inauongozi mmbovu sijawahi kuona.

Haina mpangilio wa kueleweka wapi wakae wamachinga wapi wakae bodaboda na daladala zipark kwa utaratibu gani. Mabanda ya wamachinga yamejengwa juu ya mitaro, mitaro ni michafu, barabara ni chafu, hakuna maeneo ya abiria kukaa zaidi ya wa mwendokasi tu. Abiria wanapigwa na jua na mvua muda wote.

Hapaeleweki soko ni lipi, barabara ni ipi na stend ni ipi. Ni vurumai muda wote kuna wapiga debe na vibaka wengi wanaohatarisha usalama wa raia.

Naomba serikali iuangalie kwa karibu sana uongozi wa stendi ya Mbezi Luis kwa ukaribu sana stendi ni mpya lakini imekuwa kama dampo.
Ilitakiwa awali ya yote itawaliwe na nhia kami kila sehemu.

Ilipaswa kuwa direction kisasa zaidi na waongozaji na ssheria kusimamiwa. Ila sishangai. Nina mtu wa karibu anafanya kazi manispaa ya ubungo. Kwa namna mtumishi yule wa umma mamlaka zao zinavyohudumu ni hovyo kupindukia.

Hapa nielezee experience kidogo manispaa ya KINONDONI na Manispaa ya ubungo.

Kwanza baada ya kuamzishwa manispaa hii ya ubungo watumishi walihamishwa kutoka kino kwenda ubungo. Moja ya observation zangu. Ubungo walipelekwa wazembe. Yule mgatuaji mchagua wahamaji aliondoa waliokero KINONDONI na kuwatupilia ubungo.

Kama kawaida si wengine huchambua na kuangalia utofauti ubungo ikawa the worse manispaa in town.

Angalia barabara zake, Angalia huduma za afya. Elimu shule za msingi zinahali mby kupindukia, unakumbuka enzi za jiwe kuna shule ilishukiwa ikajengwa ndani ya miezi.

Kwa kifupi ubungo ni jangw la kitaifa

1. Hawajui kutumia mali walibarikiwa, stend safi usimamizi hovyo

2. Si wabunifu, creativity ni zero. Mzee wa watu na wahamdisi wamebuni ile mizunguko kam flyover. Ubungo leadership wanaona kawaida. Ile ni design safi kabisa. Morogoro road inavyo entechange ma domestic pathways hakkuna foleni tena, na Main Bus Terminal Mbezi Lois
 
Hata gharama za huduma ya choo mbezi 500 na makumbusho 300 ila vyoo vya stendi ya mbezi viko HOVYO KABISA VINATOA HARUFU KALI SANA. Niliwahi kuwauliza mbona mawasiliano vyoo nj visafi na bei ya huduma iko chini? WALINIANGALIA KWA KUNIPENDA SANA
Upande wa vyoo mbezi nilivipenda, ila kwa pale kuna machawa sijui ndio wapenz wa jinsia moja, ukikosea tu utashambuliwa
 
Hata gharama za huduma ya choo mbezi 500 na makumbusho 300 ila vyoo vya stendi ya mbezi viko HOVYO KABISA VINATOA HARUFU KALI SANA. Niliwahi kuwauliza mbona mawasiliano vyoo nj visafi na bei ya huduma iko chini? WALINIANGALIA KWA KUNIPENDA SANA
Duu kukata gogo 500?, hii kiboko.
 
Back
Top Bottom