Uongozi mathubuti wa mbowe unavyoinyima usingizi CCM

Kizuio

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
845
Reaction score
522
Kwa muda mrefu kumekuwa na hoja kutoka kwa wana CCM kwamba kwa nini Mbowe amekuwa mwenyekiti kwa muda mrefu kama kwamba ni mfalme na kwa nini hataki kupisha watu wengine wakiongoze chama hicho.

Je, CCM wanakitakia mema Chadema? Jibu ni wazi ni hapana. Wanafanya hivyo ili kukiondolea Chadema uongozi wenye uzoevu chini ya Mbowe. Mambo yafuatayo yameongeza shida katika chama tawala—ruzuku ya chama tawala imepungua baada ya Chadema kuongeza viti vingi bungeni na katika mabaraza ya serikali za mtaa kufikia hata baadhi ya maeneo nyeti na mikoa mikubwa, kuwa chini ya upinzania, mathalani, Jiji kubwa la kibiashara—Dar es Saalam na majiji ya Mbeya, Arusha, na manispaa za Moshi na Bukoba. Hapa lazima Mbowe apingwe na aonekane king’ang’anizi ndio maana wanamfananisha na mfalme. Nia ni kuwafanya wana Chadema wamwone hafai wamtupe chini, ili iwe rahisi kwa cha tawala kurejesha ufalme wake.

Mbowe ni kiongozi mwenye misimamo usioyumba—hasa kwa nafasi yake kama Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni. Hili nalo nikikwazo kikubwa kwa chama tawala. Wanafikiri kwamba kuwa na mtu imara na jasiri kama Mbowe, kutaendeleza msuguano mkubwa kutoka kambi ya upinzani na kwa jinsi upinzani unavyosimama kwa umoja, imekuwa vigumu sana kuwagawa chini ya uongozi wa Mbowe. Kuondoka kwa baadhi ya Wabunge kutoka Chadema ni mbinu moja wapo ya kumdhoofisha Mboye kisiasa.

Mbowe amekuwa kiungo muhimu sana katika umoja wa Katiba ya wananchi ( Ukawa), pamoja na baadhi ya wenyeviti wenza kuchechemea, yeye ameendelea kusimama imara, hivyo kwa vyovyote ni mtu asiyetakiwa na chama tawala—maanan ni sehemu ya kikwazo cha maslai ya chama tawala

Mbowe ni mjuvi wa siasa za majukwaani, ni miongoni mwa wanasiasa wachache sana hapa nchini, wanaojua kujenga hoja mujarabu wawapo jukwaani, ni mzungumzaji mzuri sana, hivyo kumzima kwakupiga kelele kuwa hafai, ni ndio kiwango cha uzito wake katika kujenga hoja na ni mwiba kwa CCM. Inabidi aondolewe katika majukwaa ya kisiasa kwa namana yoyote ile. Kuhamahama kwa wanachama hasa kutoka Jimbo la Hai analoliwakilisha bungeni, wanachama wa Chama cha Mapinduzi wanamnyooshea vidole Mbowe kwamba ndiye chanzo cha wanachama kikimbia Chadema.

Lakini pia ni jambo la kujiuliza toka lini CCM kiliamua kupigia kelele uwenyeviti wa Augustine Mrema wa TLP, John Cheyo wa UDP na akina Dovutwa, Prof Lipumba na wengine wa aina hiyo. Jibu,ulalo kichwani mwako. Akili za kuambiwa changanya na zako.

Kama magufuli alivyosema watatawala milele tanzania [emoji1241] basi ni lazima police watumike kuinyanyasa chadema kinyume na sheria na kuhakikisha mbowe anachafuliwa kwa namna yoyote ile
Mbowe ametafutwa sana kwenye biashara zake ili tu wampate na kosa lakini hawajafanikiwa sasa wanatumia mbinu ileile ya kumzushia kuhusika katika kifo cha wangwe na sasa wanayatumia ipasavyo magazeti ya tanzanite, uhuru na jamvi la habari kumuhusisha tena na kupigwa risasi Tundu lisu

Bahati mbaya kwao lisu yuko hai na anazipinga hoja zao kwa mbowe kikamilifu
hii Hama Hama pia inahusika kwa lengo lile lile la kumchafua mbowe

Mbowe kama mbowe ana mapungufu yake kama binadamu lakini cha kushangaza toka ccm ikabiliwe na upinzani mkali wa Chadema na vyama kuungana ccm ni kumtukana mbowe pamoja na Chadema

Sote tunajua wakati Nccr mageuzi ikiwa juu nini walizushiwa
Sote tunajua wakati Cuf ikiwa juu nini ilizushiwa
Na sasa chadema inatafutwa vilevile ila tofauti ni kwamba wamekumbana na mwamba Mbowe ambaye anazijua mbinu zao zote

Mwaka 2004 nilikuwa ccm kindakindaki lakini mtu mmoja tu aliibadilisha akili yangu mwaka uliofuatia 2005 naye si mwingine ni Freeman Mbowe kiongozi shupavu barani Africa

Tuendelee kumuunga mkono

Anayefikiri kutumia tume ya uchaguzi, police, magereza, mahakama ataiua Chadema anajisumbua sana
 
Mbowe
images.jpg
go9g1385.jpg
 
Mathubuti ndiyo kitu gani wewe?
 
Hakuna cha madhubuti wala nini, Mbowe yuko soft sana siku hizi, kawa muoga sana, watu wake wanaonewa na kuumizwa kila siku hakuna kitu cha maana kinafanyika zaidi ya press zisizo na kichwa wala miguu, unaambiwa Mbunge wako kaumizwa na police huko na kalazwa mahabusu bila kosa unashindwa kusimama kiume kumtetea, upole huu wa upinzani ndo unafanya haki zinaminywa na katiba haifuatwi, upinzani umekua wa kimaneno zaidi kuliko vitendo, siku watu wagome kuonewa afu police waue watu zaidi ya 20 muone hii nchi itakavyokua na adabu... Ila kwa mwendo huu wa upinzani, haki tusahau.
 
Una uhakika kwamba hakuna mwanachama wa CHADEMA mwenye kutaka kufanyike mabadiliko ndani ya chama? Kama hawako, basi msipoteze muda kudai demokrasia nje ya chama!
 
Hakuna cha madhubuti wala nini, Mbowe yuko soft sana siku hizi, kawa muoga sana, watu wake wanaonewa na kuumizwa kila siku hakuna kitu cha maana kinafanyika zaidi ya press zisizo na kichwa wala miguu, unaambiwa Mbunge wako kaumizwa na police huko na kalazwa mahabusu bila kosa unashindwa kusimama kiume kumtetea, upole huu wa upinzani ndo unafanya haki zinaminywa na katiba haifuatwi, upinzani umekua wa kimaneno zaidi kuliko vitendo, siku watu wagome kuonewa afu police waue watu zaidi ya 20 muone hii nchi itakavyokua na adabu... Ila kwa mwendo huu wa upinzani, haki tusahau.
Siku zote ccm wanataka kuihusisha chadema na ugaid na mateso yote haya kwa upinzani ni ushahidi wanatafuta
Mbowe hutumia akili nyingi sana
Unakumbuka kesi ya ugaid aliyopewa lwakatare mbunge wa bukoba mjini
 
Wewe kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri KWAMBA CCM NI MWAMBA HASWA!
Watapiga wapuuzi na waoga tu na Wenye njaa ila sisi mashetani hatutapiga wala kukiri tutaendelea kuwa mashetani kwa ccm daima
 
Mbowe dikteta tuu hana lolote wewe toka 1998 yeye tu ndo mwenyekiti tukimpa uraisi jee c ndo atakuwa kama mseveni
 
Back
Top Bottom