Kishongo
JF-Expert Member
- May 4, 2010
- 932
- 64
Inasikitisha kuona jinsi wabunge vijana wa Chadema wanavyonyimwa fursa za kujifunza kutoka kwa wabunge wengine wazoefu kutoka vyama vingine.
Kipindi hiki ndicho muafaka kwa vijana hawa kugema elimu, busara na uzoefu wa wenzao kwa njia ya kubadilishana mawazo. Wenzao kina Zito na Halima walipata fursa hiyo walipoingia bungeni kwa mara ya kwanza. Hata Mbowe na Slaa walipitia mkondo huo huo, ndio maana sasa wanaonekana kubobea katika siasa na bungeni.
Kwa sasa ni vigumu sana kwa wabunge vijana wapya kubadilishana mawazo wazi wazi na wabunge wa CCM, CUF au NCCR. Hii ni kutokana na ukweli kwamba akibainika kufanya hivyo wataitwa msaliti na majina mengine yanayofanana na hilo. Matokeo yake wanaishia kuulizana na kuelimishana wenyewe kwa wenyewe, na kuishia kudanganyana au kurithi mapungufu ya viongozi wao.
Ikumbukwe kuwa vipaji vya vijana hawa ni hazina ya taifa na si ya Chadema. Uongozi wa juu wa Chadema kuendelea kuwatenga, kuwatisha/kuwaogofya wasishirikiane na kupata uzoefu kutoka kwa wabunge wengine ni sawa na kuwamaliza kisiasa.
Aina hii ya uongozi ndiyo imeanza kukimaliza chama kwa sababu haina upeo na haizingatii maslahi ya Taifa.