Uongo Wikipedia kuhusu Dini Tanzania

Uongo Wikipedia kuhusu Dini Tanzania

Halafu kuhusu CIA kujua kila kitu sio kweli hizo hadithi za wajinga

Mitume na Manabii pamoja na Mashetani hawakujua kila kitu hata malaika hawajui kila kitu kwa mujibu wa imani yangu na kwa mujibu wa wanasayansi pia na kwa mujibu wa mtu yoyote.

Nimewapa link hapo CIA wakikiri kuwa huwa wanadanganya public sana kupitia media na njia nyingine.

Takwimu wanazitoa wapi yaani simple logic tu halafu hizo ni za kwao na mimi nachoshangaa kabisa ni kuwa hiyo issue serikali yetu long time haikutaka kujua idadi hiyo

Nachokwambia mfano wangeandika kuwa raisi wetu ni Lowasa lazma wahusika wangehusika lakini kwenye hili tena ambalo huwa wanalikataa sana mbona hawachukui hatua kutoa hizo data za uongo
Lowassa siyo Rais ndiyo maana hawajaandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani sida ni nini hapo. Mahali fulani imeandikwa waungwana huchunguza. Naona watu wanabisha halafu hawana hizo takwimu wanazozani ni sahihi. People are subjective instead of being objective. Una takwimu sahihi kutoka vyanzo vinavyojulikana tupia siyo mnaleta siasa. Otherwise Wikipedia stands and remains correct. Full stop..!
 
Echolima -huyo chalii anamkaribia Dr. William Campbel?, hiyo video ilishasambaa whatsapp zote tunayo, huyo amewah kufanya Debate na nani duniani? Muangalia Dr Zakir katika 'Universal brotherhood'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante ndugu mi nashangaa watu wanaleta udini hata ingeandikwa 50% kwa 50% siyo sawa na pia CIA kupitia source zao wakiamua kuandika hicho kitu kwa wanavyoamini wao kwenye website zao au vitabu vyao hiyo ni shauri yao lakini kwenye page ya WIKIPEDIA AMBAYO INAHUSU NCHI YETU ilibidi vitu vingi vya takwimu vitolewe na serikali yetu au viwe approved na serikali.
Ngoja tumalize kupima mikojo ili tupate na idadi kamili ya wachochezi...
 
View attachment 558921 Habari ndugu,
Nimefungua wikipedia nlikuwa napitia nchi yetu hii TANZANIA lakini ajabu nimekuta takwimu za dini, lakini nijuavyo mimi nchi yetu huwa haina idadi wala makadirio kati ya WAISLAMU NA WAKRISTO.

Sasa hawa wikipedia wanadai hizi data wamezipata kutoka CIA.

Tanzania - Wikipedia
Leta takwimu sahihi, siyo unapinga tu.

Sent from my Nokia ya Tochi using JamiiForums Mobile App
 
Ss km huamini basi! Wikipedia kila mtu anaweza kuandika na kuedit chochote ndo maana waalimu wengi hawapendi wanafunzi wao waitumie km reference point! KAMA UNAAMINI WIKIPEDIA INA UHUSIANO NA CIA HAYA ENDELEA..

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya nimesearch Kenya nimekuta hao hao jamaa wameweka takwimu za MAKABILA lakini hawakuweka za DINI.

Ndio muwe mnajua hawa watu ni hatari wanajua kumanipulate vitu.

Sasa sijui hizo za makabila kenya wamezipata wapi pia na ikawaje wakashindwa kupata za dini huko.

View attachment 559173
 
Kenya hiyo hiyo wikipedia vipi hao mnaowaabuudu CIA MBONA hawajaweka TAKWIMU za dini lakini eti wameweka za MAKABILA!?
 
Kwani sida ni nini hapo. Mahali fulani imeandikwa waungwana huchunguza. Naona watu wanabisha halafu hawana hizo takwimu wanazozani ni sahihi. People are subjective instead of being objective. Una takwimu sahihi kutoka vyanzo vinavyojulikana tupia siyo mnaleta siasa. Otherwise Wikipedia stands and remains correct. Full stop..!
Mubindi,
Suala la takwimu nchi petu baina ya Waislam na Wakristo ni jambo nyeti
sana na kwa hakika Afrika yote hili ni jambo linaloleta ubishani mkubwa
sana.

Wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes ilifika mahali lazima hili suala
nilizungumze.

Naweka hapo chini kile nilichosema:

''According to the 1957 population census, Muslims outnumbered Christians at a ratio of three to two. This, at that time, meant that Tanzania was a leading Muslim nation South of the Sahara. But in the first post-independence census of 1967 the total figures for Tanzania Mainland were 32% Christian, 30% Muslim and 37% local belief (August H. Nimtz Jr, Islam and Politics in East Africa, University of Minneapolis, 1980, p.11). These figures show Pagans as a leading majority in Tanzania. The 1967 census has not been able to show the reasons for the sudden decrease of Muslim population nor the growth of animists amidst believers in the span of the last ten years.

This was the last population census showing religious distribution.

Unfortunately power sharing in the political system in Tanzania is very much skewed against Muslims, although it is known that the stability of any nation depends on proper balancing of these facts. Different sources provide different Muslim -Christian religious distribution figures. These conflicting figures are as a result of sensitivity of the issue. Among African countries with sizable population of Muslims and Christians, like Tanzania and Nigeria,[1] the inquiry as to which faith commands a leading majority, is a source of potential conflict and controversy. Tanzania is of no exception. D.B. Barret[2] gives figures which show Muslims as a minority in Tanzania. The Muslim population is purported to be 26%, Christian 45%, local belief 28%. Tanzania National Demographic Survey figures for 1973 put Muslims in Tanzania slightly above Christians at 40%, Christians 38.9% and local belief 21.1%. But according to Africa South of The Sahara, [3] Muslims in Tanzania are a leading majority at 60%. This figure has remained constant in all its publications since 1982. Since research by Tanzanian Muslims on Islam is scant or almost non-existent, the issue of Muslim population has yet to be tackled from an Islamic point of view. [4]

Distribution of authority and power sharing is a factor which should not have been a cause of conflict in independent African countries. Ironically this has become a point of controversy only under indigenous governments.

It is a sensitive issue because ethnicity, religious identity and clanship is an important factor in independent African states. Power distribution and numerical strength has also to be reflected in the sharing of political power along those lines.

During colonial rule, distribution of power under ethnicity and religious bias in Africa by colonising powers were not perceived as so serious a breach of trust by subjects as to warrant civil upheavals.

Fortunately tribalism is not pronounced in Tanzania, but religion has been a factor of discrimination since colonial days.''

[1] Ali A. Mazrui, ‘African Islam and Competitive Religion: Between Revivalism and Expansion’, in Third World Quarterly Vol. 10. No. 2 April, 1988, pp. 499-518.
[2] D.B.Barret, Frontier Situations for Evangelisation in Africa ,Nairobi, 1976.
[3] Africa South of The Sahara, Europa Publication, London, No. 20, 1991, p. 1027.
[4]The only conclusive Muslim research is by Dar es Salaam University Muslim Trustee (DUMT), see 'The Position of Muslims and Islam in Tanzania', in Al Haq International (Karachi) September/October 1992.

Bahati mbaya nimeandika haya katika Kiingereza lakini tunaweza tukafanya mjadala kwa Kiswahili.

Katika hayo niliyoweka hapo juu nimefuta kipengele kimoja kinachosema kuwa takwimu za sensa ya mwisho iliyokuwa na kipengele cha dini ''zilichezewa.''

Nimekifuta makusudi kwa kuwa ingawa ipo ''citation,'' nina hakika kitasababisha mapambano makali hapa jamvini.

Sasa turudi latika hizi takwimu za CIA.

Nilikuwa nafanya mhadhara Chuo Kikuu Cha Iowa, Marekani kuhusu ''Uislam
na Siasa Tanzania Historia ya TANU na Uhuru wa Tanganyika.''

Katika mhadhara ule nilieleza sababu za Waislam katika takriban miaka 20
iliyopita kuwa na maandamano na mapambano ya mara kwa mara na serikali.

Nikaeleza sababu kuu ni kuwa Waislam wamekuwa pembeni katika elimu na
hivyo kuwa pembeni katika kugawana madaraka ya kuendesha nchi.

Waislam walitaka hili liangaliwe na serikali kwani ipo harufu ya hujuma.

Katika kipindi cha maswali na majibu na ilipobaki kama dakika tatu hivi nihitimishe,
ndipo likaja swali hili lililokuwa na takwimu za CIA na muulizaji alikuwa profesa wa
historia akasema kuwa wakipatacho Waislam wa Tanzania hiyo ndiyo haki yao kwa
kuwa wao ni wachache, yaani ni ''minority.''

Hili swali naamini liliwekwa hadi mwisho kwa kuwa katika mazungumzo yale walitaabika
sana ni historia ya uhuru niliyokuwa nawafunulia, historia ya wazalendo Waislam
katika kupambana na ukoloni, historia ambayo kwao wao ilikuwa ngeni.

Wao walizoea mihadhara ya kuja na historia rasmi iliyomtaja Mwalimu Nyerere
peke yake kuwa ndiyo aliyoikomboa Tanganyika kutoka kwa Waingereza.

Hawakutaka nitoke pale kichwa juu kifua mbele walitaka wanifedheheshe kwa hizi
takwimu za CIA zinazonyesha kuwa Tanzania ina Waislam wachache na mambo
yote ni shwari ila kwa vurugu hizi za, ''Waislam wa siasa kali.''

Historia yangu ilikuwa imewahuzunisha.

Katika hadhira ile alikuwapo Prof. James Giblin aliyafanya utafiti na kuandika kitabu
kuhusu Vita Vya Maji Maji.

Alikuwapo pia Prof. Michael Lofchie aliyeandika kitabu kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar,
''Revolution in Zanzibar,'' na hawa wote wameishi Tanzania na wanaijua vyema.

os3Jmwpepk4NjhnyO-GRdVBgq2VfpE6UEmxTCH7jdJqm5BCXLzDJWFQsiJo9AOqcCNREkE5XswCD4znagHfGcD2He8I1MkeHSN30GtQdtyhOxo1HxphA4ZUzuyV58eGRrItZaAUJj2VzOUa1xrxIVDKvO2N-ad9WZPhWQiBLy9h_5M8Vub-0rmtEzAyIaK-n2Sf9R8q9ZHCWgOm_XggpwcG0RaTKkEaBQOixteQkK_wBnA-NSiVtg38as2YwEaSSoPxkixbt53ETo5Oc5-ciLXniQWAqmWIwEswcg9-w_25Vsoa37Zyi-YBdiJHVYc2F6Px8ZPDqTvx07lNgFK8_xbfa-ZuXlCUoPzGO5WlgrrRkDHvrm9mPkS19WE_G8NT6JBm3ndKxEcqCskbqKYL_iYKmSLCHKrj_h-yY1QAmxRY0JQ9aHPPnPO6MxQ4_Ef-oqi_0VrtMI5YiTWrr_obrKsIOurgY_aXaDLwTLy0bYLnSejMSnH7LFnHAWbEq6WeMg3QlErglLdt0Sikurx8dO8Ck5CMcRw6paC3w1WQpqfUuwUEL2cJGdTe2ZUWfrgpTe_N_n1nIfSNuUoHl9eeffN_sHn38EUo9y0jbcMxLnd0uVfDWBgP9oA=w480-h360-no

Prof. Michael Lofchie

uslD_NF9P_43JbzRHnr10bTDrA3JTk0Iku6owEC6hHJaKBEgGOIJ6CsCfBuom1ECmtd61X6COn6-L8oynJO8e9f60uCAoWkXIBF1Zui7W9aGms4m9nRIXCB2EUrJ0JseVM-3w2eethNB-MEsZvHwS2AqQHeBOlgUYlbohuwOD3qDfqHSExxqkQAPW_ac5TYS_B4S6tNRSmk1CBCg9mgATT42PK_uJ2QJ3lue5orb--nE68xdktQrLE-TJWi_BFycWBo1Gt_9mKR5m0IY--8rhPr-HXPi6MclEizaxCBnc1lsvSbrb-gMS-fwEqL1MJ1nhnNzROfdlO3sfU-JTBv_IyPWOs-UnfqYhfsLqKkIwcDqnggI6rKRrFRzMeru7zNqOU7xswgjxbp56HKmeoGeEqWIwy0UBF5pvBMtwPlgGZHSJLAt1Um-Oeu-7SYekWpfY6lXqJqwNssVhzdjwbpXSd1s-QwhChqttdlCHZMuodL-q6ZML4z8GJNbU0LbpiEiIRuvi_QE97e-SNBzVTTrJ-gHTw_-SWWlnttIodhK_sjxxgYhcPTf6_y1I167xamD1V956He3hr7RMA48UIY49SrZbLS_UQ25oLPYWSDS1hpiv2bX8-SYhw=w480-h360-no

Prof. James Giblin

Jibu langu kwao halikuwa kwangu mimi kugonganisha takwimu zangu kama zilivyo
katika kitabu cha Abdul Sykes, na takwimu zao za CIA, la hasha.

Mimi nilijibu swali lao kwa kuwauliza wao swali.

Niliwaambia kuwa naomba wanionyeshe nchi yoyote duniani katika historia yao
wananchi walio pungufu yaani, ''minority,'' walionyanyuka na silaha mikononi
kupambana na taifa lililoingia katika nchi yao kwa nia ya kuwatawala.

Nikawarejesha katika hitoria ya Vita Vya Maji Maji na kuwaambia wafanye rejea
na waangalie ni nani waliunda majeshi ya kupambana na Wajerumani.

Nikawakumbusha kisa cha Sultani Abdulrauf Songea Mbano wa Wangoni
alivyonyongwa na Wajerumani kwa kuongoza vita dhidi yao.

Nikawaambia wafanye tena rejea waangalie harakati za siasa za uhuru zilipoanza
baada ya Vita Vya Pili Vya Dunia (1938 - 1945) ni nani walikuwa mstari wa mbele
katika, ''nationalist politics,'' Tanganyika?

Kweli inawezekana adui aingie katika nchi bila ya ridhaa ya wenye nchi na ikawa
walionyanyuka kupinga uvamizi huu wakawa ni wale, ''minority?''

''Majority,'' ya wenye nchi wako wako wapi hadi mapambano ya kuikomboa nchi iwe
mikononi kwa ''minority,'' na katika Tanganyika iwe Waislamu?

Ukumbi wote ulikuwa kimya.

Maprofesa wa historia ya Afrika walikuwa wanajaribu bila shaka kutafuta mfano
utakaoweza kupambana na hoja yangu.

Hawakuweza kuupata.
Nchi zote duniani mapambano ya ukombozi huongozwa na wale waliokuwa, ''majority.''

Nikamaliza kwa kusema kuwa sina ugomvi na takwimu za CIA lakini Waislam wa
Tanzania wanaujua ukweli.

Palepale Jonathon Glassman bingwa wa African History kutoka Northwestern University,
Evanston Chicago akaniomba niende chuoni kwake tukafanye madahalo kama ule
tuliofanya pale Universty of Iowa.

Glassman amekaa sana Pangani na Tanga mjini wakati anafanya utafiti wake na
kaandika kitabu ''Feats and Riots,'' anaijua vizuri Tanzania.

Nilikubali mwaliko na nilizungumza Northwestern University, Ukumbi wa Eduardo
Mondlane
.
 
Mleta mada naona wengi hawajakuelewa bado!! Mleta mada kauliza kua in Tanzania watu hawahesabiwi kwa dini zao,sasa hao CIA wamepata wapi hiyo accurate figure?
ila hutoa taarifa za dini yake. Hivyo ni rahisi sana kupata idadi japo hata kwa makadirio.
 
[HASHTAG]#mohamed said[/HASHTAG]

Hapa watu wanajitoa fahamu,
Nimewapa link kuonesha CIA WAKIKIRI kutumia MEDIA kudanganya UMMA kwa malengo kabisa,

jirani ya Tanzania,KENYA.
takwimu za Kenya hazikugusia DINI lakini badala yake wameonesha UKABILA ndio ninachojaribu kuwaonesha wenzangu wajiulize kuwa kwa vipi hao CIA hawajaweka takwimu za DINI nchini Kenya kwenye hiyo article yaKenya kwenye Wikipedia.

Propaganda and Disinformation: How the CIA Manufactures History

Na

https://www.google.com/amp/www.glob...edia-to-distribute-disinformation/5424860/amp
 
Nani anaweza kunijibu ? ? Ni kwa nini sensa ya tanzania 2012 waislam walikataa kata kata wasihesabiwe ? ? walikuwa na lengo gani ? ?
 
Silicon...
Soma jibu la Waislam hapo chini:

BAKWATA yatangaza rasmi kutoshiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Tanzania
13/6/2012

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini. “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.

Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

“Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

“Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.

Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.

Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.
 
Shukran nimeelewa
 
Back
Top Bottom