Uongo Wikipedia kuhusu Dini Tanzania

Uongo Wikipedia kuhusu Dini Tanzania

Naelewa mkuu lakini
Inakataa nilishajaribu nikaweka unknown wamefuta jaribu wewe

Kingine mamalaka zetu ziko wapi kuona kama data za nchi zinawekwa za hovyo inatakiwa wakemee
Hivi mnataka mamlaka zijisumbue na kupoteza muda kuhusu imani zilizokuja kwa merikebu kwa lengo la kutugawa!!

Ili iweje?

Mamlaka ishughulikie matatizo ya afya maji makazi chakula elimu umeme barabara nk. Hayo ya imani katiba hairuhusu maana imeandikwa MAMLAKA HAINA DINI.

Nchi ya makafiri hii sheikh. Huamini badi toa takwimu zako hapa kama zinakubalika na wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Israel waislamu ni wengi kuliko christians,tumia hicho kisimu chako kupata elimu kuliko kukitumia kwa kutokwa povu humu jf au kuandika usichokijua.
Asante Mkuu, nina imani hiyo haikuwa yangu,nilichokuwaa najaribu kumuambia ndugu hapo ni kuwa amedai mimi Mdini kwa kusema ISRAEL sio taifa kubwa ni propaganda tu sana zinapigwa ndo nikawa najaribu kumuelewesha.
 
Silicon...
Soma jibu la Waislam hapo chini:

BAKWATA yatangaza rasmi kutoshiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Tanzania
13/6/2012

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini. “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.

Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

“Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

“Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.

Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.

Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.
Hili jibu KUNTUUUU kabxaaa ni LIVE wala haina chenga

Sent from Calculator Phone vesion007
 
Kama hamjawahi kuhesabiwa si wao wamehesabu ebooo.

Wapinge basi kwa takwimu.

Nchi hii HAINA DINI ni ya ma kaffirriiii sheikh.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuna wanaume vilema asilimia 95 % Tanzania.
vipi unaweza kupinga hii kwa takwimu.
Kutokuwa na takwimu hakuumanishi kila uambiwacho ni kweli ndo maana kuna tofauti ya MBUZI NA BINAADAMU.
Ni akili za mwanadaamu kuweza kujua UONGO WA KIPUMBAVU.
 
Naelewa mkuu lakini
Inakataa nilishajaribu nikaweka unknown wamefuta jaribu wewe

Kingine mamalaka zetu ziko wapi kuona kama data za nchi zinawekwa za hovyo inatakiwa wakemee
Kwahiyo nawe ulitaka ukaongezee uongo wako maana je, unatakwimu sahihi
 
Kwahiyo nawe ulitaka ukaongezee uongo wako maana je, unatakwimu sahihi

Ndugu we ni mwanaJF long time kwanza soma elewa halafu ndo changia sio kukurupuka.

Kukurupuka waachie waliojiunga humu kipindi cha Vi- Wonder
 
Sensa ya kitu chochote husaidia gvt husika kupeleka huduma za jamii
Mfano sensa ya mifugo husaidia kufaham wapi kuna mifugo mingi na ni huduma zipi hazipo ili wapelekewe kulinga na hitajio la mahali
Sensa ya watu na makazi kadhali husaidia kufahamu idadi yao na ni huduma gani za kijamii hawana wapelekewe
Kwa idadi ya kidini wapi ni wengi wapi si wengi mfano ikijulikana kuwa waislamu ni wengi hii inaweza kurahisisha huduma zao kwa mujibu wa dini yao kadhalika kwa wakristo.
Na hii tusidanganyane hizi ni propaganda tu kuwa waislamu ni wachache ili huduma za kikristo zisiwe tabu kupitishwa.
Kama vipi gvt imalize utata kufanya sensa hii
Hii ina umuhimu mkubwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama wao wanataka uongo na kuzuia UKWELI kosa la nani,

Wao wamechukua kutoka CIA, wakati CIA inasifika kwa uongo tena mwingine ambao hauna hata mantiki,

Na nimewaambia mbona article ya Kenya hamuangilii huko hawajeka statistis za Dini wameweka za Makabila.

Always wao wanatafuta wanachihisi kinaweza kuwa kibaya kuwapumbaza watu.

Kingine wikipedia hao hao mbona takwimu za USA hawajatoa CIA, kwa sababu wananchi wao hawaamini CIA sana.

Na kuhusu CIA kuwa waongo anayekataa link ziko nyuma nilishazirusha na siyo lazma link zangu ukitafuta utapata uongo wa CIA
Haya maelezo yako sio ya kweli.Ziko nchi nyingi tu zimewekwa taarifa za asilimia za wananchi kwa dini.Hata marekani yenyewe taarifa za dini na jamii zilizoko wameweka.sasa nao tuseme wameweka ili kuchochea nini.Kwaiyo kama tanzania kupata takwimu za makabila ni ngumu kuliko za dini kwanini wasitumie hizo.Na wakati huo huo inajulikana kupata takwimu za makabila kenya ni rahisi kuliko dini au kinyume chake pia kwa nchi nyingine.kwaiyo usidhani labda hiz takwimu niza tanzania na kenya tu.Ni mambo ya dunia nzima.
 
Haya maelezo yako sio ya kweli.Ziko nchi nyingi tu zimewekwa taarifa za asilimia za wananchi kwa dini.Hata marekani yenyewe taarifa za dini na jamii zilizoko wameweka.sasa nao tuseme wameweka ili kuchochea nini.Kwaiyo kama tanzania kupata takwimu za makabila ni ngumu kuliko za dini kwanini wasitumie hizo.Na wakati huo huo inajulikana kupata takwimu za makabila kenya ni rahisi kuliko dini au kinyume chake pia kwa nchi nyingine.kwaiyo usidhani labda hiz takwimu niza tanzania na kenya tu.Ni mambo ya dunia nzima.

Ndugu unakubali kwamba CIA HUWA NI WAONGO!?
 
Back
Top Bottom