Uongo wa TANESCO mwisho leo - September 14, 2015

Uongo wa TANESCO mwisho leo - September 14, 2015

Kanywe sumu wewe au kama vipi hamia nchi jirani tuachie nchi yetu na amani yetu, sisi hatuhitaji maneno yenu hapa. HAPA NI KAZI TU MTAISOMA NAMBA MWAKA HUUU.

Heri wafu waliolala mauti kuliko pumbavu linaloishi kwa hasara duniani.
 
Katika mashirika mabovu na yanayohitaji reformation, TANESCO ni mojawapo. Ni nchi gani umeme unakatwa 12hrs kila siku?

Kwa kweli administration ijayo ifanyie kazi mapungufu makubwa yaliyopo ndani ya hilo shirika.
Siamini kuwa kila siku kunakuwabna hitilafu tu, au miundombinu mibovu.

Hapa kuna wasimamizi wabovu, watendaji wabovu na viongozi wa nchi ni wabovu sana...
 
Kanywe sumu wewe au kama vipi hamia nchi jirani tuachie nchi yetu na amani yetu, sisi hatuhitaji maneno yenu hapa. HAPA NI KAZI TU MTAISOMA NAMBA MWAKA HUUU.

Kazi gani hiyo aisee; mngekuwa wachapa kazi si mngeshapewa uwaziri mkuu kabla ya hao walioondoka?
 
Serikali ya watu wasiowajibika, ingekuwa nchi za wenzetu waziri udanganye wananchi ni siku nyingi umewajibika tena mwenyewe. Lakini kwetu anaongea huku anatabasamu hana hata wasiwasi sababu kwake umeme upo twente fo awaz. Anastandby generator la haja ...wanaahidi mamabo kisiasa tu wanajua hakuna tatizo.
Hivi ni lini mwisho wa baraza la mawaziri au halina mwisho hadi uchaguzi ufanyike?
 
Huku kwetu toka watangaze mwisho wa mgao ndo imekuwa balaa zaidi, wanakata kama hawana akili nzuri!
 
Pamoja Na ahadi zote Na pesa nyingi sana serekali imetumia ambazo ni kodi zetu Na mikopo mkubwa tutakayolipa imeshindwa kutupa Umeme, hakuna kazi wala biashara inayoendelea Kwa sasa, Leo ni tar 23/9/2015 hakuna Umeme , ulikatika tar22 asubuhi, Leo ni tar 23 usiku hakuna, ccm itaona hasira za watanzania tar25 October 2015.
 
Jitu Limeingia madarakani 2005 mpka linatoka 2015 halijaweza kutatua hata asilimia 1 ya tatzo la umeme..
Alafu utaliona jukwaani "nimefanya mambo mengi" huku linachekacheka..

Hii nchi ngumu hii,bora ningezaliwa ethiopia..
 
Toka Jana SAA kumi usiky had saa Tatu usiku ndo wanarudisha umeme hiyo mitambo inatengenezwa usiku wa manane au? Tanesco mnatuona ss n wajinga sana
 
Kwa huu mgao watakao ipigia CCM kura inabidi wakapimwe akili, hapa nlipo nimefunga rasimi biashara yangu baada ya kuendesha kwa hasara kwa miezi 3 mfululizo mgao ni mkari sana na sijawahi shuhudia mgao wa aina hii, lawama zote ziwaendee CCM.
 
Eti wanasema wanajaribu mitambo ya GAS uongo tu pesa yote imepelekwa kwenye Campain, TANESCO wako hoi(nukuu ya Mbowe) ni mgao kwa kwenda mbele walimsakama Prof Muhongo kwa hila tu sasa tutamkumbuka maana alikuwa amedhibit wizi sasa limebaki la manyani, Watz tutegemee GIZA TOTOROO la kufa mtu hadi hapo atakapochaguliwa kiongozi mwenye machungu na rasilimali za hii nchi,NI WIZI WIZI WIZI WIZI WIZI WIZI kila mahali hadi kuchapisha mabango ya campain 1.7b imeondoka (kambi ya wezi hakuna wa kukemea mwenzie)
 
Washanzi kweli kweli walitudanganya kuwa ni gas kumbe ni mgao !!
 
Malofa Ndio sasa Tunajuta na Upumbafuuuu wetu..Nchi Ipo gizani na Ipo Mfilisi..

Daaah watanikoma 25/10..Mbona Muda Haufiki.
 
Ikumbukwe kuwa maeneo mengi ya nchi hii bado kuna mgao wa umeme unaendelea wakati hawa jamaa walisema watakapoanza kutumia gesi kuzalisha umeme mgao itabaki kuwa historia!
Kwa huku kahama mgao ni kawaida umeme ukiwaka siku moja kesho yake hakuna!
Sasa juzi jumatano umeme haukuwepo, jana alhamisi umeme uliwaka ina maana leo ni zamu ya kukatwa umeme siku nzima
lakini cha ajabu asubuhi walikata kama dk 10 then wakawasha kumbe eti kwa sababu leo kuna mkutano wa kampeni wa mgombea urais ccm ambao ulikuwa ufanyike jana wakaahirisha sababu ya sikukuu!
Ieleweke kuwa siku lowassa alipokuja kahama umeme ulikatwa siku nzima ingawa haikuwa siku ya mgao wa umeme kwa eneo hili!
Kwa hali hii nimeamini kweli tanesco mnatumika kisiasa na ikiwa mgombea wa chama cha upinzani anakuja siku hiyo hata iweje lazima mkate umeme ila akija wa ccm umeme haukatwi eneo hilo hata iwe siku ya mgao!.
...endeleeni kutumiwa hivyo ila mwisho wa yote umekaribia!
 
Back
Top Bottom