Uongo wa Mwanamke wa Daraja la Sarenda.

pole sana kiongozi, jaribu kumpa mistari ya bible kidogo kabla ya kwenda kulala inaweza ikamfanya asipate ndoto za ajabu

Yaani huu uvumi,sijui uzushi,ulianza humu humu kidogo kidogo,yaani na watu mkauchekelea tu kwa sababu mleta maada alisema kausikia sijui kanisani au sijui alikua natoka kanisania Azania front na ujinga mwengine mwingi,
Oneni sasa madhala yake,tuweni waangalifu na yale tuyaletayo humu,hii Jf inasomwa na watu wengi
 
Amekuwa psychologically affected.
mimi na mama yake tumekaa chini na kumueleza sana kuwa huo ni uvumi na uongo,
tumeongea nae kwa upendo huku tukiwa tumempeleka sehemu nzuri iliyotulia.
bado swala hilo linamtatiza sana, ndio maana mara kwa mara amekuwa akipiga kelele usiku.
jumatatu nataka nimpeleke Muhimbili.

Huwezi kufanikiwa kumshauri kwa kutaka kumuaminisha kuwa tukio lile si la kweli hata kama utatumia upendo kiasi gani.

Why m i saying this? Kwa sababu lile ni tukio la kweli lililotokea na yule mwanamke kweli kakutwa baadaye uchi. Gari pia ilikuwa pale mpaka jioni na watu waliiona.

Unajua watoto sio fools kama tunavyowafikiria. Because of their angelic nature and an eager to learn brain the event at Salendar is a scientific possibility na yeye kama mtoto anaamini hivyo.

Umesema mtoto wako anasoma Olympio so lazima utakuwa unajiweza. Kama unajiweza lazima utakuwa unamruhusu mtoto wako kutazama katuni. Matukio ya aina hii ya kuweza kutoweka na kupaa kwa watu yako mangapi katika katuni za wazungu? Mbona hujawahi kumwambia kuwa ni ya uongo? Inakuwa tu la uongo kama likifanyika Daraja la Salendar?

Kwa maoni yangu tukio hili halina tofauti na POPOBAWA, JINI MAHABA au CHUMA ULETE (kama hufahamu style hizi uliza). Yule ombaomba ametumia innovation kidogo tu kutoka kwenye technique ambayo tayari inaexist in the world.
 
Uvumi wa mwanamke aliyeota manyoya na kisha kupotea umeleta athari nyingi sana.
miongoni mwa athari hizo ni kwamba wale watoaji sadaka kwa ombaomba wa maeneo ya daraja hilo na ombaomba wengine waliozagaa kwenye mitaa mingi ya jiji hili wamekuwa wazito kutoa hizo sadaka na kupelekea kipato cha maomba omba kupungua.
Mwanangu anayesoma Olympio amekuwa akiweweseka usiku kwa kuongea maneno yasiyoeleweka. Ukimwamsha na kumuuliza alikuwa anaota nini, anakwambia kuwa ameota konda kamteremsha Sarenda darajani halafu kakutana na mtu mwenye manyoya ya paka kampeleka kuzimuni.
Mwanangu amekuwa akikosa raha na amekuwa mwingi wa mawazo, kula yake imekuwa ya taabu na hana raha kabisa
.

Du. Na wewe umeanza uongo!!!!!!!!!!!!!
 
funika kwa damu ya yesu, yote hayatakupata
Usikute na huyu mtoto anashida ya kuvamiwa silently. Niliwahi kupata kesi ya dada mmoja Mtwara ambaye alikuwa akiona mambo kama haya kwenye ndoto kumbe yalikuwa ni ya kweli.
Ilikuja bainika baadaye kuwa amevamiwa na majini yale yale aliyokuwa akiyaona katika ndoto.
Tulimfunika kwa damu ya Yesu kama unavyosema na alikuwa huru kutoka katika vifungo hivyo. Sasa yuko huru kwa jina na damu ya Yesu.
Wewe Kiranja hiyo ndio itamsaidia na si Muhimbili. Kuna mambo Muhimbili watakuzungusha tu na mwisho watakwambia amepata shida ya msongo wa akili.
 
pole sana kiongozi, jaribu kumpa mistari ya bible kidogo kabla ya kwenda kulala inaweza ikamfanya asipate ndoto za ajabu

Yaani hapo ndio utakuwa umeharibu kabisa. Ndani ya Bible pia kuna matukio ya kupaa na kutoweka ya watu wengi sana na ambayo siku zote tunamwambia mtoto kuwa its possible. Wachache katika biblia waliopaa na kutoweka kwa staili ya kisalenda salenda ni Yesu, Elijah (Wafalme 2 Sura ya 2 mstari 1-12), Enock (mwanzo 6: 1- 4), Malaika anayeruka (ufunuo 8:13).

kwa hiyo tutafute namna nzuri ya kutoa maelezo bila ya kuwachanganya watoto.
 
hivi huyo mama bado kayeyuka?

Hapana alishapatikana akiwa uchi wa mnyama na watu wakiwa wameshammega. Hii dunia kuna watu wana hamu tofauti na namna tofauti za kupata ngono. Hii stlyle ya huyu ombaomba ni kali na kama mtu ukiijulia hutapata tabu ya kutongoza.
 
Usikute na huyu mtoto anashida ya kuvamiwa silently. Niliwahi kupata kesi ya dada mmoja Mtwara ambaye alikuwa akiona mambo kama haya kwenye ndoto kumbe yalikuwa ni ya kweli.
Ilikuja bainika baadaye kuwa amevamiwa na majini yale yale aliyokuwa akiyaona katika ndoto.
Tulimfunika kwa damu ya Yesu kama unavyosema na alikuwa huru kutoka katika vifungo hivyo. Sasa yuko huru kwa jina na damu ya Yesu.
Wewe Kiranja hiyo ndio itamsaidia na si Muhimbili. Kuna mambo Muhimbili watakuzungusha tu na mwisho watakwambia amepata shida ya msongo wa akili.

Mkuu,

mimi nadhani hili swala ni uzushi mtupu,lilianza humu kama mzaha tu,na muanzailishi tunamjua wote labda nadhani kulikua na maslahi binafsi na matokea ya uzushi huu au kwa kundi fulani la watu ambao watanufaika ama wameshanufaika na uzushi huu.
 
Ila lazima pia unapomfunika huyu mtoto umkumbushe pia kuwa Yesu naye alipaa kisalenda salenda. (sitaki kukashifu dini lakini nataka tufikiri zaidi).
 
Ukweli wale Omba omba huwa waanikwaza sana. huwa kila siku najiuliza inawa kweli hawana hata ndugu wa mbali ambao ana uwezo kidogo kuwasaidia? sisi wengine mbona tuna ndugu huko vijijini mbao wengine ni wazee sana na wengine hawajiwezi, tunajitahidi kuwasaidia? ukweli wanakera sana. Natamani sana siku niamke nisione hata ombaomba mmoja
Nilikuwa nina moyo sana wa kuwasaidia Ombaomba wa hapa dar. Nilikuwa ninachenji 10000 kwa 500 kila mwisho wa mwezi, kila ninapokutana nao nawapa. Moyo uliisha nilipohamishiwa Dodoma. Kule wengi ni wasanii, hawataki kufanya kazi, wanaweka gundi machoni, wengine wanajivalisha miti miguuni waonekane ni vilema mradi tu waombe hela. Tangu nihamie Dodoma ninamsaidia mtu ambaye ukimtazama tu utajua kuwa ni mhitaji lakini wengine hawa.... Mungu anisamehe
 
Amekuwa psychologically affected.
mimi na mama yake tumekaa chini na kumueleza sana kuwa huo ni uvumi na uongo,
tumeongea nae kwa upendo huku tukiwa tumempeleka sehemu nzuri iliyotulia.
bado swala hilo linamtatiza sana, ndio maana mara kwa mara amekuwa akipiga kelele usiku.
jumatatu nataka nimpeleke Muhimbili.

kiranja dont even try to go there! wanaweza wakaanza kum-treat mtoto kama ana tatizo la akili wakati ukweli hana tatizo na hiyo itazidi kumchanganya. kama wengine walivyoshauri jaribu kumpa ushauri na kumwambia kuwa hiyo habari si kweli, na ikiwezekana muhusishe mwalimu wake, ili awatangazie pia darasani kwamba hiyo habari ni uvumi hakuna kitu kamahicho, na pia marafiki zake wanaweza kumsaidia kumtoa hofu kuwa ni uongo. Pole sana.

Ila kwa kweli na mie nilikuwa maarufu wa kufungua kioo kutoa pesa nadhani pamoja na kutokuamini lakini nimepunguza mtindo huo, ukweli ukipeleka sadaka kanisani wakati mwingine matumizi yake yanakuwa nje ya yale tunayotarajia thats why watu wengine wameamua kutoa saadaka zao kwa walengwa moja kwa moja
 
FL,
Wewe kama wewe hautaweza kuwasaidia, ombaomba ni wengi sana tukiacha hawa waliopo Dar na mikoa mingine wapo ni wengi tu. Hapa ndio tujifunze kuwa serikali yetu haifanyi vizuri kuleta maisha bora kwa kila MTz. Kuna Idara ambayo ipo kwa kazi hiyo (Social Welfare Department) lakini Idara hii ni aibu tu, Serikali imeisahau kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! ukienda kwenye ofisi za Idara hiyo unaweza kulia, kuna foleni kubwa sana ya watu wenye matatizo mbalimbali ya kijamii wanaohitaji msaada lakini uwezo wa Idara hiyo kuhimili matatizo ni mdogo mno. Ukienda kwenye ofisi hizo utakuta kuna wenye matatizo kama ya Mke kutelekezwa yeye na watoto, Ugomvi ndani ya ndoa, watoto waliookotwa mitaani au kwenye mitalo, Ombaomba wakitaka kusaidiwa,akina mama wanaodai matunzo kutoka kwa mabwana au waume zao, machangudoa wanaohitaji mbadala wa kazi zao na mengine mengi saaaaaaaaaaana. Mimi natamani Idara ile iwezeshwe ili hayo maisha bira kwa kila mtanzania yaonekane
Fugwe hii alvatar yako inaonyesha kama vile uliwahi kusoma Tumaini University Iringa
 
Nashangaa utendaji wa maaskari wetu.Ukisoma sheria ya makosa ya jinai Penal Code Cap 16,RE 2002,iko wazi na inapiga marufuku suala la kuzurura na kuombaomba,sema tu sheria zetu zimekuwa ni kama mtaji lakini utekelezaji haupo.Makamba enzi zake alijitahidi.
 
Enzi ZA MWALIMU UZEMBE NA UZURURAJI LILIKUWA NI KOSA KUBWA.
UKIKAMATWA UNAZURURA NI JELA.
 
Enzi ZA MWALIMU UZEMBE NA UZURURAJI LILIKUWA NI KOSA KUBWA.
UKIKAMATWA UNAZURURA NI JELA.
nadhani kuna baadhi ya makabila (am sorry to say that) ambao umasikini au kuwa ombaomba kwao ni ufahari!!!! labda nitoe mfano, sijawahi kusikia /kumkuta ombaomba wa kabila kama mchaga, mhaya mnyakyusa etc wengi wao utasikia ni wagogo, wazaramo, wanyamwezi etc sasa sijui tatizo ni nini??? na pia kuna ombaomba wale ambao ni walemavu(at least hao unaweza ukaelewa sababu ya wao kuomba) ingawa pia wanaweza kuwa na familia ambazo zinawaangalia, wazee (hawa wanapaswa kutunzwa na jamaa/family zao) watoto (hawa wanapaswa kukamatwa na kurejeshwa makwao wakasome kundi hili linanikera sana) wanawake na wanaume wenye nguvu zao ila wameamua kuomba tu (hawa wanatakiwa kukamatwa, kutandikwa viboko llukiki na kutupwa gerezani ikibidi). Ila kuna aina mpya ya ombaomba ambayo inanikereketa - hawa wanaoomba siku ya IJUMAA kwenye maduka,majumba ya ibada hasa misikitini/jamatini na kwenye maeneo ya makaburi - hawa hata siju niwaweke fungu gani - inakera na ni aibu sana!!!!!
 
Labour camps zinahitajika. Too many people still able to a certain extent of toiling for a living, living off others. I suppose the same can apply to a vast majority ya watanzania. Bloody rent seekers
 
hivi wale ombaomba
1.ni mataahira?
2.hawana wazazi?
3.kwa nini wasipelekwe kwenye vituo vya kulelea watoto?

Kaka wale hawaki, kwani huko hawawezi kunywa bia na nyama choma. Hawa jamaa ni miradi ya watu. Kuna watu wanabeba kila siku asubuhi na kuwarudisha nyumbani. Ukitaka kujua hilo wewe jaribu kufanya kama unataka kumnyang'anya hela uliyompatia kwa nguvu uone utakavyo shambuliwa.

Nafikiri hili suala lilitakiwa kuwa chini ya ustawi wa jamii lakini ndiyo hivyo ufisadi kila mahala.
 
Mkuu,

mimi nadhani hili swala ni uzushi mtupu,lilianza humu kama mzaha tu,na muanzailishi tunamjua wote labda nadhani kulikua na maslahi binafsi na matokea ya uzushi huu au kwa kundi fulani la watu ambao watanufaika ama wameshanufaika na uzushi huu.
Uzushi wapi?
Maana hili halikuanzia hapa JF kumbuka limeanzia mtaani hukohuko kabla ya kuja JF.
Unadhanije kwamba ni uzushi?
kwani nini uanadhani haiwezi kuwa kweli?
 
Back
Top Bottom