Uoga wa Serikali/CCM

Uoga wa Serikali/CCM

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,070
Reaction score
136,458
Ni mara kadhaa sasa nimeona na kusikia watu wakisema kuwa eti serikali inaogopa.

Kwamba inaogopa maandamano yanayopangwa kufanyika tarehe 26 mwezi Aprili.

Watu wasemao hivyo wanasema hivyo kwa sababu wamejiaminisha kuwa kama serikali ingekuwa haiyaogopi hayo maandamano basi baadhi ya viongozi wasingeyazungumzia hata kidogo.

Si ajabu hata hapa atajitokeza mtu atayesema kuwa hata mimi nayaogopa hayo maandamano na ndo maana nimeanzisha tena uzi unaoyahusu.

Sasa jana rais Magufuli naye kazungumzia watu kuandamana. Na si mara yake ya kwanza kufanya hivyo. Keshafanya hivyo mara kadhaa huko nyuma.

Magufuli kutaja neno ‘maandamano’ hiyo jana imekuwa nongwa. Watu wanataka kutuaminisha kwamba hayo maneno ya mitandaoni huko kuhusu hayo maandamano yanamnyima raha na usingizi rais kwa sababu mpaka yeye kayazungumzia hiyo jana.

Mimi sidhani kama serikali inaogopa. Ninachokiona ni serikali yenye watu wanaojua na kutambua kinachozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii. Kujua na kutambua huko si uoga. Si kuogopa.

Kuogopa ni pale ambapo wale waliokuwa wanapiga sana kelele za maandamano kutokujitokeza na kuandamana siku ambayo walikuwa wamepanga kuandamana. Huo ndo uoga na huko ndo kuogopa.

Maana tayari wameshaambiwa ole wao waandamane. Wataenda kusimulia yatayowapata. Sasa siku ya siku ikifika na hakuna anayeingia barabarani, huko ndo kuogopa.

Lakini mtu kusema kuwa kasikia kuna watu wamepanga kuandamana au Ngabu kuja kuanzisha nyuzi hapa kuhusu hayo maandamano, sioni uoga hapo.

Kwa hiyo, mimi nadhani na naamini kuwa wote wasemao kuwa serikali inaogopa wanasema hivyo kujipa faraja tu.

Wanajiaminisha kuwa serikali inaogopa ili wajisikie vizuri tu. Wajione na wao kelele zao dhidi ya serikali zina athari ingawa kiuhalisia sivyo hivyo.
 
..kinachonishangaza ni lugha ya CHUKI, VITISHO, na UKATILI inayotumiwa na viongozi.

..inawezekana viongozi hawaogopi maandamano, lakini lugha wanazotumia zinaacha maswali mengi na kusababisha wananchi watoe kila aina ya tafsiri ikiwemo KUOGOPA maandamano.
 
..kinachonishangaza ni lugha ya CHUKI, VITISHO, na UKATILI inayotumiwa na viongozi.

..inawezekana viongozi hawaogopi maandamano, lakini lugha wanazotumia zinaacha maswali mengi na kusababisha wananchi watoe kila aina ya tafsiri ikiwemo KUOGOPA maandamano.

Hapo kwenye lugha naweza kubaliana nawe.
 
Sijaelewa hata upuuzi unaoongelea hapo. Hebu nitumie summery kwa hi no +25526042018
 
Tokea uweke akili kando unapost vituko na kujihami tu. Hukuwa hivi mkuu.
 
Mimi sielewi kwanini kuna promo sana ya haya maandamano kutoka kwa wasiyoyataka kuliko Ilivyo kwa wanayoyataka. Sijaona nyuzi zinaosema tutaandamana kwa wingi kama ninavyoona za kuzuia maandamano.
 
Back
Top Bottom