Unyonyeshaji bora wa maziwa ya mama na maziwa mbadala iwapo ni lazima

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
1602427980232.png

Mama ambaye amejifungua mara ya kwanza anaweza kuhitaji msaada katika kunyonyesha. Msaidie ili aweze kuwa mtulivu na makini kwa kazi hiyo. Msaidie kwa kutumia mablanketi na miito ili aweze kukaa wima na kujisikia vizuri. Waombe wanafamilia na wageni kumpa mama na mtoto faragha. Mtie moyo. Unyonyeshaji huwa rahisi kadri mama atakavyoendelea kunyonyesha na kupata uzoefu.

Maziwa ya mama ni bora kwa mtoto kuliko aina yoyote nyingine ya maziwa au mchanganyiko wowote wa vyakula vingine

Mwepushe mama maumivu kutokana na michubuko ya chuchu kwa kumweka katika mkao mzuri wa unyonyeshaji. Geuza mwili wote wa mtoto umwangalie mama ili shingo yake isipinde. Subiri hadi atapopanua mdomo wake. Halafu mweke kwenye ziwa. Chuchu na eneo jeusi linalozunguka linapaswa kufunikwa ndani ya mdomo wa mtoto.

Maziwa ya mwanzo ya mama ni sawa na kimiminika cha dhahabu

Maziwa ya mwanzo hutoka katika kiwango kidogo, lakini kiwango hicho ni sahihi kwa mtoto ambaye ndiyo amezaliwa. (Tumbo la mtoto ambaye ndiyo amezaliwa hubeba kiasi cha vijiko vya chai vichache tu vya maziwa kwa wakati.) Maziwa ya kwanza yananata na huonekana ya njano njano. Lakini ingawa huonekana tofauti, ndiyo chakula sahihi kwa mtoto ambaye amezaliwa . Maziwa hayo yana virutubishi muhimu vilivyotengenezwa na mwili wa mama yake kwa ajili ya kumkinga mtoto dhidi ya maambukizi . Usimwage au kupoteza maziwa ya kwanza: ni muhimu kwa mtoto kuliko dawa yoyote ile. Unyonyeshaji ndani ya siku 2 za mwanzo ni muhimu kwa sababu husaidia kufungulia maziwa yaliyokamaa ambayo mama huanza kuzalisha ndani ya siku 3 baada ya kujifungua. Kadri mtoto anavyonyonya ndivyo na wingi wa maziwa ambayo mama yake atazalisha.

Je mtoto anapata maziwa ya kutosha?

Usiruhusu mtu yoyote akwambie kuwa huwezi kuzalisha maziwa ya kumtosha mtoto wako, hasa katika siku chache za mwanzo wakati mwili wako ndiyo unaanza kuzalisha maziwa.

Kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa watu wengine na kutojiamini, akina mama( au mabibi, mashangazi au wakunga ambao wanasaidia kutoa msaada) huanza kuwalisha watoto ambao ndiyo wamezaliwa au watoto wachanga maziwa ya kopo, au uji, au vyakula vingine. Vyakula hivi vya ziada ni kupoteza fedha bure na pia vinaweza kusababisha mtoto kuharisha. Kuharisha husababisha mtoto kupoteza uzito na kuwa dhaifu.Na matumizi ya vyakula hivi husababisha mama atengeneze maziwa kidogo.Hivyo, hujikuta akiamini zaidi kwamba hawezi kumlisha mtoto wake vya kutosha kwa kutumia maziwa yake pekee. Kama wewe ni mfanyakazi wa afya, unaweza kuzuia mduara huu wa matatizo makubwa ya afya kwa kuwaonyesha akinamama kuwa una imani na uwezo wao wa kuwanyonyesha watoto wao. Msaidie mama kumweka mtoto katika mkao mzuri wa kunyonya, lakini pia mpatie mama nafasi ya kujifunza yeye mwenyewe jinsi gani unyonyeshaji unamsaidia mtoto. Ongea naye vizuri, taratibu. Kuwa na subira.
Kutengeneza maziwa ya kutosha

Nyonyesha mara kwa mara. Kadri unavyonyonyesha, ndivyo utatengeneza maziwa zaidi.
Tumia vinywaji vya kutosha na kula zaidi. Mlishe mtoto wako kwa kujilisha mwenyewe.
Pumzika mara kwa mara.Iwapo baba na wanafamilia wengine watasaidia na kazi zingine za nyumbani, mama atamhudumia mtoto vizuri zaidi.

Kadri unavyonyonyesha mara nyingi ndivyo utakuwa na maziwa mengi zaidi.

Watoto wengi hupoteza uzito kidogo katika wiki yao ya kwanza. Hili ni jambo la kawaida. Lakini baada ya hapo, upunguaji uzito humaanisha mtoto hapati lishe yakutosha. Vilevile, watoto hawakojoi sana siku yao ya kwanza, lakini baada ya hapo wanapaswa kutoa mkojo kila baada ya saa chache. Iwapo mtoto hatakojoa sana baada ya siku 2, atakuwa hapati maziwa ya kutosha. Je, kama mtoto atakuwa ananyonya mara kwa mara lakini hakojoi au kuongezeka? Katika hali kama hiyo ambayo siyo ya kawaida, unaweza kuhitajika kutafuta maziwa mbadala. Usimpe sukari au maji ya mchele. Usimpe maziwa mbadala ya makopo isipokuwa kama utakuwa na uhakika wa kumpatia kiasi kilichopendekezwa (kuongeza maji husababisha mtoto kuharisha na kuugua). Na usitumie chupa: hazisafishiki kwa urahisi na hivyo hueneza vijidudu ambavyo husababisha mtoto kuharisha.

Maziwa mbadala yanaweza kutolewa iwapo mama atafariki au atatengana na mtoto wake, au kwa nadra sana iwapo atakuwa kweli hatengenezi maziwa ya kutosha. Unaweza kumuomba mama mwingine kumnyonyesha mtoto huyu. Lakini kwanza apate kipimo cha virusi vya UKIMWI kujua iwapo yu salama. Hii ni kwa sababu virusi vya UKIMWI vinaweza kuenezwa kwa mtoto kupitia unyonyeshaji. Njia nyingine ni kutumia maziwa ya wanyama, mfano maziwa ya ngo’mbe au mbuzi yakiandaliwa kama kwa vipimo a,bavyo wataalamu wa afya wataelekeza.

Kama unalazimika kwenda kazini au kumuacha mtoto nyuma kwa sababu yoyote ile, unaweza kujaribu kukamua maziwa yako ili utakapokuwa umeondoka mtu mwingine aweze kumpa mtoto maziwa hayo.

Nawa mikono yako vizuri na kusafisha chombo cka kukamulia. Kukamulia maziwa ya mama kwenye chombo. Kamata ziwa kwa vidole vyako na dole gumba likiwa pembeni mwa eneo jeusi linalozunguka chuchu. Kandamizia ziwa kwenye kifua chako. Halafu bonyeza vidole vyako pamoja ukiwa unalekea kwenye chuchu. Jisikie huru na fikiria kuhusu mtoto wako wakati unakamua maziwa hayo-hii itasaidia maziwa kutoka kwa urahisi. Maziwa ya mama yatabaki salama kwa saa 8 kama hakutakuwa na hali ya joto kali nje.

Maambukizi ya kuvu mdomoni

Tumia kitambaa kidogo kisafi kusambaza dawa ndani ya mdomo wa mtoto.

Mabaka meupe ulimini au ndani ya shavu na kero wakati wa kunyoya vinaweza kuwa dalili ya maambukizi ya kuvu mdomoni. Maambukizi hayo yanaweza kwenea hadi kwenye chuchu ya mama na kusababisha wekundu, mwasho, na maumivu.

Jaribu kusuuza chuchu na siki (vinegar), na baadaye kwa maji ya kawaida. Au kama huna siki, jitahidi tu kusafisha na kukausha chuchu yako kila baada ya kunyonyesha. Iwapo hii haitasaidia, paka dawa ya Jiivi kidogo kwenye chuchu mara 2 kwa siku 3. Pia paka Jiivi ndani ya mdomo wa mtoto mara moja kwa siku. (Kila kitu kitageuka kuwa na rangi ya zambarau lakini ni salama). Kama Jiivi haitasaidia, mpe mtoto dawa ya nistatini (nystatin).

Kama maambukizi ya kuvu yatakuwa yanapotea na kurudi, mtoto anaweza kuwa na tatizo lingine ambalo linadhoofisha kinga yake ya kupambana na maambukizi. Kwa mfano, watoto wachanga wenye VVU wanaweza kupatwa na kuvu mdomoni mara nyingi zaidi. Angalia VVU na UKIMWI.
Maumivu ya ziwa, uvimbe, kuziba, au maambukizi

Wakati mwingine maziwa yanaweza kuziba mrija (njia ndogo ndani ya ziwa ambazo husafirisha maziwa). Ziwa huanza kuvimba, hugeuka kuwa jekundu na kutoa maumivu. Mara baada ya hapo, maambukizi yanaweza kuanza.

Maswali mbalimbali kuhusu unyonyeshaji maziwa ya mama

Kumekuwa na hoja tofauti toka kwa watu mbalimbali juu ya unyonyeshaji. Binafsi sielewi wapi niangukie... Nikaona nawashirikishe ili kupata maoni yenu. Je, kunyonyesha hadharani [Breastfeeding in Public] ni kosa?

Wanaume mnasemaje? Kina dada/mama vipi mwasemaje?
----

Michango mbalimbali ya wadau
kwa kweli mie huwa hata muda wa kufikiria kuwa mtu ananiangalia huwa sina hasa huyu mwanagu mkubwa, aah namwachia ajinafasi popote pale, akisema tu mama nyonyo, namwambia jichukulie mwenyewe!

Ukisema tukiangaliwa unamaanisha wanawake wote au baadhi? Kama baadhi nitakubaliana na wewe kiasi fulani. Labda unawaangalia kwa macho mengine na wakishashtukia wanakuwa furious kwa sababu wakati wa kunyonyesha aina fulani ya feelings zinapungua. hivyo ukikodolea nyonyo yake huku unameza mate wanaanza kujisikia kichefuchefu na ndio inakuwa mwanzo wa kutolewa mimacho.
-----
Watu wazima wanakula hadharani na hakuna yeyote anayewazuia kufanya hivyo.

Vichanga navyo vina haki ya kula hadharani tukumbuke maziwa ya mama ni chakula kwao wakati wengine wana mawazo kwamba maziwa ya mama hayastahili kuonyeshwa hadharani kwa sababu ambazo hazina msingi inapokuja kwenye kunyonyesha watoto hadharani.

Kuna baadhi ya nchi wasichana kuanzia miaka 16 wako huru kutembea maziwa wazi lakini wakati huo huo akina mama wenye watoto hawaruhusiwi kunyonyesha hadharani!!!
-----
View attachment 349147

Watu wengine bana kama si matatizo ni nini sasa, yaani kitendo cha mama kutoa ziwa kumnyonyesha dogo wewe eti unalitamani khaa!! kama siyo ugonjwa basi una matatizo ya kisaikologia, waone madaktari haraka. Na nyie kina dada eti kutoa ziwa kumnyonyesha mtoto analia eti anawadhalilisha aisee!!!

Kina Mama, kina dada mtoto akililia nyonyo we mpe popote pale ulipo!! Tena ikiweziekana yatoe yote mawili ili dogo awe anachagua lenye maziwa mengi.
 
For real I dont have anything against our beloved mothers but it sucks and just makes me sick.

Utakuta mama ananyonyesha ukimwangalia(macho hayana pazia) ana throw such a disgusting look kama vile you asked her anyonyeshe.

I dont mean to offend anyone but just find better locations u breastfeed ila sio publicly. It's not right kabisa.
 
Watu wazima wanakula hadharani na hakuna yeyote anayewazuia kufanya hivyo.

Vichanga navyo vina haki ya kula hadharani tukumbuke maziwa ya mama ni chakula kwao wakati wengine wana mawazo kwamba maziwa ya mama hayastahili kuonyeshwa hadharani kwa sababu ambazo hazina msingi inapokuja kwenye kunyonyesha watoto hadharani.

Kuna baadhi ya nchi wasichana kuanzia miaka 16 wako huru kutembea maziwa wazi lakini wakati huo huo akina mama wenye watoto hawaruhusiwi kunyonyesha hadharani!!!!
 
... breastfeeding is not a mistake, hata ukifanya hivyo ndani ya ndege au kwenye submarine ni poa tu!!
 
... breastfeeding is not a mistake, hata ukifanya hivyo ndani ya ndege au kwenye submarine ni poa tu!!
Wee SteveD, my wife wako akiwa ananyonyesha kwenye basi na ndio mzao wake wa kwanza unajisikiaje? Think of it... Uh? Pains eh? Wambie ukweli kama inauma... Kama kweli haikuumi basi ni vema akaanza ku-practice kwa sasa :)
 
Breastfeeding in public is not an offense. I am a still breast feeding my boy, I hope it won't offend you if I do at your wedding reception;)
... wala usijali mama, miye nitakuwepo kukusaidia kumbeba mtoto ukiwa unam breastfeed!! ;)
 
Duh jamani kunyonyesha hadharani sio vibaya, but i wdnnt go unleashing my gals to everbody. So my suggestion kama ikiwezekana mama ajistiri, they call them nursing covers but u surely can improvise, nyumbani hasa kanga will be great, na kila mtu anayo ama???

pili, if its in avery busy place, it wd be good to move to a less busier area to avoid distractions and be more at ease, if you are tense maziwa yatagoma etc.

tatu, dont forget to wipe/clean tits before feeding.

fourth: this is the greatest way to establish a bond with your baby, so lets keep breastfeeding!!!!!
 
... wala usijali mama, miye nitakuwepo kukusaidia kumbeba mtoto ukiwa unam breastfeed!! ;)

Ha ha ha Steve...utamsaidia mama kumbeba mtoto wakati ananyonyesha..!!!!

Ukiona mtoto anakupiga mateke, hujue umekodolea hoteli yake kwa muda mrefu... Si unajua watoto nao wana wivu...lol
 
Duh jamani kunyonyesha hadharani sio vibaya, but i wdnnt go unleashing my gals to everbody. So my suggestion kama ikiwezekana mama ajistiri, they call them nursing covers but u surely can improvise, nyumbani hasa kanga will be great, na kila mtu anayo ama???

pili, if its in avery busy place, it wd be good to move to a less busier area to avoid distractions and be more at ease, if you are tense maziwa yatagoma etc.

tatu, dont forget to wipe/clean tits before feeding.

fourth: this is the greatest way to establish a bond with your baby, so lets keep breastfeeding!!!!!

...if you have got it, flaunt it!! -God given assets shouldn't go hidden!

...and it is right time to practice if you haven't so far, do you need help on this?!

...if you have got it, flaunt it!! -God given assets shouldn't go hidden!

...and it is right time to practice if you haven't so far, do you need help on this?!wewe SteveD, wakati wa kunyonyesha sio wakati wa kuflaunt your twins hadharani!!

flaunting floppy things around wdnt be fun!!!!!!LOL
 
Duh jamani kunyonyesha hadharani sio vibaya, but i wdnnt go unleashing my gals to everbody. So my suggestion kama ikiwezekana mama ajistiri, they call them nursing covers but u surely can improvise, nyumbani hasa kanga will be great, na kila mtu anayo ama???

pili, if its in avery busy place, it wd be good to move to a less busier area to avoid distractions and be more at ease, if you are tense maziwa yatagoma etc.

tatu, dont forget to wipe/clean tits before feeding.

fourth: this is the greatest way to establish a bond with your baby, so lets keep breastfeeding!!!!!

Shishi, kwa nini kichanga kijifiche wakati kinakata msosi? Imagine wewe unapita barabarani huku unakula labda muhindi wa kuchoma, karanga au ndizi halafu watu wakushinikize eti ujisitiri kwa sababu unakula hadharani, Utajisikiaje? Na una maoni gani kuhusiana na nchi ambazo wasichana na akina mama wanaruhusiwa kutembea maziwa wazi kabisa bila hata sidiria lakini akina mama hawaruhusiwi kunyonyesha hadharani?
 
Hiyo shughuli ya kujificha ili kunyonyesha si nitapitwa na mavituz harusini? Vinginevyo nisihudhurie kabisa; ila napenda sana nihudhurie, tafadhali.

Kama nyonyo ni ndefu kiasi kwamba inafika mgongoni, je ukimtupia hata ukiwa umembeba kuna ubaya wwt?
 
Breastfeeding in public is not an offense. I am a still breast feeding my boy, I hope it won't offend you if I do at your wedding reception;)

Tunarudi palepale yeah its not an offense lakini mbona mkiangaliwa (macho hayana pazia) mna throw very disgusting looks?
At least cover yourself with those nursing covers as suggested by one of the members.
 
Kama nyonyo ni ndefu kiasi kwamba inafika mgongoni, je ukimtupia hata ukiwa umembeba kuna ubaya wwt?

Tatizo unaweza kulitupa mgongoni ukafikiri mtoto atalidaka kumbe lifedhuli fulani limempiga kikumbo mtoto na kujipendelea lenyewe....
 
Tatizo unaweza kulitupa mgongoni ukafikiri mtoto atalidaka kumbe lifedhuli fulani limempiga kikumbo mtoto na kujipendelea lenyewe....

...QM, wakati unaandika hivi nauhakika ulinifikiria mimi... weee haya bana :( . Kamwe, nakuhakikishieni hapa kwa vile nimejitolea kumsaidia mama, miye sita - mid-air intercept hilo titi!!
 
Hiyo shughuli ya kujificha ili kunyonyesha si nitapitwa na mavituz harusini? Vinginevyo nisihudhurie kabisa; ila napenda sana nihudhurie, tafadhali.

Kama nyonyo ni ndefu kiasi kwamba inafika mgongoni, je ukimtupia hata ukiwa umembeba kuna ubaya wwt?

Mtupie mgongoni uone wenye kiu kweli wanalidaka na kulifyonza.
Hujawahi sikia mtu kabakwa kisa alikuwa ananyonyesha?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom