Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 233
- 563
Nakubaliana kabisa kuwa maziwa ya mama yanavirutubisho vyote anavyohitaji mtoto
Nakubaliana kabisa kuwa maziwa ya mama ni chakula bora na muhimu kwa mtoto mchanga na anatakiwa kunyonyeshwa hadi anapofikisha angalau miaka miwili
Nisichokielewa ni hii kampeni ya miaka ya hivi karibuni ya kuwahimiza kina Mama kutowapa watoto wao kitu chochote isipokuwa maziwa ya mama tu hadi atakapofikisha miezi sita
Kwa umri wetu wengi mlioko jukwaa hili hatukukumbana na hii kampeni kitu kinachomaanisha wazazi wetu walitulisha walivyoona vinafaa sisi kula hata kabla ya miezi sita na tulibaki salama
Hawa wataalamu wa afya wameona madhara gani tuliyoyapata sisi ambayo hawataki hawa watoto wetu wayapate?
Kwanini hii kampeni inahusu watoto wote bila kujali kwamba kila mtoto anazaliwa na utofauti? Ni kweli kuwa mtoto anayezaliwa Kigoma vijijini huko na mama aliyekuwa anashinda shambani toka mimba inatungwa atakuwa sawa na mtoto anayezaliwa Masaki na mama aliyekuwa anashinda kwenye kiyoyozi na kutembelea gari toka mimba inatungwa?
Hawa watoto wanaozaliwa mazingira tofaufi kwanini wapangiwe matumizi sawa ya chakula hadi watakapofikisha miezi sita?
Je, waliofanya tafiti na kuja na haya mapendekezo walifanya tafiti zao Tanzania au yalikuja maandiko tu kutoka kwa wadhamini? Kama yalikuja maandiko, tuna uhakika gani kama mazingira waliyofanyia tafiti zao yanaendana na mazingira yetu?
Karibu tujadili kwa pamoja