Unyonge wa Walimu unaanzia mbali. Inahitaji muda na jitihada za dhati kuumaliza

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,223
22,299
Ninaandika kwa masikitiko makubwa sana. Siku hizi imekuwa kawaida unatazama TV mara unaona muokota makopo akijisifia kuwa kazi yake inamlipa kuliko hata ya ualimu. Hujakaa vizuri unakuta mwenyekiti wa kijiji naye anawapa amri waalimu ili mradi tu mwalimu aonekane sio lolote. Unaingia FB unakuta mpuuzi Mpwayungu Village nae anaandika mambo ya kuwakandia waalimu. INASIKITISHA SANA.

Matukio ni mengi ya kuwadhalilisha waalimu yamesharipotiwa likiwemo lile la waalimu kuchapwa viboko na mkuu wa wilaya. Kimsingi waalimu wameonyesha unyonge wa hali ya juu kulinganisha na watu wa kada zingine. Mkuu wa wilaya hawezi thubutu kuwachapa viboko wahasibu, wanasheria, wahandisi au hata madereva. Nimekaa na kujiuliza sana kwanini waalimu wanakuwa wanyonge?

Sababu zipo ila nimegundua unyonge wa waalimu ni mchanganyiko wa sababu zinazoanzia mbali kabla hata mtu hajawa mwalimu. "UALIMU NI WITO" ni kauli nzuri ila nyuma ya pazia ni kauli inayomjaza unyonge mtu kabla hata ya kuomba kwenda kusomea ualimu. Yaani mtu kabla hata hajaomba kwenda kusomea ualimu anakuwa ashajua anaingia sehemu ambayo unatakiwa tu ujali wito na sio maslahi na haki zako zingine. Yaani unajitolea kuwa mshumaa kuteketea huku ukimulikia wengine. Namlaani aliyesambaza huo usemi wa ualimu ni wito.

Waalimu walioingia kwenye ualimu kwa kuipenda kazi ni wachache kuliko wale walioingia kwa sababu hawakufanya vizuri kwenye mitihani yao ya F4 & F6 na wale walioenda ualimu kwa unafuu wa kupata ajira. Mwaka 2006 nilibahatika kuwa miongoni mwa walioingia kwenye ualimu kupitia crash program Monduli TTC nikafanya kazi hadi 2007 kwahiyo ninachoandika nina ushahidi nacho wa kutosha. Pale Monduli tulikuwa na kocha wa kimataifa Ahmed Arajiga. Kama waalimu wanaingia kusomea ualimu wakiwa na unyonge kwamba wanaenda kwenye kazi ya wito bila kujali sana maslahi sasa wakiwa pia wameenda kwa sababu maksi zake hazikutosha kwenda fani zingine ndo inakuwa unyonge ×2. Nakumbuka wengi tulioingia kwa crash program hatukukaa kabisa mashuleni tulienda vyuoni na kusomea fani zingine kabisa.

Kundi linaloingia kwenye ualimu kwa unafuu wa kupata ajira nalo ni kubwa sana. Kimsingi ukipiga hesabu vizuri utaona waalimu wengi waliingia kwenye ualimu kwa kukosa nafasi ya kusomea fani zingine na uoga wa maisha. Mtu ana div One nzuri ya sayansi anakuwa na uoga akisoma fani nyingine atakosa kazi na kuamua kujitupia kwenye ualimu.

NINI KIFANYIKE? Binafsi naona kuanzia ngazi ya familia kuelimishana kuwa ualimu sio wito tu bali na maslahi pia. Waalimu waache unyonge na kujiona wanastahili kufakamia keki ya taifa kama watu wengine.
 
Back
Top Bottom