Walimu wa hesabu/hisabati

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,586
4,274
Kwa sababu ambazo sifaham, tangia miaka ya 1990, tumekuwa na tatizo kubwa la ukosefu wa waalimu wa hesabu.
Tatizo ni kubwa zaidi kwa shule za msingi za umma ambapo waalimu wenye vigezo vya kufundisha somo hilo pengine ni chini ya asilimia 10% ya mahitaji. Nafikiri tukiwa wakweli, matokeo tunayopata sasa kwa asilimia 90% yanasababishwa na ukosefu wa waalimu wa hesabu; Hivyo visababu vingine ni vya kuunga unga tu bila uhalisia......

Kwa uchapakazi wa Serikali iliyopo madarakani, na nia yake njema ya kuwasaidia watoto wa masikini;
Nafikiri ipo haja sasa ya kuja na mpango mkakati wa kurekebisha hali hiyo.

ANGALIZO; Hata tukipeleka waalimu wenye Diploma au Degree huko shule za msingi, kama kigezo cha kuwa na pass ya kueleweka ya hesabu hakita angaliwa, ufaulu wa somo la hesabu utaendelea kuwa mbaya!
 
_20231205_104349.JPG
 
Back
Top Bottom