Ungepewa nafasi uchague

Ungepewa nafasi uchague

Kuoa/kuolewa na mtu anaekupenda au unaempenda ungechagua nini?

Anaekupenda au unaempenda?
anayenipenda kwa sababu mtu anaweza kujifunza kumpenda mtu anaempenda hata kama mwanzoni mtu huyo alikuwa hapendwi na muhusika kuliko kuumiza kichwa na kupungua uzito ukitafakari kumpata mtu asiekupenda ila wewe kwake ndio mahaba niue.
 
hili swali kwa huu mfumo dume linawafaa zaidi wadada mi naona halinuhusu kwa sababu mi lazima nimpende mtu ndio nimuoe sasa sijui wadada wanaongoja kuolewa
 
ukiwa unampenda mtu hayo yote huna habari ayo unachowaza ni how you feel juu yake naamini ushapenda

lakini kusema umuache huyo mtu kwa sabbu kuna mtu anaekupenda na wewe umpendi kwa kweli ni kitendawili

ila umetoa sababu nzuri

Kwanza nikupongeze kwa mada nzuri! Kumbe ukiamua huwa unaweza kuja na mambo mazuri!
Pili uhalisia wa maisha ni kwamba akikubalia unayempenda maana yake ni kwamba na yeye amekupenda na si vinginevyo.
Kwa hiyo hakuna suala la yeye anakupenda na wewe haumpendi. Hapo hatuongelei mambo ya kizamani ya kulazimishwa na wazazi au mila za zamani za wahaya za kubeba msichana kwa nguvu!
Mara nyingine tena nampongeza masai dada katika ubora wake!
 
kuna mtu unampenda jamani you will risk everything just to have him hivi waweza acha hiyo na kuwa na mtu anaekupenda ??

Akikupenda utampenda tu, labda kama dhana ya kupendwa hatuifahamu vizuri? Kupenda sio kutamani! Kupenda ni kujitoa kwa ajili ya mwingine kwa gharama yoyote, upendo husamehe, huvumilia, huamini, hauhesabu mabaya!
Ni wasichana wachache sana hubahatika kupendwa kwa maana halisi ya kupendwa! Walio wengi hutumiwa tu kama vyombo vya kukidhi tamaa ya wanaume! na tamaa ni ya kitambo kidogo, tamaa ikitimizwa na wewe huna chako, kama si leo ni kesho!
Utajuaje anakupenda na sio anakutamani? Jibu ni rahisi, akikupenda atakuheshimu, hatataka ngono kabla ya ndoa! Akiomba tendo la ndoa kabla ya ndoa hakupendi huyo! anakutamani tu!
Anayekupenda atasubiri!
 
japo yeye ndo kaninunulia lakini hata kuangalia saa haangalii kwenye simu yangu hahaha😂😂😂😂😂

Badilishaneni simu kwa weekend nzima toka ijumaa jioni mpaka jumatatu asubuhi na umpe pass words zote! Hii inasaidia sana kuthibitishiana uaminifu! Ukipigiwa weka spika kama yuko karibu!
 
Kabisaaaa!! Wengi hukimbilia kwa wale tunaowapenda ndio maana nyuzi za kutendwa humu haziishi na vilio vya mapenzi rundoooo!! Tatizo unakuta anayekupenda hana vigezo unavyovipenda hata theluthi, kwahiyo hata kujifunza kumpenda inakuwa ngumuuuuu.

Kwa hiyo utamkubali asiyekupenda ili maadam tu ana vigezo?
 
japo yeye ndo kaninunulia lakini hata kuangalia saa haangalii kwenye simu yangu hahaha😂😂😂😂😂

Mwanamume akiiogopa simu ya mumewe au ya mchumba wake ni dalili tosha kuwa hamwamini mkewe hivyo anajilinda asipate ugonjwa wa moyo!

Dawa yake pekee ni kumpa simu yako kwa maneno mazuri kama vile "mpenzi simu yangu ni nzuri sana, kwa hiyo nakupa zawadi uitumie kwa siku nzima, utanipa kesho asubuhi! pass word (kama inayo ) ni hii! MTU akipiga nipokelee mwambie mwenye simu ametoka kidogo kama una ujumbe nipe nitamfikishia" Akikataa kuichukua mbembeleze mwambie "usiniumize kwa kukataa zawadi yangu"
Tatizo ni kwamba je ni wangapi walio waaminifu kiasi cha kufanya hivyo?
 
Back
Top Bottom