Ungependekeza Bilion 600 za Dreamliner zitumikee wapi?

Ungependekeza Bilion 600 za Dreamliner zitumikee wapi?

Mimi ningependekeza zinunue magari na vifaa vya zimamoto nchini kote kwa kadri itakavyowezekana. Ni ushenzi wa hali ya juu kwa jiji kama Dsm lenye watu takribani milioni 5 halafu lina fire station moja tu ambayo magari yake ni kama mnavyoyajua.
Mkoani Manyara gari la zimamoto lipo Babati ambapo ni umbali wa kama saa nzima kutoka mji mdogo wa Katesh ambao eti unategemea gari hilo hilo.
Wenzetu Uingereza sheria imetamka kwamba likitokea tukio la dharura la kuhitaji zimamoto, gari la wagonjwa au polisi basi wahusika wanapaswa kufika eneo la tukio ndani ya dakika 8, zikizidi hapo bila sababu ya msingi mtu anawajibishwa na kufikishwa mahakamani.
Sisi tulibugi step wapi?
 
No 4 umeongea la muhimu sana Mkuu.

Nilikuwa nacheki data za upatikanaji wa maji nchini kwenye mikoa mbalimbali..

Zaidi ya robo tatu ya Mkoa wote wa Tabora hawapati maji..

Na gharama zake zizikumbuki lakini nafikiri hazi zidi 100Bil.

Si bora kuwaondolea Tabora shida ya maji na sehemu nyingine za nchi...!!??

Huo m dreamliner nani ataupanda kuja kutalii hapa Tanzania... na asa ivi ndio tuna majanga ya ZIKA tena...shida tupu kwenye huo Utalii anaousema.

Maana alisema anataka ndege ya kuchukua watalii USA mpaka Tz.
Huyo MTU wenu mbona alikuwa huku huku kwa nyadhifa kubwa tu! Mbona muda wote huo hakumaliza hizo kero?? Acheni ujinga wenu na Siasa za kitoto!!
 
Ningependekeza inunuliwe ndege kuuuuubwa, isaidie kuleta watalii for direct flight na kuongeza mapato ya nchi yetu ili tuwekeze kwenye Huduma za maji, umeme, mikopo kwa vijana n.k.

Namaanisha kuwa kusudio la serikali ni sahihi.
 
Kuna wachumi na wataalam elekezi wengi humu
Kupanga ni kuchagua,tumechagua kufufua Shirika la ndege ili tuinue pato kutokana na utalii
Nyimbo za Maji,elimu na kilimo zinasikika sasa kwa ajili ya ndege tu,sijui zinawauma nini
 
Ningependekeza fedha bilioni 600 zitumike katika hili

1. Kuboresha miundombinu ya Dar kwa kujenga barabara za mwendokasi nyingine katika sehem zenye msongamano.

. AU
2. Ningetumia fedha hizo kukopesha vijana wenye mpango mkakati wa biashara kuweza kujiajiri wenyewe.

AU
3. Ningesambaza umeme katika sehem ambazo umeme haujafika

AU
4. Ningesambaza huduma za Maji katika sehem kame

. AU
5. Ningeimarisha shule za msingi kwa kukarabati miundombinu.

Wewe unapendekeza nini?
ziende katika kilimo na kuanzisha viwanda!
 
Ningependekeza inunuliwe ndege kuuuuubwa, isaidie kuleta watalii for direct flight na kuongeza mapato ya nchi yetu ili tuwekeze kwenye Huduma za maji, umeme, mikopo kwa vijana n.k.Namaanisha kuwa kusudio la serikali ni sahihi.

Na wasipokuja?
 
Zikajenge kiwanja cha bombardier Chato ili mtukufu aliyetukuka sana akienda mapumzikoni bombadier isije kukwama tena!
 
atupe vijana wa ccm tunao tetea serikali hata kama imekosea

maana tunapitia kipindi kigum saana, kwa group letu la whatsapp kila mtu analalamika pesa hamna
 
Ningependekeza inunuliwe ndege kuuuuubwa, isaidie kuleta watalii for direct flight na kuongeza mapato ya nchi yetu ili tuwekeze kwenye Huduma za maji, umeme, mikopo kwa vijana n.k.

Namaanisha kuwa kusudio la serikali ni sahihi.
UBARIKIWE SANA. ...serikali yetu ina watu makini...
 
Hivi kama Mkulu ndiye anayepanga bajeti almost yote ya nchi hii kuna haja gani ya kuwa na Bunge la Bajeti linalokaa zaidi ya miezi 2 kule Dodoma huku 'likatafuna' mabilioni ya shilingi wanazolipana posho?!

Tulijionea majuzi alipokwenda pale Ukonga Magereza akiahidi kuwapelekea bilioni 10!

Tulijionea mwezi June mwaka huu, Mkulu alipoenda kwa Mzee wa Upako akimuahidi kumtengenezea barabara ya lami toka barabara ya Mandela hadi kanisani kwake!

Na hivi sasa tumemsikia Mkuu akitamba kuwa tayari keshanunua ndege 6 za Bombardier na hiyo 'babu' kubwa ya Boeing Dreamliner ya bilioni 600!

Sasa kama bajeti yote ya nchi inapangwa na Mkuu, tuna haja gani ya kuendelea 'kuteketeza' mabilioni ya shilingi kuwalipa wabunge wakati bajeti yao haina maana tena?
Wabunge wote kimyaa...
Bunge butu
 
Mkuu wanakuja na za kukodi, matokeo yake wanapitia kwanza Kenya wanaacha fedha pale halafu ndio wanakuja Tanzania.
Mkuu soko la ndege unalijua vizuri?
Ndio maana nchi za kibeparu zimeachia wafanya biashara kufanya kazi hii.
Litatushinda, na wote tutashuhuduaa humu
 
Mkuu wanakuja na za kukodi, matokeo yake wanapitia kwanza Kenya wanaacha fedha pale halafu ndio wanakuja Tanzania.
Sio mbaya wakiacha hela kwa jirani na huku wakaleta pia, msiambukizwe kuwa na roho mbaya kiasi hicho.
 
Mimi pesa yote hyo ingeingizwa katika ujenzi wa maabara za kisasa katika shule zote za sekondari za kata.
 
Ageongeza tena 1 ziwe mbili
Ili huko mbele ya safari zikuze utalii
 
Dah...ipelekwe vijijini..ikalipwe ile 50m..watu wapige vyombo tu😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom