Ungependekeza Bilion 600 za Dreamliner zitumikee wapi?

Ungependekeza Bilion 600 za Dreamliner zitumikee wapi?

No 4 umeongea la muhimu sana Mkuu.

Nilikuwa nacheki data za upatikanaji wa maji nchini kwenye mikoa mbalimbali..

Zaidi ya robo tatu ya Mkoa wote wa Tabora hawapati maji..

Na gharama zake zizikumbuki lakini nafikiri hazi zidi 100Bil.

Si bora kuwaondolea Tabora shida ya maji na sehemu nyingine za nchi...!!??

Huo m dreamliner nani ataupanda kuja kutalii hapa Tanzania... na asa ivi ndio tuna majanga ya ZIKA tena...shida tupu kwenye huo Utalii anaousema.

Maana alisema anataka ndege ya kuchukua watalii USA mpaka Tz.
Unajuaje kama hawatakuja hao watalii umeongea nao? Hiyo zika itakuwa nchini milele kama ndiyo sababu ya watalii na wageni wengine kutokuja nchini?
 
Mkuu acha tu.
Ajira hakuna, tunaletewa mandege ya ajabu ajabu
je wakati ambao hatukuwa na ndege kulikuwa na ajira za kutosha tulinganishe? Au umeiona au kusikia nchi gani duniani yenye ndege au isiyo na ndege watu wake wote wanaostahili kuajiriwa wameajiriwa?
 
Hata ukipendekeza ni sawa unaoga kwenye tope

Mtu hasikii wala hashauriki hiyo midege ndio furaha yake
akikaa akisimama
akilala akiamka
akila akitembea
anawaza Dreamliner kama vile anaiona pale KIA
inapaa utamwambia eti kuna watz huku wanashida na maji!!??
Siku zote hawa watu ambao huwa wanajidai eti
katoka familia sijui ya mkulima huwa wanabadilika
na hawasaidii chochote.
ananunua ndege ambazo watanzania baadhi wenye maisha ya juu ndo watapanda
lakini si mtanzania wa maisha ya chini ambae hata panadol
inamshinda kununua,.

Hata hivyo hawa watanzania wa chini wakati mwingine
hawana akili anasumbuka dawa, maji shidah lakini
Ikifika wakati wa kampeni ndio utaona ujinga wake,
Na mimi nasema acha waisome namba.
Wewe Magu katununulie Dreamliner allah...!!!.
Unajuaje kama hashauriki? Unaweza kutoa ushauri alioukataa? Na je ushauri maana yake amri au hiyari ya mtu kuutumia ama la?
 
Hivi kama Mkulu ndiye anayepanga bajeti almost yote ya nchi hii kuna haja gani ya kuwa na Bunge la Bajeti linalokaa zaidi ya miezi 2 kule Dodoma huku 'likatafuna' mabilioni ya shilingi wanazolipana posho?!

Tulijionea majuzi alipokwenda pale Ukonga Magereza akiahidi kuwapelekea bilioni 10!

Tulijionea mwezi June mwaka huu, Mkulu alipoenda kwa Mzee wa Upako akimuahidi kumtengenezea barabara ya lami toka barabara ya Mandela hadi kanisani kwake!

Na hivi sasa tumemsikia Mkuu akitamba kuwa tayari keshanunua ndege 6 za Bombardier na hiyo 'babu' kubwa ya Boeing Dreamliner ya bilioni 600!

Sasa kama bajeti yote ya nchi inapangwa na Mkuu, tuna haja gani ya kuendelea 'kuteketeza' mabilioni ya shilingi kuwalipa wabunge wakati bajeti yao haina maana tena?
Ndege barabara ya mzee wa upako na pesa ya magereza ndiyo budget yote ya nchi?
 
Elimu, mikopo kwa wnafunzi na ada zifutwe kwa wote, halafu zingewekezwa kwenye tafiti mbalimbali za kisayansi.

Sasa naamini kwa pesa za mchezo namana hii Lowasa angetoa elimu bure hadi chuo kikuu
 
Pekekeen wanafunzi boom
Hali mbaya watu washa anza biashara isyo na matangazo
Kupanga ni kuchagua. Wameamua kufanya biashara hiyo isiyo na matangazo hata wakiwa na pesa ya kutosha watafanya tu kwa sab wamechagua.
 
Mimi ningependekeza zinunue magari na vifaa vya zimamoto nchini kote kwa kadri itakavyowezekana. Ni ushenzi wa hali ya juu kwa jiji kama Dsm lenye watu takribani milioni 5 halafu lina fire station moja tu ambayo magari yake ni kama mnavyoyajua.
Mkoani Manyara gari la zimamoto lipo Babati ambapo ni umbali wa kama saa nzima kutoka mji mdogo wa Katesh ambao eti unategemea gari hilo hilo.
Wenzetu Uingereza sheria imetamka kwamba likitokea tukio la dharura la kuhitaji zimamoto, gari la wagonjwa au polisi basi wahusika wanapaswa kufika eneo la tukio ndani ya dakika 8, zikizidi hapo bila sababu ya msingi mtu anawajibishwa na kufikishwa mahakamani.
Sisi tulibugi step wapi?
Hujaona magari ya washawasha hapa bongo yanazima moto?
 
Kuna wachumi na wataalam elekezi wengi humu
Kupanga ni kuchagua,tumechagua kufufua Shirika la ndege ili tuinue pato kutokana na utalii
Nyimbo za Maji,elimu na kilimo zinasikika sasa kwa ajili ya ndege tu,sijui zinawauma nini
Kweli kabisa na mbona wakati hakuna ndege hizo huduma za elimu maji na afya zilikuwa na ubora gani ulikilinganisha na sasa wakati ndege zimenunuliwa?
 
Yes, moto wa upinzani.
Sio moto wa upinzani mabweni yaliyoungua mtwara washawasha iliwahi kufika kabla ya zimamoto na tayari serikali imetoa circular magari ya washawasha kote nchini yazime moto
 
je wakati ambao hatukuwa na ndege kulikuwa na ajira za kutosha tulinganishe? Au umeiona au kusikia nchi gani duniani yenye ndege au isiyo na ndege watu wake wote wanaostahili kuajiriwa wameajiriwa?
Wanasema hakuna kuajiri kwakuwa serikali haina pesa.
Sasa pesa ndo zinafanya upuuzi km huo.
 
Hana pesa za kununua ndege ya billion 600. 600 billion ndilo pato letu halisi la mwezi kwa sasa. Hii ni ndoto yake ya kumtambia kagame.
 
Wanasema hakuna kuajiri kwakuwa serikali haina pesa.
Sasa pesa ndo zinafanya upuuzi km huo.
Nani alikuambia ajira imesitishwa kwa sab pesa hakuna? Ajira ilisimama kwa sab ya uhakiki na tayari watu 70000 wanaajiriwa mwakani fab ni idadi kubwa kuliko mwaka jana.
 
Nani alikuambia ajira imesitishwa kwa sab pesa hakuna? Ajira ilisimama kwa sab ya uhakiki na tayari watu 70000 wanaajiriwa mwakani fab ni idadi kubwa kuliko mwaka jana.
Porojo zile.
Pesa hakuna..
 
Ningewapeleka kurisit wenye vyeti feki, maana wengi wao wanajitambua

Ningewalipia mahari vijana wanaotaka kuoa zinazobaki tunawafanyia sendoff wote siku moja uwanja wa taifa.
 
Tatizo kubwa la watanzania walio wengi ni Maji, hayo mengine yatajihangaikia
 
Porojo zile.
Pesa hakuna..
Kwanini tuamini zile ni porojo bali za kwako sio porojo? Haingii akilini uhakiki unafanyika nchi nzima na unaonekana kwenye vyuo maofisi ya serikali hadi kwa wastaafu zoezi ambalo lina gharama kubwa. Je pesa za kutimizia porojo hizo kwa mujibu wako zimetoka wapi? Na kwanini wasitumie pesa za kufanyia porojo hizo kuajiri watu angalau wachache? Je hiyo ajira iliyotangazwa pesa zimetoka wapi au nazo ni porojo?
 
Kwanini tuamini zile ni porojo bali za kwako sio porojo? Haingii akilini uhakiki unafanyika nchi nzima na unaonekana kwenye vyuo maofisi ya serikali hadi kwa wastaafu zoezi ambalo lina gharama kubwa. Je pesa za kutimizia porojo hizo kwa mujibu wako zimetoka wapi? Na kwanini wasitumie pesa za kufanyia porojo hizo kuajiri watu angalau wachache? Je hiyo ajira iliyotangazwa pesa zimetoka wapi au nazo ni porojo?
Uhakiki gani unafanyika mwaka mzima?
Ulishaona wapi hii?
 
Back
Top Bottom