Ungependekeza Bilion 600 za Dreamliner zitumikee wapi?

Ungependekeza Bilion 600 za Dreamliner zitumikee wapi?

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
15,316
Reaction score
23,186
Ningependekeza fedha bilioni 600 zitumike katika hili

1. Kuboresha miundombinu ya Dar kwa kujenga barabara za mwendokasi nyingine katika sehem zenye msongamano.

. AU
2. Ningetumia fedha hizo kukopesha vijana wenye mpango mkakati wa biashara kuweza kujiajiri wenyewe.

AU
3. Ningesambaza umeme katika sehem ambazo umeme haujafika

AU
4. Ningesambaza huduma za Maji katika sehem kame

. AU
5. Ningeimarisha shule za msingi kwa kukarabati miundombinu.

Wewe unapendekeza nini?
 
No 4 umeongea la muhimu sana Mkuu.

Nilikuwa nacheki data za upatikanaji wa maji nchini kwenye mikoa mbalimbali..

Zaidi ya robo tatu ya Mkoa wote wa Tabora hawapati maji..

Na gharama zake zizikumbuki lakini nafikiri hazi zidi 100Bil.

Si bora kuwaondolea Tabora shida ya maji na sehemu nyingine za nchi...!!??

Huo m dreamliner nani ataupanda kuja kutalii hapa Tanzania... na asa ivi ndio tuna majanga ya ZIKA tena...shida tupu kwenye huo Utalii anaousema.

Maana alisema anataka ndege ya kuchukua watalii USA mpaka Tz.
 
Mkuu acha tu.
Ajira hakuna, tunaletewa mandege ya ajabu ajabu
 
Ningependekeza inunuliwe ndege kuuuuubwa, isaidie kuleta watalii for direct flight na kuongeza mapato ya nchi yetu ili tuwekeze kwenye Huduma za maji, umeme, mikopo kwa vijana n.k.

Namaanisha kuwa kusudio la serikali ni sahihi.
 
Hata ukipendekeza ni sawa unaoga kwenye tope

Mtu hasikii wala hashauriki hiyo midege ndio furaha yake
akikaa akisimama
akilala akiamka
akila akitembea
anawaza Dreamliner kama vile anaiona pale KIA
inapaa utamwambia eti kuna watz huku wanashida na maji!!??
Siku zote hawa watu ambao huwa wanajidai eti
katoka familia sijui ya mkulima huwa wanabadilika
na hawasaidii chochote.
ananunua ndege ambazo watanzania baadhi wenye maisha ya juu ndo watapanda
lakini si mtanzania wa maisha ya chini ambae hata panadol
inamshinda kununua,.

Hata hivyo hawa watanzania wa chini wakati mwingine
hawana akili anasumbuka dawa, maji shidah lakini
Ikifika wakati wa kampeni ndio utaona ujinga wake,
Na mimi nasema acha waisome namba.
Wewe Magu katununulie Dreamliner allah...!!!.
 
Mimi ningenunua zana za kilimo na kuwagawia bure au kuwakopesha kwa bei poa wananchi wa vijijini. Na hapa sikusudii meno ya kulimia(watu watalimia meno).

Ni wakati sasa nguvu na nyenzo zielekezwe kuboresha maisha ya walalahoi wa vijijini nchini ili kupunguza kasi ya wadanganyika kuhamia mijini na kuongeza tatizo la ukosekanaji wa kazi, uajiri au mitaji ya kujiajiri.
 
Mimi bora Q500 MISSILE DEFENCE YA RUSSIA ILE MPYA KABISA ILI MALAWI WAKILETA ZAO TUKACHUKUE KANCHI HAKO.
 
Maji ya nini....mbona hili swala liko miaka nenda miaka rudi.na siku zote Wakubwa wale kule ndani wanalalamika wanapiga vijembe halafu wanunga mkono hoja....Mutapata maji kweli kwa namna hiyo....TUBADILIKE..
 
Ningependekeza inunuliwe ndege kuuuuubwa, isaidie kuleta watalii for direct flight na kuongeza mapato ya nchi yetu ili tuwekeze kwenye Huduma za maji, umeme, mikopo kwa vijana n.k.

Namaanisha kuwa kusudio la serikali ni sahihi.
Kwani watalii wamekosa ndege za kija huku?
 
Hivi kama Mkulu ndiye anayepanga bajeti almost yote ya nchi hii kuna haja gani ya kuwa na Bunge la Bajeti linalokaa zaidi ya miezi 2 kule Dodoma huku 'likatafuna' mabilioni ya shilingi wanazolipana posho?!

Tulijionea majuzi alipokwenda pale Ukonga Magereza akiahidi kuwapelekea bilioni 10!

Tulijionea mwezi June mwaka huu, Mkulu alipoenda kwa Mzee wa Upako akimuahidi kumtengenezea barabara ya lami toka barabara ya Mandela hadi kanisani kwake!

Na hivi sasa tumemsikia Mkuu akitamba kuwa tayari keshanunua ndege 6 za Bombardier na hiyo 'babu' kubwa ya Boeing Dreamliner ya bilioni 600!

Sasa kama bajeti yote ya nchi inapangwa na Mkuu, tuna haja gani ya kuendelea 'kuteketeza' mabilioni ya shilingi kuwalipa wabunge wakati bajeti yao haina maana tena?
 
Ningependekeza fedha bilioni 600 zitumike katika hili

1. Kuboresha miundombinu ya Dar kwa kujenga barabara za mwendokasi nyingine katika sehem zenye msongamano.

. AU
2. Ningetumia fedha hizo kukopesha vijana wenye mpango mkakati wa biashara kuweza kujiajiri wenyewe.

AU
3. Ningesambaza umeme katika sehem ambazo umeme haujafika

AU
4. Ningesambaza huduma za Maji katika sehem kame

. AU
5. Ningeimarisha shule za msingi kwa kukarabati miundombinu.

Wewe unapendekeza nini?

Mkuu naona unapoteza muda kujadili vitu vya kusadikika. Umeelezwa hiyo hela imetumika kununua ndege sasa unataka mapendekezo yapi sababu najua HAYATEKELEZEKI.
 
Pekekeen wanafunzi boom
Hali mbaya watu washa anza biashara isyo na matangazo
 
Back
Top Bottom